Mabadiliko makubwa elimu nchini- mtaala wabadilishwa

Mabadiliko makubwa elimu nchini- mtaala wabadilishwa

Mleta mada kuna mahala hujaelewa vizuri,
Somo la Civics na General study yatafutwa ila kuna somo la Historia ya Tanzania na maadili ndio litakuwa na maudhui ya hayo masomo yaliyofutwa.

Lakini pia bado haujapitishwa, imetolewa kama maoni kwanza, ili wadau wapitie watoe maoni yao na kukosoa penye kurekebishwa na kuboreshwa.
 
basi na huko makazini wabadilishe kila kitu kiwe kinafanyika kwa kutumia lugha ya kiswahili kwanza ndio tuachane na lugha ya kiingereza. naomba unipe namna ya kuambia serikali au makampuni binafsi wafanye hivyo maana inaonekana ni rahisi sana kwako si ndio?
Kwani huko taasisini ni kingereza kinatumika? Umefanya wapi iyo survey yako maana hata hapa nilipo lugha yetu ni kiswahili cjui wewe kwanini unakitetea hicho kingereza unataka turudi kwenye ukabila?
 
Naamini Kiswahili kingetumika kuanzia chekechea mpaka chuo kikuu, wanafunzi wengi wangeweza kuyamudu masomo yao. Maana hii ndiyo lugha yetu ya Taifa. Kingereza kingetumika kama zilivyo lugha nyingine za ziada mfano Kifaransa, Kichina, nk.

Haya mambo ya kufundisha kwa Kiswahili Elimu ya msingi, na baadaye kuwabadilishia wanafunzi lugha wanapofika sekondari na chuo; inaleta mvurugano mkubwa.

Na ndiyo maana wadau wengi tunateseka kuwapeleka watoto shule za English medium ili kufidia hizi changamoto pale mtoto anapoingia sekondari.
Uko sahihi mkuu English libaki kuwa somo la lazma tu ngazi zote za elimu.
 
Kuondoa masomo ya uraia, aliyeshauri haya achunguzwe.

Muhutasari huu hapa.
Maboresho ya sera ya elimu. Yapo mengi ila hapa wamewasilisha machache tu.

[emoji254][emoji254][emoji254][emoji254][emoji254]

...Masomo kupunguzwa sekondari,

...civics na general study kufutwa kabisa,

...somo la elimu jumuishi kwa mitaala ya ualimu kuanzishwa..

....walimu wa diploma watafundisha primary tu....hii muifikirie upya. Ni muhimu kuangalia uwezo

hakuna tena kutoa certificate za grade A za shule za msingi.....waliopo wataendelea ila hakuna kuingiza wengine vyuoni.

....walimu wa shule za msingi watamaliza form six na wakienda chuoni wanafundishwa pedagogy pekee(bila content) kwa miaka 2 na kwenda kufundisha primary.

....walimu kuongezwa mishahara..
Walimu wenye mazingira magumu watalipwa posho ya mazingira magumu kuliko wale wa mjini.

.....elimu ya msingi miaka 6 tu.

walimu kusajiriwa katika bodi ya walimu na kupewa lesen ya kufundisha kama ilivyo bodi za mawakili na madaktari.

.....maafisa wa elimu wilayani wapunguzwe....
hili tayari limefanyiwa kazi. Kwa meru tayari wamesambazwa jana......lusajo kapelekwa Karatu, Neema kapelekwa Ngorongoro, Morice kapelekwa longido....wamebakia ofisini Mulokozi, baharia na Angel tu.

walimu kuwapa elimu wanafunzi kupinga ulawiti na ushoga. Marufuku kulala kitanda 1 watoto 2 au zaidi.

Masomo ya biology na geography yatakuwa optional kwa o-level. Mtoto sio lazima ayasome, wakati huo civics na GS yatafutwa yataishia primary level tu. Hapa itarudi siasa. Walioshauri hii wanajua umuhimu wa SoMo la uraia??

walimu vyuoni watalazimika kusoma pia elimu ya ufundi na kufundishwa mashuleni.

Michepuo/combinations mpya kuongezeka kwa A-level. Michepuo ya kazi gani??

Wanafunzi kufundishwa ujasiliamali mashuleni ili wawe na uelewa wa kujiajiri- hii ni Bora Ibaki vyuoni pekee.

Miundombinu ya shule nyumba za walimu kuongezwa. Hivi utajenga nyumba nchi nzima? Za walimu wangapi??

Kutaanzishwa shule za veta kwa ngazi ya sekondari. Wanafunz wakimaluza darasa la 6 wataenda wote sekondari na watapewa mtihan wakiwa form one kuchuja wengine wasome masomo ya jumla na wengine wasome ufundi.

Huu ni kama umbea mitandaoni.

Kwa hiyo ukifuta uraia sekondari utarudisha siasa?? Nchi hii inachukuliwa kirahisi sana
Maelezo yako kuna mahala hayakosawa na mapendekezo hayo, hata hivyo bado hayajapitishwa ila ni maoni ya awali kabsa,
 
Haya mabadiliko yamehusisha wadau wa elimu au ni watu tu wizaran wamekaa kujaribisha mawazo yao
Hivi ulawiti na ushoga kwa watoto wa tz kwan limeshakuwa ttz au ni kuanza kuwajaza tu mawazo yatakayopelekea wao kuanza kujaribu huo ujinga
 
Maelezo yako kuna mahala hayakosawa na mapendekezo hayo, hata hivyo bado hayajapitishwa ila ni maoni ya awali kabsa,
Mwaka 2007 walijadili kufanya masualakadhaa, Mwaka 2008 yakawa implementated.

