Mabadiliko makubwa elimu nchini- mtaala wabadilishwa

Baadhi ya mapendekezo nakubaliana nayo kwa 100%. Mfano;
-Elimu ya ujasiriamali
-Kutoa elimu juu ya athari za ushoga na ulawiti
-Kupunguza Maadisa Elimu
-Kupunguza idadi ya masomo ya O level
-Kuongeza mishahara ya walimu
-Kuwalipa posho maalum ya kujikimu kwa walimu wa Vinijini
-Kuwasajiri walimu kwenye Bodi na kutoa leseni. Naamini hii itaongeza uwajibikaji na pia kupunguza mlolongo wa "mabosi wa walimu"
-Kuondoa elimu ya astashahada (Grade A). Hii itapunguza ile dharau ya kuonekana walimu ni kundi la watu waliofeli form four.
-Kuanzisha shule za VETA (ikiwezekana kila Kata) ili wale watoto wasiopenda kusoma elimu ya sekondari, waense wakasomee elimu ya ufindi.

Mapendekezo ambayo sijayaafiki ni haya hapa;
-Kujenga nyumba za walimu nchi nzima! Hii ni siasa. Badala yake walimu wangekopeshwa mikopo yenye riba nafuu kwa ajili ya ujenzi wa makazi yao.
-Watoto kusoma mpaka darasa la 6! Aisee vitakuwa bado ni vitoto vidogo, na hii italeta changamoto kwa walimu wa sekondari ambao hawajaandaliwa kufundisha watoto wenye umri mdogo.
-Kufuta somo la Uraia ni kuwanyima wanafunzia uwezo wa kuifahamu nchi yao katika upande wa siasa.
-Kuongeza michepuo mipya. Kama wana mpango huo, basi wapunguze hii mingine ya sasa isiyo na tija. Mfano hii michepuo ya masomo ya ARTS ingebakia michache tu.

All in all, napenda kuwapongeza waandaaji wa huo mtaala mpya kwa jitihada zao za kusikiliza matakwa ya wadau wa Elimu, wakiwemo wa humu jamii forums.

Binafsi nimefarijika sana. Maana mambo yangi mengi niliyo yapigia kelel siku za nyuma, yamenumuishwa kwenye huu mtaala mpya wa elimu.
Una maoni gani kuhusu suala la lugha ya kufundishia? I am just curious
 
Kuondoa masomo ya uraia, aliyeshauri haya achunguzwe.

Muhutasari huu hapa.
Maboresho ya sera ya elimu. Yapo mengi ila hapa wamewasilisha machache tu.

[emoji254][emoji254][emoji254][emoji254][emoji254]

...Masomo kupunguzwa sekondari,

...civics na general study kufutwa kabisa,

...somo la elimu jumuishi kwa mitaala ya ualimu kuanzishwa..

....walimu wa diploma watafundisha primary tu....hii muifikirie upya. Ni muhimu kuangalia uwezo

hakuna tena kutoa certificate za grade A za shule za msingi.....waliopo wataendelea ila hakuna kuingiza wengine vyuoni.

....walimu wa shule za msingi watamaliza form six na wakienda chuoni wanafundishwa pedagogy pekee(bila content) kwa miaka 2 na kwenda kufundisha primary.

....walimu kuongezwa mishahara..
Walimu wenye mazingira magumu watalipwa posho ya mazingira magumu kuliko wale wa mjini.

.....elimu ya msingi miaka 6 tu.

walimu kusajiriwa katika bodi ya walimu na kupewa lesen ya kufundisha kama ilivyo bodi za mawakili na madaktari.

.....maafisa wa elimu wilayani wapunguzwe....
hili tayari limefanyiwa kazi. Kwa meru tayari wamesambazwa jana......lusajo kapelekwa Karatu, Neema kapelekwa Ngorongoro, Morice kapelekwa longido....wamebakia ofisini Mulokozi, baharia na Angel tu.

walimu kuwapa elimu wanafunzi kupinga ulawiti na ushoga. Marufuku kulala kitanda 1 watoto 2 au zaidi.

