Tetesi: Mabadiliko Baraza la Mawaziri; J. Makamba, Mhagama, Ummy Mwalimu nje; Adadi Rajabu, Bashe watajwa

Tetesi: Mabadiliko Baraza la Mawaziri; J. Makamba, Mhagama, Ummy Mwalimu nje; Adadi Rajabu, Bashe watajwa

Safiiiiiiiiiii....
Adadi Rajabu sio mtendaji kivile, aluvyokuwa DCI rushwa ilishamiri sana... labda Magufuli amdhibiti sana, sbb hii SERIKALI HAKUNA MCHEZo..!!....

Kama proved alikuwa mlarushwa hakuna kuhangaika nae. Mbona wapo wenye rekodi nzur na wenye kuweza kazi na waadilifu? Kwanin kuhangaika na wasio waaminifu?

Yaaani Rais aanze kuhangaika kumfundisha mzee kama yule au mtu mzima kias kile jinsi ya kutokula rushwa? Huko ni kupoteza muda tu na Rais hana muda huo

Ni bora kutumia muda mwingi kumtafta mtu mwenye uwezo na msafi kuliko kupoteza muda kumfundisha kazi asiye weza kazi au kumfundisha uadilifu mtu asiye muadilifu
 
Hivi Bashe ana asili ya wapi? Nipeni Cv yake wajameni

Kuna mtu kapost eti apewe Wizara ya maliasili. Nimeshangaa sana.

Ikiwa hivyo itakuwa vyombo vyetu vya kufuatilia nani ni nani na anafanya nin na network yake ikoje na mambo kama hayo havifanyi kazi ipasavyo. Labda kama ilikuwa kuzushiana tu
 
Mkuu evansGREATDeal alikuwa anacheka??Mimi sikubahatika kumuona...Ila niliona tu yule jamaa pembeni sijui ni naibu waziri wa nini,akicheka baada ya Amada wa Misungwi kurudi toka kujibu swali na nyongeza

Nasikia jamaa alikuwa ananuka pombe kama umesogelea PIPA la "komba" la kuchachua pombe ya komoni
Hata pale anaposoma alikuwa anakunja kunja uso...Daah kweli siasa ni fitna,jamaa ile hang over aliwekewa Royal Village,watu wakaongeza "ingredients" kwenye glass yake.Massauni akatengenezewa tukio la kumfanya aende Zanzibar kwenye kongamano la Vijana wa Zanzibar University,huku nyuma akabaki mtu mzima peke yake
Walishindwaje kumzuia asiingie watoe kisingizio cha ugonjwa. Hii nchi imegeuka kuwa witch hunt. Familia haikuwa naye Dodoma? Hana secretary au pa? Watu wa wizara yake walikuweko? Mawaziri wenzake na wabunge marafiki je? Kweli siasa za sasa hivi ni hatari!
 
Naona kuna jitihada za kuwapigia debe wafuasi wa mheshimiwa aliye katwa wawepo kwenye baraza la mawazir la magufuli

Watu wengine wenye uwezo bado wapo. Wengi tu

Pamoja na mambo mengne kama kiongozi ukitaka kuhujumiwa kirahisi mlete mtu asiye kuamini, ambaye sio loyal kwako kama msaidiz wako wa karibu
 
mvua njooo katarina njooo,najaribu kujikumbusha haka kawimbo ka enzi za utooo tulipokua tukiona wingu limetanda tuliimba hivyoo.japo hatukua tukijua madhara ya mvua katarina
Enzi zangu ilikuwa mvua njoo, katarina usije. Katarina kilikuwa kimbunga? Mimi nilijua jina la mtu, mtoto unayekatazwa kucheza nae lakini kila siku lazima aje, kumwambia huwezi!
 
Rais Magufuli wananchi tunakuomba tuwekee Kifaa Toka jeshini wizara ya Mambo ya ndani.Mtu sahihi ni Dr Gen Balele
 
Huyo hawezi kutoka, labda kama hakua kwenye kamati ya UFUNDI ya ushindi na hakukua na figisufigisu, anaweza kumwaga Mboga wakimwaga ugali. Huyo ni liability, anapewa uwaziri sio kwa kuwa anaweza lahasha, ila kwa sababu kuna vitu anavifaham. Hata hivyo kwa mkuu alivyo, chochote chaweza kutokea!
Hata akimwaga mboga itamsaidia nini??zaidi ya kuishia kubaya zaidi!!
 