Hujawajua bado wale watu wa wizarani..

Nimesema wanakosa kazi za kufanya kabisa
 
Naamini Kiswahili kingetumika kuanzia chekechea mpaka chuo kikuu, wanafunzi wengi wangeweza kuyamudu masomo yao. Maana hii ndiyo lugha yetu ya Taifa. Kingereza kingetumika kama zilivyo lugha nyingine za ziada mfano Kifaransa, Kichina, nk.

Haya mambo ya kufundisha kwa Kiswahili Elimu ya msingi, na baadaye kuwabadilishia wanafunzi lugha wanapofika sekondari na chuo; inaleta mvurugano mkubwa.

Na ndiyo maana wadau wengi tunateseka kuwapeleka watoto shule za English medium ili kufidia hizi changamoto pale mtoto anapoingia sekondari.
You must be kidding eeh....kwa soko gani la ajira hii nchi ukafundishe watu kwa kiswahili mpaka chuo? Au kiswahili kinazungumzika nchi ngapi labda? Hivi umewaza taaluma kama za udaktati au engineering zikafundishwe kiswahili like seriously? Kiswahili ibaki kuwa native language, kingereza iwekwe mkazo kwenye mitaala toka primary school since ndiyo lugha shindani kidunia period!
 
Huu ni mtazamo wangu. Hivyo siyo lazima ufanane na wa kwako. Na nimetoa pia na sababu zangu. Sawa?

Kwani nchi zote duniani zinatumia hiyo lugha yako ya kingereza kufundishia wanafunzi wao?
 
Haya mabadiliko yamehusisha wadau wa elimu au ni watu tu wizaran wamekaa kujaribisha mawazo yao
Hivi ulawiti na ushoga kwa watoto wa tz kwan limeshakuwa ttz au ni kuanza kuwajaza tu mawazo yatakayopelekea wao kuanza kujaribu huo ujinga
Kuna umuhimu wa kuwafundisha watoto namna ya kupambana na hili tatizo.
 
Kuna umuhimu wa kuwafundisha watoto namna ya kupambana na hili tatizo.
Nimeona pia kitandan hakuna kulala wa2 😀 madawati toka uhuru changamoto kitanda na godoro lake kila mwanafunzi wataweza
 
Kwahiyo suala la lugha ya kufundishia msingi na sekondari hawajaliona!!!
 
Acha uwongo mkuu mbona darasa la 1 hadi la 7 wanafundisha kwa kiswahili na watu wanafaulu? Inashindikana nini sekondari na hata chuo!
Na tafiti nyingi zinaonesha wanafunzi huelewa zaidi pale wanapofundishwa kwa lugha ambayo ni lugha mama.

Na kwa Kiswahili, hakuna shaka yoyote ile, kinazungumzwa na Watanzania walio wengi ukilinganisha na kingereza.

Sasa kama Taifa, kuna sababu gani ya kuendelea kuwatesa watoto kufanya mitihani kwa kugha ya kingereza, huku wakitumia lugha ya kiswahili kwenye mawasilkano yao ya kila siku?
 
kwenye swala la lugha lazima wafundishe kwa kiingereza. kwa sababu kazi nyingi zinafanyika kwa lugha ya kiingereza so naona labda iwepo namna ya kufundisha kiingereza kwa njia ambayo ni simple mwanafunzi kuelewa kirahisi zaidi.
Japokuwa ninafahamu kuna nchi za wenzetu wanafundisha kwa lugha zao mama ni kwa sababu wana akili sana sana ndio maaana wamefanikiwa . kwa hapa Bongo hata kuvumbua kitu fulani sisi wenyewe hakuna sasa si bora tu tujifunze kwa lugha ya kiinhereza maana vitu vingi tunajifunza kutoka kwao.

halafu muda wa kutengeneza masomo yote yawe kwa kiswahili na kutafasiri tutapata wapi? sio rahisi sana.

Ila naungana mkono na wewe kukazia kwenye somo la IT on general kwanzia sekondari kwenda A level. itasaidia sana watu kujua basics wakiwa bado shuleni. kama wanavyofanya international schools.
Vumbi la kongo,nguvvu za kiume treatment,mafuta ya upako,maji ya baraka bado sio ugunduzi kweli ama kumfanya amwage maji mengi achafue shuka
 
Elimu ujuzi haihitaji hizo takataka.. Watazisoma primary..
Tatizo tumezoea kusoma vitu vingi visivyo na maana..
 
Waweza tuwekea tuipitie?

Kwanini somo la sheria lisiwekwe lazima O level, ili kila mtu ajue sheria na haki zake

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Kile chama chakavu hakiwez ruhusu kamwe. Yaan waweke somo la sheria ili watu wajue haki zao?????? Weeeeeeeee yaan waraise awareness Mhhhhhh wakati hk chama kinatumia ujinga wa raia kama mtaji
 
Back
Top Bottom