Mabadiliko Baraza la Mawaziri: Doto Biteko ateuliwa kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati. Makamba Mambo ya Nje, Pindi Chana Katiba na Sheria

Mabadiliko Baraza la Mawaziri: Doto Biteko ateuliwa kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati. Makamba Mambo ya Nje, Pindi Chana Katiba na Sheria

Naibu waziri mkuu? 🤔 Hiki cheo toka lini kipo 🤔
Hiki cheo mara ya mwisho alikishika Mrema kama sikosei enzi za Mwinyi.

Kiuhalisia ni cheo cha utashi wa raisi, hakipo kikatiba.

Ila kinachotafakarisha hapa ni pale Biteko atakapokosea kama Naibu Waziri wa Nishati, je waziri akimuadhibu si itakuwa anamuadhibu Boss wake ambae ni Naibu Waziri Mkuu? Maelekezo ya Waziri wa Nishati yatakuwa na mashiko kwa Naibu wake ambae kiuhalisia ni Boss wake?
 
Watanzania hawajaridhika na Mkataba. Hii teua tengua sio Suluhisho.....
"serikali Ina namna mbili tu..
1. Kiheshimu hofu na maoni ya wananchi kwamba hawajaridhika na suala hili, au
2. Kuwapuuza wananchi na kuendeleza na suala hili.

Lakini wapime madhara ya kila uamuzi watakaoifanya"

Mapinduzi yapo mlangoni mwako.
 
Katiba ya Jamhuri ya Muungano inasemaje kuhusu cheo cha Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano.

Kama hakipo katika katiba je ofisi ya Naibu Waziri Mkuu, wasaidizi wa Naibu Waziri Mkuu, Itifaki za Usafiri za Naibu Waziri Mkuu, marupurupu yake na mazagazaga vingora, malazi, ulinzi yaendayo na cheo hiki kikubwa cha Naibu Waziri Mkuu bajeti yake itatoka wapi n.k n.k
 
Back
Top Bottom