Mabadiliko sheria tano za soka kutoka FIFA, kuchezwa dakika 60, kadi za njano na mengine

Shirikisho la mpira wa miguu ulimwenguni FIFA, lipo katika kufanya majaribio ya mabadiliko ya baadhi ya sheria ambazo huwenda zikaja kuanza kutumika siku za usoni huku lengo kuu ikiwa ni kuuboresha zaidi mchezo huo pendwa.

WhatsApp-Image-2021-07-20-at-1.58.18-PM.jpeg

Majaribio hayo yameanza kufanywa kwenye Mashindano ya Vijana yanayoitwa ‘Future Of Football Cup’ ambapo SC Heerenveen, AZ Alkmaar, PSV Eindhoven na Club Brugge PSV, AZ Alkmaar, RB Leipzig na Club Brugge ni miongoni mwa timu za vijana ambazo zinashiriki kwenye mashindano hayo ya majaribio ya FIFA yanayo husu mabadiliko makubwa ya sheria.

Mabadiliko ya sheria tano (5) mpya katika mchezo huo wa soka yanakuja ambazo zinaweza baadaye kupendekezwa kuwa rasmi katika mashindano yote ya mpira wa mnguu.

Sheria hizo tano (5) mpya ambazo FIFA wanazifanyia majaribio katika mashindano hayo ya Future of Football Cup ni kama zifuatazo.

1. MECHI KUCHEZWA DAKIKA 60, BADALA YA 90
Moja katiya sheria ambazo Shirikisho la Mpira wa Miguu duniani FIFA inazifanyia majaribio ni mpira kuchezwa dakika 60 badala ya 90 kama ilivyozoeleka.

Kwa maana hiyo kipindi cha kwanza kitakuwa na dakika 30, na kipindi cha pili mwamuzi atachezesha hizo hizo 30 na hatimaye kukamilika dakika 60 na sio dakika 90 tena.

Mwamuzi wa mchezo pia atasimamisha saa yake endapo kuna kitu chochote kitatokea uwanjani kama vile mabadiliko ya wachezaji, mpira kutoka nje nk.

2. IDADI YA WACHEZAJI WA ‘SUB’ KUONGEZEKA (substitution)
Kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa Corona duniani, idadi ya mabadiliko ya wachezaji imeongezeka kutoka watatu (3) hadi kufikia watano (5). FIFA inafanya majaribio katika mashindano hayo ya The Future of Football kuangalia kama itawezekana timu kufanya mabadiliko ya wachezaji kadri timu husika itakavyoweza.

3. KADI ZA NJANO
Maboresho yanayofanyika ni kuwa mchezaji anapopewa kadi za njano atatoka nje ya uwanja kwa maana ya kwenda benchi kwa muda wa dakika tano (5) kisha ataruhusiwa kurejea tena uwanjani.

Kwa mantiki hiyo kadi za njano zitakuwa na adhabu zaidi kuliko ilivyozoeleka kwa sasa.

4. MIPIRA YA KURUSHA
Inatarajiwa pia kuondoa sheria ya mipira ya kurusha, endapo mpira ukitoka nje utaanzwa kwa kuweka chini kisha kupigwa kwa miguu na sio kurushwa kama ilivyozoeleka hivi sasa.

5. CHENGA KWENYE KONA (Dribbling)
Mipira ya kona mchezaji ataruhusiwa kuanzisha mpira mwenyewe pasipo kupata msaada kutoka kwa mchezaji wa timu yako. Mchezaji anayepiga kona anaweza kupiga chenga mwenyewe bila kumuanzishia mchezaji mwenzake.

Mwanzoni mwa mwaka huu Florentino Perez alikuja na wazo la kupunguzwa kwa muda kwenye mchezo wa soka wakati walipokuwa wakiitengeneza michuano ya European Super League ambayo ilikuja kupigwa marufuku.

Alipozungumza na El Chiringuito, Perez alisema “Mpira lazima ubadilike, lazima tuchambue kwa nini vijana wenye umri kati ya 16 hadi 24 asilimia 40 miongoni mwao hawavutiwi na soka. Wanasema mechi huwa ndefu mno, na hivyo wanaingia kwenye ‘platforms’ nyingine za burudani. Ni lazima tubadilike kama tunahitaji mchezo wa soka uwendelee kuishi.”

