Mabachela: Ni chakula gani kigumu kupika geto?

Mabachela: Ni chakula gani kigumu kupika geto?

Aisee ni mseto wa choroko na mchele.... ila najua kuupika kwa uzuri kabisa, naukunia nazi kwa uzuri kabisa..
Changamoto ipo kwenye maandalizi yake tu mpaka kuja kuula masaa ya kutosha yanatumika jikoni.
Ukiupata na chuzi la ngisi wa nazi hatari we jamaa... usithubutu. Nimeupika wiki iliyopita....

Post sent using JamiiForums mobile app
 
1. Chapati
Napenda sana chapati ila dah process ya kupika chapati inahitaji uvumilivu sana.

2. Makande
Sio siwezi kuyapika, ila nayo process yake siiwezi ya kuyabadnika halafu usicheze mbali kila wakati kuongeza maji. Sikumbuki ni mara ngapi nikiwa mdogo niliunguza makande kwa kucheza. Mpaka leo naogopa kujaribu

3. Pilau
Dah kupika pilau ghetto ni another level aisee! Hapo ni sawa na kusema hutaki kuoa kabisa. Hapana..hii naiweza ila nadhani kisaikolojia tu nahisi nikifikia level ya kupika pilau peke yangu nitakuwa nimeshindikana.

4. Tambi
Sio ngumu, ila mpaka leo sijawahi kujua vipimo sahihi vya tambi. Sometimes unajikuta umepika nyingi sometimes umepika kidogo alimradi tu vipimo vikosewe tu.
 
Ile Pilau niliyopika siku ile ya Ckrismass Mungu mwenyewe ananajua. Isingekuwa majirani kuokoa jahazi kwa kuleta kihotpot cha pilau makinikia nilikuwa naumbuka siku ile.
 
Tambi nayo ndo changamoto
Kwang kupika aiseee!!
Nazpenda lakin naishia tuu
Kudoea kwa ndugu zang
Waislam wakat wakiwa kwenye mfungo

[Color= yellow]Triple A[/color]
Hahahahahah
Hatare.
Tambi ni maji yako na mixture ya chumvi na sukari tu mkuu.
 
Tambi nayo ndo changamoto
Kwang kupika aiseee!!
Nazpenda lakin naishia tuu
Kudoea kwa ndugu zang
Waislam wakat wakiwa kwenye mfungo

[Color= yellow]Triple A[/color]
Hahhahha
Pole sana mkuu.
Tambi ni maji yako tu na mixture ya sukari na chumvi.
Labda usiweke vile vikorombwezo.
 
Mim nina miaka 28...nimeanza kukaa ghetto tangu 2014....baada ya kumaliza chuo na napika kila kitu kwa ufasaha mpaka shemej yenu akija kunitembelea still napika mimi yeye anajifunza ila sijaanza bado kupika vitu kama sambusa maandaz na vyapati...ila pilau wali ndiz ugali na mboga zote nashusha tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Aiseee hongera sana....kama unamudu kupika vyote hivo.
Maana kuna wanawake wengine hivo unavyovipika hawaviwezi.
Nakumbuka mchaga wangu alinikaribisha nyumbani kwake alipika samaki wa nazi na wali wa basmat.
Ilibidi tule tu chipsi aisee
Nyanya chungu ziko kushoto, bamia limesambaa hujui mbegu zi kwapi, gamba la nje li kwapi, vitunguu vinapiga mbizi katikati ya nazi iliyojichuja, anasema alitia tui 3 kwa mpigo.
Nyanya zimesimama kama ziko sokoni.
Vitunguu swaumu anasema alivisaga na maganda yake.
Huo wali sasa...hahahhaha
alipikia kikombe kimoja cha maji maana alijua basmat inaiva haraka.
Anapakua chakula, chakula kinatuangalia macho makavu.
Aliagiza chipsi kwa aibu

Ila nilikaa nae chini nikamfundisha kupika vyakula vizuri.
Sasa hivi sina wasiwasi, naweza rudi misele nikakuta kaangusha biriani la kuku na linalika fresh tu.
Anakuna mpaka nazi, na kuandaa mpaka manda za sambusa.
Ubachela ni kazi aisee.
 
Kuosha vyombo ndo sipendi kabisa, habar ya kwenda sokon ndo staki kusikia kabisa
 
1. Chapati
Napenda sana chapati ila dah process ya kupika chapati inahitaji uvumilivu sana.

2. Makande
Sio siwezi kuyapika, ila nayo process yake siiwezi ya kuyabadnika halafu usicheze mbali kila wakati kuongeza maji. Sikumbuki ni mara ngapi nikiwa mdogo niliunguza makande kwa kucheza. Mpaka leo naogopa kujaribu

3. Pilau
Dah kupika pilau ghetto ni another level aisee! Hapo ni sawa na kusema hutaki kuoa kabisa. Hapana..hii naiweza ila nadhani kisaikolojia tu nahisi nikifikia level ya kupika pilau peke yangu nitakuwa nimeshindikana.

4. Tambi
Sio ngumu, ila mpaka leo sijawahi kujua vipimo sahihi vya tambi. Sometimes unajikuta umepika nyingi sometimes umepika kidogo alimradi tu vipimo vikosewe tu.
Pole sana mdogo wangu.
Uzuri wa vitu hivi uone kwa macho vikipikwa, na sio ku-google.
Maana kuna wengine wana-google mapishi.
Mimi hakuna chakula nisichokiweza, labda kivumbuliwe jana.
Msosi unaonipa shida yaani siupatii kivile japo unalika ni kupika Tandoori chicken na beef biriani lenye biringanya.
 
Aisee ni mseto wa choroko na mchele.... ila najua kuupika kwa uzuri kabisa, naukunia nazi kwa uzuri kabisa..
Changamoto ipo kwenye maandalizi yake tu mpaka kuja kuula masaa ya kutosha yanatumika jikoni.
Ukiupata na chuzi la ngisi wa nazi hatari we jamaa... usithubutu. Nimeupika wiki iliyopita....

Post sent using JamiiForums mobile app
Usintamanishe wewe looh kesho nitapika inshaallah[emoji39] [emoji39] [emoji39] [emoji39] [emoji39] [emoji39]
 
Hahahahaha acha kabisa kuna yale marangi rangi yale acha siku moja nichukue nikaweka kwenye wali nikijifanya fundi wa kujaribu vitu...aisee niliendesha balaaa
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom