Mabachela: Ni chakula gani kigumu kupika geto?

Mabachela: Ni chakula gani kigumu kupika geto?

Kiberiti Kidogo

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2017
Posts
575
Reaction score
918
Nina imani mabachela tuko wengi sana humu.

Katika suala la kupika na kuosha vyombo huwa ni habari ingine. Vipi wewe mkuu ni msosi gani kuupika au kuuandaa huwa unakupa mawazo sana japo unaupenda. Na ukiula mahala unahisi umekosewa kupika sio kama ungeupika japo hujawahi kuutest geto.

Mimi bana WALI naupenda ila kuuandaa hadi utoke ni hatari sana. Halafu nikiwa nakula kitaa huwa mwepesi sana kuwalaumu wahudumu wali haujaiva au wamepika bokoboko au una mawe.

Wewe je msela wa geto nini kinasumbua jikoni?
 
Kitu ambacho mabachela wengi wanachokiweza ni kuchemsha chai ya rangi na kupika tambi tu.
Kataeni au mkubali.
% kubwa ya wanaomudu kupika baadhi ya vyakula ni aidha wale waliokulia kwa dada zao au walioondoka kwenda kuanza maisha wakiwa wametoka makwao (kwa wazazi wao) wakiwa 22-25+.
Waliobaki wote ni tambi na chai ya rangi tu
 
Mzazi kitu chapati aiseeh hii theory zake zote kichwani nimezipiga kinoma kwa Bi Mkubwa mara nyingi alikuwa ananianzishia kuchanganya madude mi namalizia kuzisukuma kwenye kibao chake na kuziweka kwa moto.


Kila day nataka kujilipua kigetogeto nikamate ngano toka mwanzo hadi mwisho.

Ila day tu soon nitajilipua mzazi.
 
Back
Top Bottom