Masomo ya biology na geography yatakuwa optional kwa o-level. Mtoto sio lazima ayasome, wakati huo civics na GS yatafutwa yataishia primary level tu. Hapa itarudi siasa. Walioshauri hii wanajua umuhimu wa SoMo la uraia??

walimu vyuoni watalazimika kusoma pia elimu ya ufundi na kufundishwa mashuleni.

Michepuo/combinations mpya kuongezeka kwa A-level. Michepuo ya kazi gani??

Wanafunzi kufundishwa ujasiliamali mashuleni ili wawe na uelewa wa kujiajiri- hii ni Bora Ibaki vyuoni pekee.

Miundombinu ya shule nyumba za walimu kuongezwa. Hivi utajenga nyumba nchi nzima? Za walimu wangapi??

Kutaanzishwa shule za veta kwa ngazi ya sekondari. Wanafunz wakimaluza darasa la 6 wataenda wote sekondari na watapewa mtihan wakiwa form one kuchuja wengine wasome masomo ya jumla na wengine wasome ufundi.

Huu ni kama umbea mitandaoni.

Kwa hiyo ukifuta uraia sekondari utarudisha siasa?? Nchi hii inachukuliwa kirahisi sana
Kwa harakaharaka, kama hiyo ni kweli naomba kusema yafuatayo:
1. Elimu ya sekondari lazima masomo haya yafundishwe: fizikia, kemia, jiographia, historia, bilojia
na hesabu. Baada ya darasa la 10/8 kemia na fizikia yawe optional kama ilivyo sasa
2. Naunga mkono kupandisha sifa za walimu wa shule za msingi kuwa wenye diploma, na pia waalimu hao kufundishwa pedagogy (mbinu za kufundisha masomo) badala kufundishwa tena masomo.
3. Mimi siafiki upunguzwaji wa miaka ya elimu ya msingi na wakati huohuo miaka ya sekondari inabakiileile. Nafikiri ingekuwa busara kuangalia kwa jirani zetu mambo yakoje.
4. Tanzania ni mwanachama wa EAC. Malengo au ndoto za EAC ni siku moja hizo nchi kuungana na kuwa na utawala sawa. Hii maana yake ni kuwa wana EAC watakuwa na uhuru na ruhusa kufanya kazi popote pale kwenye EAC. Hii ina maana tuwe na elimu itakayowapa waTZ ushindani kwenye ajira. Kila mtu anajuwa TZ ilipopunguza mwaka mmoja katika shule ya msingi elimu yetu iliethirika saana. Sasa tunapunguza mwaka mmoja zaidi na huenda hii ikaongeza kuathirika kwenye elimu yetu. Kwa vile hata ajira sasa hivi haipo, tuna haraka gani kuwaharakishawatotokumaliza shule mapema na wakiwa wachanga?
 
Una maoni gani kuhusu suala la lugha ya kufundishia? I am just curious
Naamini Kiswahili kingetumika kuanzia chekechea mpaka chuo kikuu, wanafunzi wengi wangeweza kuyamudu masomo yao. Maana hii ndiyo lugha yetu ya Taifa. Kingereza kingetumika kama zilivyo lugha nyingine za ziada mfano Kifaransa, Kichina, nk.

Haya mambo ya kufundisha kwa Kiswahili Elimu ya msingi, na baadaye kuwabadilishia wanafunzi lugha wanapofika sekondari na chuo; inaleta mvurugano mkubwa.

Na ndiyo maana wadau wengi tunateseka kuwapeleka watoto shule za English medium ili kufidia hizi changamoto pale mtoto anapoingia sekondari.
 
Baadhi ya mapendekezo nakubaliana nayo kwa 100%. Mfano;
-Elimu ya ujasiriamali
-Kutoa elimu juu ya athari za ushoga na ulawiti
-Kupunguza Maafisa Elimu
-Kupunguza idadi ya masomo ya O level
-Kuongeza mishahara ya walimu
-Kuwalipa posho maalum ya kujikimu kwa walimu wa Vinijini
-Kuwasajiri walimu kwenye Bodi na kutoa leseni. Naamini hii itaongeza uwajibikaji na pia kupunguza mlolongo wa "mabosi wa walimu"
-Kuondoa elimu ya astashahada (Grade A). Hii itapunguza ile dharau ya kuonekana walimu ni kundi la watu waliofeli form four.
-Kuanzisha shule za VETA (ikiwezekana kila Kata) ili wale watoto wasiopenda kusoma elimu ya sekondari, waense wakasomee elimu ya ufindi.

