Mabachela: Ni chakula gani kigumu kupika geto?

Mandazi na chapati wakuu nimejaribu kukaa karibu na mama lkn kila nikienda getoni lazma nikosee
 
Mnhh. Kuna demu alikuja ghetto nikamuomba anipikie hizo tambi, kwa kweli kilichotokea nilienda kununua pakti mpya nkatoa kitu mwenyewe
 
Tuma kitchen foil, mifuko ya plastic sio mizuri kwa afya
 
Nikupe recipe rahisi kabisa. Chemsha nyama ama kuku, weka kando. Kaanga kitunguu, kikiwa brown tia binzari kidogo na nyama kaanga kiasi then weka nyanya chache. Zikiiva tia supu ya kutosha na ndizi zako zilizomenywa na kuoshwa. Zikikaribia kuiva weka nazi ya azam na punguza moto ili nazi isikatike.

Voilaaaa[emoji13]
Me hadi Leo Natamani Ndizi Nyama, Ila kupika Issue

Ubachelor Shida Sana.
 
Au achemshe nyama
Akatie kila kitu
Aweke na ndizi kabisa.
 
Hii inakuwa na kaharufu flani ka nyanya ambazo hazijaiva vizuri inanikera.

Kama nyama ni nyingi ya kutodha, ndizi chuku chuku huwa tamu pia kwa sababu ya supu nzito. Ila isiwekwe nyanya kabisa, carrots, hoho na vitunguu vinatosha
Au achemshe nyama
Akatie kila kitu
Aweke na ndizi kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…