LGE2024 Maazimio ya mkutano wa Kamati Kuu ya CHADEMA baada ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

LGE2024 Maazimio ya mkutano wa Kamati Kuu ya CHADEMA baada ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Siku nimesoma kitabu cha Prof. Issa Shivji cha PanAfricanism or Pragmatism nilishtuka sana..

Kuna sehemu anasema ''...vijana wawili wa idara ya usalama walioiba nyaraka toka ikulu ya zanzibar na kumpelekea Nyerere walikuwa ni Hassan na Maalim Seif Sharif Hamad''

So maalimu wa ana Agent till death, ila kwa Mbowe hapana, jamaa anapambana kikwelikweli.
Fuatilia kipindi ccm wananunua wabunge na madiwani wa CDM,tone yake,body language I mean facial expression, hakuakisi uzito wa lile jambo wakati wanachama walikwa na hasira kuna wengine walitamani hata kuwakata mapanga wale waliojiuza ila yeye alikuwa normal sana tena sanaaaa.
 
Hapo kwenye namba 7 neno wananchi lingeondolewa na kuwekwa wanachama wa chadema!
Yaani mbowe anajiaminisha na kutaka kutuaminisha kwamba hata wanachama wa CCM na wale wasiokuwa na vyama kama mimi kwamba tunaweza shawishika kuacha kutoa ushirikiano kwa wenyeviti na wajumbe waliotangazwa kuwa wameshinda ! Halafu ni ushirikiano gani anaokusudia ?! Kwa maana katika baadhi ya mambo ukiacha kutoa ushirikiano kwa kiongozi unajidhuru wewe mwenyewe kwa kuwa kuna mambo kadhaa huwezifanikiwa bila kumshirikisha mwenyekiti kwa sababu raia ndio wanamhitaji mwenyekiti na sio mwenyekiti anayewahitaji raia.
Mwenyekiti anahitaji ushirikiano wa wananchi wakati wa kampeni na wakati wa kupiga kura ili wampe kura!.
Akishakalia kiti cha uenyekiti hapo wananchi ndio huhitaji ushirikiano wa mwenyekiti ili awape maendeleo aliyowaahidi wakati wa kampeni.
Miaka mitano hatukutoa ushirikiano wowote kwa Wenyeviti wa Mitaa mbona hatujadhurika na tunaendelea kupeta.
 
Fuatilia kipindi ccm wananunua wabunge na madiwani wa CDM,tone yake,body language I mean facial expression, hakuakisi uzito wa lile jambo wakati wanachama walikwa na hasira kuna wengine walitamani hata kuwakata mapanga wale waliojiuza ila yeye alikuwa normal sana tena sanaaaa.
I see.
 
Miaka mitano hatukutoa ushirikiano wowote kwa Wenyeviti wa Mitaa mbona hatujadhurika na tunaendelea kupeta.
Na ilivyokuwa hamkutoa ushirikiano wowote kwa hao wenyeviti wa mtaa , HAO WENYEVITI WALIDHURIKA AU KUPUNGUKIWA NINI KWA KUKOSA USHIRIKIANO WENU?!.
Hawakudhurika wala kupungukiwa chochote kwa sababu nchi inao raia wazalendo kama sisi ambao tuliwapa ushirikiano na tutaendelea kuwapa ushirikiano daima.
NYINYI ENDELEENI KUSUSA NA SISI TUTAENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA VIONGOZI WA NCHI YETU.
 
Anasema ukitaka mhuri wa mwenyekiti mtaani ususie kama ni dili uiache 😂😂
Wanachokifanya chadema ni michezo ya kitoto.
Wao wasusie tu, sisi tutaendelea kutoa ushirikiano kwa viongozi wetu wa mitaa,Kata,wilaya ,mikoa na na taifa kwa ujumla!.
 
MAAZIMIO YA KAMATI KUU

Baada ya kutafakari matukio hayo na mengine, Kamati Kuu ya Chama imeazimia mambo yafuatayo;

1. Kamati Kuu inatamka kwamba kilichotokea tarehe 27 Novemba, 2024 hakukuwa na uchaguzi halali, huru na haki bali uporaji na uhalifu wa kiuchaguzi.

2. Kamati Kuu inalaani mauaji, vipigo/kujeruhi na ukamataji kwa wagombea, mawakala, viongozi na wanachama kabla, wakati na baada ya uchaguzi uliofanywa na Jeshi la Polisi.

3. Kamati kuu inawapongeza wagombea wote waliojitokeza kugombea kupitia Chadema.

4. Kamati kuu inawapongeza wadau wote ambao wamejitokeza hadharani na kulaani uchafuzi huu ambao ni hatari kwa uhai wa taifa letu, tunaendelea kutoa rai kwa wadau wengine kusema hadharani misimamo yao kuhusu uchaguzi huu; Aidha tumesikitishwa na baadhi ya taasisi na watu ambao wameendelea kupongeza uchaguzi huo ambao unahatarisha uhai wa taifa letu.