Mapendekezo ambayo sijayaafiki ni haya hapa;
-Kujenga nyumba za walimu nchi nzima! Hii ni siasa. Badala yake walimu wangekopeshwa mikopo yenye riba nafuu kwa ajili ya ujenzi wa makazi yao.
-Watoto kusoma mpaka darasa la 6! Aisee vitakuwa bado ni vitoto vidogo, na hii italeta changamoto kwa walimu wa sekondari ambao hawajaandaliwa kufundisha watoto wenye umri mdogo.
-Kufuta somo la Uraia ni kuwanyima wanafunzia uwezo wa kuifahamu nchi yao katika upande wa siasa.
-Kuongeza michepuo mipya. Kama wana mpango huo, basi wapunguze hii mingine ya sasa isiyo na tija. Mfano hii michepuo ya masomo ya ARTS ingebakia michache tu.

All in all, napenda kuwapongeza waandaaji wa huo mtaala mpya kwa jitihada zao za kusikiliza matakwa ya wadau wa Elimu, wakiwemo wa humu jamii forums.

Binafsi nimefarijika sana. Maana mambo yangi mengi niliyo yapigia kelele siku za nyuma, yamejumuishwa kwenye huu mtaala mpya wa elimu. 🙏
Niko na wewe sema Kuna mdau eti akapinga ujasiriamali kufundishwa shuleni eti ubakie chuoni. Anadhani kuwa Ni wote tulioenda chuoni.

Hapa sijaona komputa from STD one pia na English itumike from kindergarten, kiswahili iwepo na civics Kama somo moja
 
Jamani biology ibakie kwa lazima hata watoto wetu wajue miili yao,lishe,
1- computer iwe lazima from STD one watoto wanaonyeshwa zile chogo wawe na idea na waambiwe kazi zao.

2- lugha ya English inatuangusha mno.

3- civics iwekwe somo moja ichanganywe na mazingira yetu usafi na uchafuzi ili tuwe na kizazi Cha kutunza mazingira,humo pia watafundishwa taratibu za barabarani please Mana hii traffic accident kuliko hata ugonjwa wowote wa mlipuko ambao unaijua hata miaka 5000 iliyopita, yaani traffic accident Ni kanga la dunia inaua kuliko hata ww1&WW2 combines together jamani pamoja hata ukiweka magonjwa ya mlipuko sijui flu huwezi ukafikia mauaji yanayofikiwa na traffic accident. Yaani hili somo lingeanza kufundishwa tokea wakiwa wadogo mno ili watoto wakue wakiwa na utaratibu wa kuheshimu traffic rules so that become second nature in their subconscious mind. Tena wawe wanafundisha gari wakishafika 18yrs Mana nayo Ni sawa na computer or simu ni basic needs katika dunia ya leo.

Wakubwa wa Sera Kama mko hapa unganeni na wadau wanaohusika wa hii sekta please mlifikirie hili suala. Naombeni mno Kama hata Raisi umo hili ongea na wadau please. Ajali za roads zinazuilika mbona Ni sawa na chanjo za magonjwa yanatibiwa.

Najua smt unakuta mtu upo comfortable umeshiba upo kwenye gari nzito ya ac so mind hawazi Sana labda unawaza Ni wapi ukapate pleasure zaidi Mana euphoria na dopamine zinakusumbua.
 
Kuifahamu miili na lishe haihitaji BIOLOGY ya Sekondari.
 
