THE BIG SHOW
JF-Expert Member
- Feb 28, 2012
- 16,950
- 13,527
Friends and Enemies,
Katika kile kinachoonekana kuwa ni vita dhidi ya rasimali za nchi kama wenyewe wanavyosema, ameibuka Askofu Mstaafu Stephen Munga ambaye ni Askofu Mkuu Mstaafu dayosisi ya kaskazini mashariki.
''Yupo Mfalme wa Wafalme, tuwe makini na kauli zetu, kama umesahau Jana ukumbuke kuwa ipo kesho'' hayo ni baadhi ya maneno yake ambayo ameyaelekeza katika kuinyooshea kidole Serikali katika utendaji wake.
Huu ni muendelezo ule ule wa kauli za watu kama kadinali PENGO na wenzao katika kuisakama serikali.
Tulishasema na tutazidi kuwaambia kuwa serikali haiwezi kuendeshwa Kwa vitisho vya maaskofu wala kwa utitiri wa kauli zao. Serikali inaongozwa Kwa taratibu, kanuni na sheria, uhuru ambao leo wanao hawa wanaojiita maaskofu ambao miaka mitatu iliyopita hawakuwa nao. Wajifunze kuutumia vizuri na siyo katika kuligawa Taifa na kuishambulia Serikali.
Serikali iwe makini na hao maaskofu na pale inapobidi isiogope Wala kusita kuwachukulia hatua, miaka mingi wamezoea kudeka na kudekezwa sasa ifikie wakati watambue kuwa zama zimebadirika, zile zama za kuwaungamia na kudeka deka kwao zimefikia mwisho.