5. Kamati Kuu imethibitisha bila shaka yoyote kwamba hakuna utashi wa kisiasa (political will) kutoka kwa Rais, Viongozi na mfumo mzima wa Serikali ya CCM juu ya uboreshaji wa mifumo ya uchaguzi ili kuleta chaguzi huru, haki na zinazoaminika nchini. Imethibitika kuwa kauli zao haziaminiki tena hivyo ni lazima pawepo na maboresho ya kisheria juu ya mifumo ya uchaguzi nchini.

6. Kamati Kuu inatoa wito kwa wadau wote nchini wakiwemo vyama vya siasa, Taasisi za dini, makundi ya kijamii,Asasi za kiraia,wasomi,wakulima ,wafanyabiashara, watu mashuhuri katika jamii na wananchi wote kuunganisha nguvu zza pamoja ili kutafuta na kudai mifumo huru ya uchaguzi nchini.

7. Kwa kuwa, wananchi wanawafahamu viongozi waliotangazwa kwa wizi, bila kushinda; Kamati Kuu inawahimiza kwamba, wananchi wa maeneo hayo kuwanyima ushirikiano viongozi wote wa serikali za mitaa na watendaji wa mitaa/vijiji na kata walioshiriki kuharamisha uchaguzi wa tarehe 27 Novemba, 2024.

8. Kamati Kuu imeazimia kuendeleza vuguvugu la kudai Katiba Mpya na kushinikiza kufanyika maboresho ya sheria na mifumo ya Uchaguzi itakayowezesha uwepo wa Uchaguzi Huru na wa Haki kuelekea 2025.

9. Kamati Kuu itaendelea kushinikiza kupatikana Tume Huru ya Uchaguzi na yenye watumishi wake walioajiriwa na Tume ambao watasimamia Uchaguzi wowote nchini kwa mujibu wa sheria badala ya kuendeleza mfumo uliopo sasa wa kuazima watumishi wa Ofisi ya Rais (TAMISEMI) kusimamia chaguzi.

10. Kamati kuu imeazimia kuwa Jumuiya ya kimataifa na taasisi zake wachukue hatua dhidi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuminya Demokrasia na kutokuwepo kwa uchaguzi huru, haki na za kuaminika nchini.
View attachment 3173665
Kikubwa nilichoelewa Mbowe bado ni kijana mbichi Uenyekiti haachii ng'ooo! Tumpigie makofi mwenyekiti wetu wa maisha💃💃💃
CHADEMA ni ya Mbowe na anatamba nayo🤣🤣🤣
 
Mbowe apumzike aachie na wengine.

Aina ya siasa za Mbowe zimeonyesha kugonga mwamba mbele ya CCM.

Ni wakati wa yeye kukaa pembeni abaki kama mshauri mkuu, siasa za aina yake kuitoa CCM ni ndoto maana hawako tayari kutoka kwa mtindo huo.

Mimi sikuamini kama wangeshiriki uchaguzi mwingine wowote bila katiba mpya na tume huru baada ya upuuzi mkuu wa 2020.

Pia kuhusu maridhiano ya Samia ule ulikuwa ni utapeli, huwezi kufanya maridhiano wakati kuna wanachama wako wengi tu wako gerezani kwa kesi za kubumba za kisiasa kutokana na upuuzi wa 2020 .
 
hakuna jipya lililoongelewa zaidi ya ku copy na ku paste ya nyma ameshachoka huyo awaachie wenye nguvu najuwa hata wewe unajuwa lakini kwakuwa ni chawa wake huwezi kukubali
Mimi najua ila siyo najuwa. Nchi ina Wanyamulenge kibao.
 
Ndio nini hiki?😂😂😂

Mbowe hana jipya yani it was predictable hii press atasema nini. As usual wapambe wake watendelea kuimba nyimbo za kusifu na kuabudu wakiamini wanampenda sana na wanakipenda sana chama wanalinda chama.

Lakini ukweli unazidi kuonekana kuwa Mbowe kaishiwa kachoka chama kinahitaji fresh mind.
Chawa happyxxx ktk frustations za kufa mtu..

Au umetoka usingizini, ukakuta notification ya mada hii na bila hata kufikiri vyema ukajiandikia zako...?

Chawa sometimes punguzeni bangi mnazokula kutoa aibu ili mkateke na kutesa raia wenzenu bila sababu...!!

Mbowe hana jipya!!?............ Huko kwenu mna jipya gani by the way...?
 
Ndio nini hiki?😂😂😂

Mbowe hana jipya yani it was predictable hii press atasema nini. As usual wapambe wake watendelea kuimba nyimbo za kusifu na kuabudu wakiamini wanampenda sana na wanakipenda sana chama wanalinda chama.

Lakini ukweli unazidi kuonekana kuwa Mbowe kaishiwa kachoka chama kinahitaji fresh mind.
Wewe una jipya gani??????
 