Kwa harakaharaka, kama hiyo ni kweli naomba kusema yafuatayo:
1. Elimu ya sekondari lazima masomo haya yafundishwe: fizikia, kemia, jiographia, historia, bilojia
na hesabu. Baada ya darasa la 10/8 kemia na fizikia yawe optional kama ilivyo sasa
2. Naunga mkono kupandisha sifa za walimu wa shule za msingi kuwa wenye diploma, na pia waalimu hao kufundishwa pedagogy (mbinu za kufundisha masomo) badala kufundishwa tena masomo.
3. Mimi siafiki upunguzwaji wa miaka ya elimu ya msingi na wakati huohuo miaka ya sekondari inabakiileile. Nafikiri ingekuwa busara kuangalia kwa jirani zetu mambo yakoje.
4. Tanzania ni mwanachama wa EAC. Malengo au ndoto za EAC ni siku moja hizo nchi kuungana na kuwa na utawala sawa. Hii maana yake ni kuwa wana EAC watakuwa na uhuru na ruhusa kufanya kazi popote pale kwenye EAC. Hii ina maana tuwe na elimu itakayowapa waTZ ushindani kwenye ajira. Kila mtu anajuwa TZ ilipopunguza mwaka mmoja katika shule ya msingi elimu yetu iliethirika saana. Sasa tunapunguza mwaka mmoja zaidi na huenda hii ikaongeza kuathirika kwenye elimu yetu. Kwa vile hata ajira sasa hivi haipo, tuna haraka gani kuwaharakishawatotokumaliza shule mapema na wakiwa wachanga?
Japan kijana wa 20 years ana PhD sisi kwann tung'ang'ane na lundo la miaka shuleni huku ukisoma Yale yale? Pia mfumo ubadrike iwe English medium primary zote za tz

Sent from my CPH1803 using JamiiForums mobile app
 
Jamani biology ibakie kwa lazima hata watoto wetu wajue miili yao,lishe,
1- computer iwe lazima from STD one watoto wanaonyeshwa zile chogo wawe na idea na waambiwe kazi zao.

2- lugha ya English inatuangusha mno.

3- civics iwekwe somo moja ichanganywe na mazingira yetu usafi na uchafuzi ili tuwe na kizazi Cha kutunza mazingira,humo pia watafundishwa taratibu za barabarani please Mana hii traffic accident kuliko hata ugonjwa wowote wa mlipuko ambao unaijua hata miaka 5000 iliyopita, yaani traffic accident Ni kanga la dunia inaua kuliko hata ww1&WW2 combines together jamani pamoja hata ukiweka magonjwa ya mlipuko sijui flu huwezi ukafikia mauaji yanayofikiwa na traffic accident. Yaani hili somo lingeanza kufundishwa tokea wakiwa wadogo mno ili watoto wakue wakiwa na utaratibu wa kuheshimu traffic rules so that become second nature in their subconscious mind. Tena wawe wanafundisha gari wakishafika 18yrs Mana nayo Ni sawa na computer or simu ni basic needs katika dunia ya leo.

Wakubwa wa Sera Kama mko hapa unganeni na wadau wanaohusika wa hii sekta please mlifikirie hili suala. Naombeni mno Kama hata Raisi umo hili ongea na wadau please. Ajali za roads zinazuilika mbona Ni sawa na chanjo za magonjwa yanatibiwa.

Najua smt unakuta mtu upo comfortable umeshiba upo kwenye gari nzito ya ac so mind hawazi Sana labda unawaza Ni wapi ukapate pleasure zaidi Mana euphoria na dopamine zinakusumbua.
Mkuu wenzio wanapanga kulifuta SoMo la urais.

They're very stupid
 
Naamini Kiswahili kingetumika kuanzia chekechea mpaka chuo kikuu, wanafunzi wengi wangeweza kuyamudu masomo yao. Maana hii ndiyo lugha yetu ya Taifa. Kingereza kingetumika kama zilivyo lugha nyingine za ziada mfano Kifaransa, Kichina, nk.

Haya mambo ya kufundisha kwa Kiswahili Elimu ya msingi, na baadaye kuwabadilishia wanafunzi lugha wanapofika sekondari na chuo; inaleta mvurugano mkubwa.

Na ndiyo maana wadau wengi tunateseka kuwapeleka watoto shule za English medium ili kufidia hizi changamoto pale mtoto anapoingia sekondari.
Toa Swahili replace with English
 
Kwenye somo Computer kama wakiliweka wahakikishe vutendea kazi viwe vya kutosho au kujadiliana na hapo kwani nakumbuka somo la Tehama lifeline vibaya mno maana unakuta shule nzima computer 2 sasa watoto 200 darasa Moja watawezaje kujifunza na kuelewa kwa ufanisi.
 
