Mabadiliko Baraza la Mawaziri: Doto Biteko ateuliwa kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati. Makamba Mambo ya Nje, Pindi Chana Katiba na Sheria

Mabadiliko Baraza la Mawaziri: Doto Biteko ateuliwa kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati. Makamba Mambo ya Nje, Pindi Chana Katiba na Sheria

Huyu ka alivyokuwa Magufuli ana asili ya nchi jirani ya Rwanda, sijui kagame anatumia ujanja gani kupenyeza watu wake kwenye safu ya uongozi wa nchi hii
Ndo kama waarabu wanatumia kufanya faiza foxy kuamini Tanzania sisi wakatoliki tunachukia uislamu na mama kaja kuwakomboa .Azam anawekeza mpra tuu na buku buku maskin.ushadkia katiliki inatoa buku
 
Kumbe jerry silaa amewekwa kukamilisha hii mission ya DP world

Anaweza kujiona ameshinda kwa sasa lakini mbele ya safari mambo yatamuendea mrama pale vizazi na vizazi vitakapomlilia
 
Attachments

  • IMG_20230907_153158.jpg
    IMG_20230907_153158.jpg
    1.3 MB · Views: 4
Nikwambie Biteko, baada ya Kalemani kuonekana kizingiti kwa mafisadi pale Nishati alipelekwa Makamba Kwenda kufanikisha misheni,ikiwemo kusaini mikataba ya kipumbavu sana,kamaliza mission,kapelekwa mambo ya nje kubarizi, umekabidhiwa uozo ufe nao,wamekudanganyia kacheo kasiko ka kikatiba uvimbe kichwa,ila hapo nishati ni kaa la moto hutapaweza,ungepaweza kama mkuu wa nchi angekuwa serious na nafasi yake
 
Dotto hana maajab yoyote hapo Nishati hali ya Umeme imezidi kuwa mbaya
 
Nikwambie Biteko, baada ya Kalemani kuonekana kizingiti kwa mafisadi pale Nishati alipelekwa Makamba Kwenda kufanikisha misheni,ikiwemo kusaini mikataba ya kipumbavu sana,kamaliza mission,kapelekwa mambo ya nje kubarizi, umekabidhiwa uozo ufe nao,wamekudanganyia kacheo kasiko ka kikatiba uvimbe kichwa,ila hapo nishati ni kaa la moto hutapaweza,ungepaweza kama mkuu wa nchi angekuwa serious na nafasi yake
Sidhani kama alizingatia ushauri wako
 
Rais Samia Suluhu amefanya mabadiliko na teuzi za sura mpya kwenye baraza la mawaziri. Uapisho utafanyika September 1, Ikulu ndogo Zanzibar saa tano kamili asubuhi.
1. Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Doto Biteko kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati. Awali alikuwa Waziri wa Madini.

2. Amemteua January Makamba kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Awali alikuwa Waziri wa Nishati.

3. Amemhamisha Balozi Pindi Chana kuwa Waziri wa Katiba na Sheria. Awali alikuwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo.

4. Amemhamisha Steven Byabato kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Awali, Byabato alikuwa Naibu Waziri wa Nishati.

5. Amemteua Jerry Silaa kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Silaa ni Mbunge wa Ukonga, Dar es Salaam.

6. Rais amemteua Anthony Mavunde kuwa waziri wa madini, mwanzo alikuwa naibu waziri wa kilimo.

7. Prof Makame Mbarawa aliyekuwa waziri wa ujenzi na uchukuzi amekuwa waziri wa uchukuzi.

8. Innocent Bashungwa amekuwa waziri wa ujenzi, mwanzo alikuwa waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa.

9. Godfrey Kasekenya aliyekuwa Naibu waziri wa Ujenzi na uchukuzi ameteuliwa kuwa Naibu waziri wa Ujenzi

10. Alexander Mnyeti ameteuliwa kuwa Naibu waziri wa Kilimo

11. David Mwakiposa Kihenzile ameteuliwa kuwa Naibu waziri wa Uchukuzi. Ni mbunge wa Jimbo la Mufindi

12. Judith Kapinga ameteuliwa kuwa Naibu waziri wa nishati, ni mbunge wa viti maalum Ruvuma.

13. Dunstan Kitandula ameteuliwa Naibu Waziri wa maliasili na Utalii, ni mbunge wa Mkinga

14. Stergomena Tax amehamishwa wizara ya mambo ya Nje kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

15. Angellah Kairuki amehamishwa kutoka TAMISEMI na kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii

16. Dkt. Damas Ndumbaro amehamishwa kutoka Wizara ya Katiba ba Sheria na kuwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo.

View: https://www.youtube.com/watch?v=7bLEuvgVGG4

======

View attachment 2733279
View attachment 2733280
View attachment 2733281
View attachment 2733282

Mabadiliko huenda yakaja baada ya Hotba ya Warioba leo.
 
Kila Mtu na "Maisha Yake"

Kila enzi na "Mambo yake"

"Akili za Watu hizo"

Mtachomoka hata kwenye UTEUZI kitabu gani cha Uongozi tukitumie

download (3).jpg

download.png
 
Moja kati ya sababu za muhimu kupata katiba mpya ni hivi vyeo visivyo na tija.

Kuna mtu anaweza kusema matokeo 5 chanya na yenye tija baada ya kuwepo hii ofisi ya naibu waziri mkuu?

Yaani ofisi inaanzishwa tu watu wanapiga pesa za walipa kodi na hakuna tija yoyote inaenda miaka 2 sasa.
 
Kuna mtu hatakiwi hapo ila ni king'ang'anizi.
 
Umeme umeanza kukatika katika...Tena bila taarifa!!! Sijui ndiyo hujuma anafanyiwa Yeye ama anafanyiwa Mama na watu wake?
 
Back
Top Bottom