Mzee Warioba alitangulia kuwapa desa lakini bado wamefeli kwa kuja na maazimio yasiyo na nguvu yoyote

Warioba aliposema waziri wa TAMISEMI ameenda kinyume na maagizo na maelekezo ya viongozi wa CCM walitakiwa watembee humo humo.

Warioba ni mtu mkubwa sana, ni mwana CCM mkongwe. Kutamka yale aliyotamka kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa ilikuwa ni credit kwa watu wote wapenda haki na wapinzani walitakiwa kupenya humo humo

Warioba kusema serikali imeenda kinyume na chama cha CCM kwa kuengua wagombea na kuandikisha wapiga kura feki na kupiga kura feki CHADEMA walikuwa wamepewa desa la maana kutembea nalo
 
CCM hawataki ustaarab; wana siasa za kilaghai hawa dawa yao ni kwenda nao ki mpera mpera...yaani weka ugoko weka chuma ni kuwapelekesha mwanzo mwisho - hiyo number 7 na 10 itawafaa saana.
 
Ni msingi umeweka kama adidu rejea kwa siku zijazo . Nawapongeza Sana chadema kwa kufanya press hii . Aidha chadema wanatunza amani ya nchi kuliko mjuavyo . Wanachofanyiwa hakivumiliki sehemu nyingine . Ila Mungu anaenda kuwagonganisha ndani ya chama Chao na chadema wataipenda baadaye ,mark my words
 
Kamati imekubal
MAAZIMIO YA KAMATI KUU

Baada ya kutafakari matukio hayo na mengine, Kamati Kuu ya Chama imeazimia mambo yafuatayo;

1. Kamati Kuu inatamka kwamba kilichotokea tarehe 27 Novemba, 2024 hakukuwa na uchaguzi halali, huru na haki bali uporaji na uhalifu wa kiuchaguzi.

2. Kamati Kuu inalaani mauaji, vipigo/kujeruhi na ukamataji kwa wagombea, mawakala, viongozi na wanachama kabla, wakati na baada ya uchaguzi uliofanywa na Jeshi la Polisi.

3. Kamati kuu inawapongeza wagombea wote waliojitokeza kugombea kupitia Chadema.

4. Kamati kuu inawapongeza wadau wote ambao wamejitokeza hadharani na kulaani uchafuzi huu ambao ni hatari kwa uhai wa taifa letu, tunaendelea kutoa rai kwa wadau wengine kusema hadharani misimamo yao kuhusu uchaguzi huu; Aidha tumesikitishwa na baadhi ya taasisi na watu ambao wameendelea kupongeza uchaguzi huo ambao unahatarisha uhai wa taifa letu.

5. Kamati Kuu imethibitisha bila shaka yoyote kwamba hakuna utashi wa kisiasa (political will) kutoka kwa Rais, Viongozi na mfumo mzima wa Serikali ya CCM juu ya uboreshaji wa mifumo ya uchaguzi ili kuleta chaguzi huru, haki na zinazoaminika nchini. Imethibitika kuwa kauli zao haziaminiki tena hivyo ni lazima pawepo na maboresho ya kisheria juu ya mifumo ya uchaguzi nchini.

6. Kamati Kuu inatoa wito kwa wadau wote nchini wakiwemo vyama vya siasa, Taasisi za dini, makundi ya kijamii,Asasi za kiraia,wasomi,wakulima ,wafanyabiashara, watu mashuhuri katika jamii na wananchi wote kuunganisha nguvu zza pamoja ili kutafuta na kudai mifumo huru ya uchaguzi nchini.

7. Kwa kuwa, wananchi wanawafahamu viongozi waliotangazwa kwa wizi, bila kushinda; Kamati Kuu inawahimiza kwamba, wananchi wa maeneo hayo kuwanyima ushirikiano viongozi wote wa serikali za mitaa na watendaji wa mitaa/vijiji na kata walioshiriki kuharamisha uchaguzi wa tarehe 27 Novemba, 2024.

8. Kamati Kuu imeazimia kuendeleza vuguvugu la kudai Katiba Mpya na kushinikiza kufanyika maboresho ya sheria na mifumo ya Uchaguzi itakayowezesha uwepo wa Uchaguzi Huru na wa Haki kuelekea 2025.

9. Kamati Kuu itaendelea kushinikiza kupatikana Tume Huru ya Uchaguzi na yenye watumishi wake walioajiriwa na Tume ambao watasimamia Uchaguzi wowote nchini kwa mujibu wa sheria badala ya kuendeleza mfumo uliopo sasa wa kuazima watumishi wa Ofisi ya Rais (TAMISEMI) kusimamia chaguzi.

10. Kamati kuu imeazimia kuwa Jumuiya ya kimataifa na taasisi zake wachukue hatua dhidi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuminya Demokrasia na kutokuwepo kwa uchaguzi huru, haki na za kuaminika nchini.
View attachment 3173665
kamati kuu imekubaliana ya kwamba Mzee Mbowe ataendelea kuwa Mwenyekiti hadi hapo atakapoamua vinginevyo
 
Back
Top Bottom