Kwa Tanzania it's too late.

Bila marekebisho ya Katiba huku kwenye Elimu,kilimo,viwanda, nishati,nk ni kujisumbua.

Heshima ya katiba ni Moja tu.

"Hakuna mpuuzi atakaye jaribu kubadili badili Chochote sio mitaala pekee". Fungueni macho yenu

Hivi azimio la Zanzibar lililengaga nini vile?? Unaweza ukaanzia kuniuliza swali Hilo kwanza.

Ukitaka kubadili Chochote basi fanya restore ya elimu kabla Mungai hajaiharibu. Utapata kituuki restore itarudi DIT walikuwa safi Sana, Hata CBE, hata mzumbe.. madegree waliyoweka kwenye hivi vyuo hayana maana
 
Ubaya wa nchi hii ni kwamba kila waziri anayekuja anakuja na lake. Wenzetu wanaandaa mitaala kwa kuangalia dunia itakuwa wapi miaka mitano - ishirini ijayo. Sisi tunapuyanga tu. Ndo maana sijaona po pote somo la kompyuta likitiliwa mkazo. Hovyo tu!

Halafu nilifikiri kwamba pengine wangetatua tatizo sugu la lugha ya kufundishia mashuleni. Hii ya sasa ya watu kuanza form one wakiwa hawajui Kiingereza inafanya watu wakariri tu vitu bila kuelewa. Suala la muhimu kama hili lakini limegubikwa na siasa....

Na kwa nini Biology inakuwa optional? Kwa nini somo la uraia linafutwa?
Umemaliza mkuu. Bado tunang'ang'ania vitu ambavyo havina relevance yeyote kwa mustakabali wa mtoto akiingia dunia halisi.
 
Ubaya wa nchi hii ni kwamba kila waziri anayekuja anakuja na lake. Wenzetu wanaandaa mitaala kwa kuangalia dunia itakuwa wapi miaka mitano - ishirini ijayo. Sisi tunapuyanga tu. Ndo maana sijaona po pote somo la kompyuta likitiliwa mkazo. Hovyo tu!

Halafu nilifikiri kwamba pengine wangetatua tatizo sugu la lugha ya kufundishia mashuleni. Hii ya sasa ya watu kuanza form one wakiwa hawajui Kiingereza inafanya watu wakariri tu vitu bila kuelewa. Suala la muhimu kama hili lakini limegubikwa na siasa....

Na kwa nini Biology inakuwa optional? Kwa nini somo la uraia linafutwa?
kwenye swala la lugha lazima wafundishe kwa kiingereza. kwa sababu kazi nyingi zinafanyika kwa lugha ya kiingereza so naona labda iwepo namna ya kufundisha kiingereza kwa njia ambayo ni simple mwanafunzi kuelewa kirahisi zaidi.
Japokuwa ninafahamu kuna nchi za wenzetu wanafundisha kwa lugha zao mama ni kwa sababu wana akili sana sana ndio maaana wamefanikiwa . kwa hapa Bongo hata kuvumbua kitu fulani sisi wenyewe hakuna sasa si bora tu tujifunze kwa lugha ya kiinhereza maana vitu vingi tunajifunza kutoka kwao.

halafu muda wa kutengeneza masomo yote yawe kwa kiswahili na kutafasiri tutapata wapi? sio rahisi sana.

Ila naungana mkono na wewe kukazia kwenye somo la IT on general kwanzia sekondari kwenda A level. itasaidia sana watu kujua basics wakiwa bado shuleni. kama wanavyofanya international schools.
 
Acha uwongo mkuu mbona darasa la 1 hadi la 7 wanafundisha kwa kiswahili na watu wanafaulu? Inashindikana nini sekondari na hata chuo!
 
basi na huko makazini wabadilishe kila kitu kiwe kinafanyika kwa kutumia lugha ya kiswahili kwanza ndio tuachane na lugha ya kiingereza. naomba unipe namna ya kuambia serikali au makampuni binafsi wafanye hivyo maana inaonekana ni rahisi sana kwako si ndio?
 
Back
Top Bottom