LGE2024 Maazimio ya mkutano wa Kamati Kuu ya CHADEMA baada ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Kilichosemwa hapo ni msimamo wa chama, kupitia kamati kuu.
Mbowe ni muwasilishaji tu..
Hivyo basi kama ni matusi tukana kamati KUU.
 
Hapo kwenye namba 7 neno wananchi lingeondolewa na kuwekwa wanachama wa chadema!
Yaani mbowe anajiaminisha na kutaka kutuaminisha kwamba hata wanachama wa CCM na wale wasiokuwa na vyama kama mimi kwamba tunaweza shawishika kuacha kutoa ushirikiano kwa wenyeviti na wajumbe waliotangazwa kuwa wameshinda ! Halafu ni ushirikiano gani anaokusudia ?! Kwa maana katika baadhi ya mambo ukiacha kutoa ushirikiano kwa kiongozi unajidhuru wewe mwenyewe kwa kuwa kuna mambo kadhaa huwezifanikiwa bila kumshirikisha mwenyekiti kwa sababu raia ndio wanamhitaji mwenyekiti na sio mwenyekiti anayewahitaji raia.
Mwenyekiti anahitaji ushirikiano wa wananchi wakati wa kampeni na wakati wa kupiga kura ili wampe kura!.
Akishakalia kiti cha uenyekiti hapo wananchi ndio huhitaji ushirikiano wa mwenyekiti ili awape maendeleo aliyowaahidi wakati wa kampeni.
 
Too pety! Press ilipaswa kufanywa na John Mrema tu au John Mnyika tu au John Pambalu tu. Yaan mwenyekiti anakuja na press uchwara ya namna hii, too pety.
 
Kumbe wewe hapo umeona tatizo ni Mbowe?

Hayo ni maazimio ya kamati kuu ya chama, siyo ya Mbowe peke yake.

Umeelewa Happy?
 
Anasema ukitaka mhuri wa mwenyekiti mtaani ususie kama ni dili uiache πŸ˜‚πŸ˜‚
 
2. Kamati Kuu inalaani mauaji, vipigo/kujeruhi na ukamataji kwa wagombea, mawakala, viongozi na wanachama kabla, wakati na baada ya uchaguzi uliofanywa na Jeshi la Polisi.
Azimio hili lilipaswa liseme,

Kamati Kuu inalaani mauaji, vipigo/kujeruhi na ukamataji kwa wagombea, mawakala, viongozi na wanachama kabla, wakati na baada ya uporaji na uhalifu wa kiuchaguzi uliofanywa na Jeshi la Polisi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…