Mabadiliko Baraza la Mawaziri: Doto Biteko ateuliwa kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati. Makamba Mambo ya Nje, Pindi Chana Katiba na Sheria

Mabadiliko Baraza la Mawaziri: Doto Biteko ateuliwa kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati. Makamba Mambo ya Nje, Pindi Chana Katiba na Sheria

Mnaweza kufikiri ameliwa kichwa au amepotezwa kumbe mwenzenu ndo kawekwa kwenye njia ya kuelekea kwenye kile akitakacho..

January Yusufu Makamba ambition yake ni kuwa Rais wa JMT

Kupelekwa wizara ya Mambo ya nje & Ushirikiano wa Afrika Mashariki ni maandalizi..

Huyu ndiye mgombea U - Rais ajaye (2025) wa CCM. Hiyo wizara ndiyo huwa inatoa Marais kwa upande wa CCM..
Membe alikuwa wizara gani?
 
1. Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Doto Biteko (MKRISTO)kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati. Awali alikuwa Waziri wa Madini.

2. Amemteua January Makamba (MUISLAM) kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Awali alikuwa Waziri wa Nishati.

3. Amemhamisha Balozi Pindi Chana (MKRISTO) kuwa Waziri wa Katiba na Sheria. Awali alikuwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo.

4. Amemhamisha Steven Byabato (MKRISTO)kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Awali, Byabato alikuwa Naibu Waziri wa Nishati.

5. Amemteua Jerry Silaa (MKRISTO)kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Silaa ni Mbunge wa Ukonga, Dar es Salaam.

6. Rais amemteua Anthony Mavunde(MKRISTO) kuwa waziri wa madini, mwanzo alikuwa naibu waziri wa kilimo.

7. Prof Makame Mbarawa (MUISLAM) aliyekuwa waziri wa ujenzi na uchukuzi amekuwa waziri wa uchukuzi.

8. Innocent Bashungwa (MRISTO)amekuwa waziri wa ujenzi, mwanzo alikuwa waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa.

9. Godfrey Kasekenya (MKRISTO) aliyekuwa Naibu waziri wa Ujenzi na uchukuzi ameteuliwa kuwa Naibu waziri wa Ujenzi

10. Alexander Mnyeti (MKRISTO) ameteuliwa kuwa Naibu waziri wa Kilimo

11. David Mwakiposa (MKRISTO)Kihenzile ameteuliwa kuwa Naibu waziri wa Uchukuzi. Ni mbunge wa Jimbo la Mufindi

12. Judith Kapinga (MKRISTO) ameteuliwa kuwa Naibu waziri wa nishati, ni mbunge wa viti maalum Ruvuma.

13. Dunstan Kitandula (MKRISTO)ameteuliwa Naibu Waziri wa maliasili na Utalii, ni mbunge wa Mkinga

14. Stergomena Tax (MKRISTO)amehamishwa wizara ya mambo ya Nje kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

15. Angellah Kairuki (MKRISTO)amehamishwa kutoka TAMISEMI na kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii

16. Dkt. Damas Ndumbaro (MKRISTO) amehamishwa kutoka Wizara ya Katiba ba Sheria na kuwa Waziri wa Utamaduni
Umezijuwa vipi dini za hawa wateule?
 
Hakuna ujumbe wowote, hata ukimtazama Kassim Majaliwa unamuona kuwa yu mgonjwa-gonjwa. Hana afya njema, ni lazima apunguziwe mzigo, ana "underperform".

Kama si maradhi physically basi ana "depression".
Inaelekea una ugomvi mkubwa sana na Mh. PM au pana kitu alikuahidi huko ujanani kisha akakutelekeza?
 
Hakuna ujumbe wowote, hata ukimtazama Kassim Majaliwa unamuona kuwa yu mgonjwa-gonjwa. Hana afya njema, ni lazima apunguziwe mzigo, ana "underperform".

Kama si maradhi physically basi ana "depression".
We limama ni lichawi? Mbona unambo ya kijinga namna hii?
 
Hii nchi tunahangaika sana. Sasa kama tokea enzi za jiwe miaka nane iliyopita staili ni hihii kweli Hamna la kujifunza ni mbinu ambayo haisaidii. Sasa Raisi anasema kwa mfano mkuu wa mkoa Hana mpango mkakati wa kuusaidia mkoa, Sasa mkuu wa mkoa leo umempeleka morogoro wakati bado hata hajatembelea wilaya zake ushamhamisha na huko unakompeleka hajakaa miezi SITA tayari ushamhamisha Sasa hapo atapanga mipango gani ya maendeleo kwenye mkoa
 
Reform kazini, hata mpira wakicheza kuna muda coach anabadili "formation" ndiyo maana halisi ya ku reform.

Ofisi ya Rais ni kubwa kuliko mnavyodhania.

Hiki cheo cha unaibu waziri mkuu kilianzia wakati wa mzee Rukhsa, mama sasa kakirudisha tena. Kuna sababu za muhimu sana tena sana, kuliko unavyofikiria.
Hapo umeanza kuongea, lakini hujamalizia bado japo umegusia kidogo!! Wakati wa mzee Mwinyi, mawaziri wal;ianza kumlalamikia Mrema kuwa anawaingilia kwenye ofisi zao, wakati huo Mrema akiea waziri wa mambo ya ndani!! Mrema ilikuwa akinusa harufu ya ufisadi kwenye wizara yoyote alikuwa anaingia huko kuhoji kama waziri wa mambo ya ndani!! Kwa kuwa Mrema alikuwa anafanya kazi njema ya kizalendo, na ili kumpa rungu litakalohalalisha yeye kuingia wizara yeyote, ndipo Mwinyi akalazimisha kuunda nafasi ya naibu waziri mkuu (ambayo kimuundo haipo) na kumpa nafasi hiyo Mrema ili kufumba vinywa vya mawaziri wanaodai kuingiliwa!!! Wote walinywea na Mrema alifanya kazi iliyoyukuka sana!!

Sasa tuambie kuna umuhimu upi kwa sasa ulio wazi kwa kila mtu?
 
Back
Top Bottom