Kuna mtu kapost eti apewe Wizara ya maliasili. Nimeshangaa sana.

Ikiwa hivyo itakuwa vyombo vyetu vya kufuatilia nani ni nani na anafanya nin na network yake ikoje na mambo kama

hayo havifanyi kazi ipasavyo. Labda kama ilikuwa kuzushiana tu

Huyu Bashe big No no no no no
 
Hahahahahahahha ngosha uraisi sio umonitor kazi unayo babu ila all in all kama unania njema na ili laana isikutafune tengeneza serikali ya umoja wa kitaifa jifanye umechizi tumbukiza kina mbowe lisu zito mnyika nakina mdee kwenye serikali yako afu kaa ikulu tikisa mguu uone kazi inavyoenda
 
tetesi za kupima upepo hizi...hata mwaka ukiisha atakuwa amemaliza wabunge wote wa ccm kwa majaribio ya uwaziri
 
Hahahahahahahha ngosha uraisi sio umonitor kazi unayo babu ila all in all kama unania njema na ili laana isikutafune tengeneza serikali ya umoja wa kitaifa jifanye umechizi tumbukiza kina mbowe lisu zito mnyika nakina mdee kwenye serikali yako afu kaa ikulu tikisa mguu uone kazi inavyoenda
Hivi watu wengine
Mnajua utaratibu
wa bunge au unaropoka tu

Ni lini ccm waliungana na Ukawa kutengeneza dola!
 
Muda wowote mabadiliko makubwa yanategemea kutokea katika baraza la mawaziri ambapo mawaziri kadhaa watatemwa kutokana na sababu kadhaa.

1. Jenister Muhagama - Anatuhumiwa kwa kuzunguka mamlaka za teuzi (Rais na Waziri Mkuu) katika sakata la kumteuwa kaimu mkurugenzi wa NSSF... Mhagama alitenda kosa hilo akishirikiana na Balozi Ombeni Sefue ambaye kwa sasa kashatumbuliwa.

2. January Makamba - Maranyingi amesikika na kurekodiwa akimsema vibaya Rais, akimsengenya Rais pamoja na kuratibu mipango mbalimbali ya kumdhoofisha Rais Magufuli. haya anayatenda katika Hotel ya Protea Dar es Salaa., na Dodoma ambapo amekuwa akifanya vikao vya siri usiku wa manane na baadhi ya wabunge wa upinzani, pamoja na wafanyabiashara wakubwa wakiwemo wa sukari

3. Ummy Mwalimu - Inasemekana kasi na uwezo wake mdogo haumrithishi Rais kwa sasa..

Katika mabadiliko hayo Adadi Rajabu, Mbunge wa Muheza inasemekana anaweza kuingia kuchukua nafasi ya Kitwanga, wengine wanaotajwa ni Bashe, mbunge wa Nzega ambaye anaweza kupewa docket ya Mazingira au Maliasili na pia Serukamba amekuwa akitajwa.

Mytake: wananchi kwa umoja wetu tumuunge mkono Rais Magufuli ana dhamira njema kabisa la kuwatumikia watanzania.
**NJE YA MADA KIDOGO**
Kutokana na kuongezeka kwa idadi kubwa ya wagonjwa walio katika hali mbaya kwenye hospitali mbalimbali hapa nchini kutokana na kuugua magonjwa yasiyokuwa na tiba na wao kuendelea kuteseka vitandani huku watu wasijue la kufanya, je, muda umefika kwa tanzania kuwa na utaratibu wa "kuua kwa huruma" kama ambavyo nchi za wazungu zinafanya? naomba maoni yako kwenye mjadala huu:

click here: Should "Mercy killing" be practiced in Tanzania?
 
Ndo mana nikasema umoja wa kitaifa wee kiazi rudi shule usije na akili zako za kitwanga na kusema watu tunaropoka
 
Back
Top Bottom