Naye Bosi wa kitengo cha maendeleo ya soka ndani ya FIFA, Arsene Wenger aliwahi kusema siku zijazo sheria nyingi za soka zitabadika.
Mpira kuchezwa dk 60 hapa aisee..!!! Zibaki dk 90.

Kwa kadi ya njano, muda wa adhabu uongezwe toka dk 5 hadi 10...
 
Kama ishu ni kuchoka basi wapunguze ukubwa wa pitch au waongeze idadi iwe wachezaji 12 au waongeze idadi za subs na kuwa zaidi ya hizo 5
 
Akifunga itakuwa ni uzembe wa timu pinzani. Kama idadi ya wachezaji ipo sawa na mipaka ya uwanja inafahamika ,kuzidi kunatoka wapi wakati wachezaji wote wapo humo humo uwanjani?
Umecheza chandimu wewe,hukumbuki tulikuwa tunafungana magoli 15 +?unajua kwa nini,?chandimu haina offside
 
Nimecheza sana ila idadi hiyo ya magoli ilikuwa inapatikana sababu kubwa ikiwa ni uwanja kuwa mdogo ukilinganisha na idadi ya wachezaji.
 
Ahaaa sio uwanja tu hata hiyo sheria ya offside ilichangia sana
 
Huu mpira Sjui unaelekea wap sasa dk 60 n netball hiyo na mipira ya kurushwa na kadi waache Kama ilivo
 
Ivi? fifa wana akili kweli dk 60 ni kurudisha soka nyuma na sio kuboresha
 
Hiyo ya mpira kutokurusha bali kuanzishwa kwa mguu,kwenye futsal wanafanya hivyo
Nalog off
 
Msingi wa mchezo wowote ni burudani.watu tunapenda kufurahishwa.

So, maboresho yoote ni muhimu yajikite ktk kumfurahisha binadamu kutoka kwny fadhaa.

Mimi ningependa iwe hivi:

Dakika 90 ni lazima ziendelee kuwepo sabab
zinarefusha muda wa kuburudika.

Ikiwa hoja ni uchovu (japo siafiki) wapunguze mashindano nje ya ligi.
au waongeze subs.

Ikitokea timu A&B zimedroo,
Halaf timu mojawapo
imetawala mchezo dhidi ya mwenzake kwa zaidi ya asilimia 70% (Ball possession)
timu hiyo ipewe point 2 badala ya 1.

Lengo la kufanya hivyo ni kusistiza culture ya soka ambayo ni entartainment kwanza.

Pia sheria ya offside iangaliwe vizuri kwasab ni too ambigious ikiwezekana teknolojia ihusishwe kutambua makosa ya offside.

Fifa wafikirie kuanzisha mashindano ya cross gender.
ningependa siku moja walau nafasi 2 kati ya 11 za uwanjani kwa kila timu waruhusiwe wanawake kucheza.

Hili nalo litaongeza entertainment.
 
Shirikisho la mpira wa miguu ulimwenguni FIFA, lipo katika kufanya majaribio ya mabadiliko ya baadhi ya sheria ambazo huwenda zikaja kuanza kutumika siku za usoni huku lengo kuu ikiwa ni kuuboresha zaidi mchezo huo pendwa.

WhatsApp-Image-2021-07-20-at-1.58.18-PM.jpeg

Majaribio hayo yameanza kufanywa kwenye Mashindano ya Vijana yanayoitwa ‘Future Of Football Cup’ ambapo SC Heerenveen, AZ Alkmaar, PSV Eindhoven na Club Brugge PSV, AZ Alkmaar, RB Leipzig na Club Brugge ni miongoni mwa timu za vijana ambazo zinashiriki kwenye mashindano hayo ya majaribio ya FIFA yanayo husu mabadiliko makubwa ya sheria.

Mabadiliko ya sheria tano (5) mpya katika mchezo huo wa soka yanakuja ambazo zinaweza baadaye kupendekezwa kuwa rasmi katika mashindano yote ya mpira wa mnguu.

Sheria hizo tano (5) mpya ambazo FIFA wanazifanyia majaribio katika mashindano hayo ya Future of Football Cup ni kama zifuatazo.

1. MECHI KUCHEZWA DAKIKA 60, BADALA YA 90
Moja katiya sheria ambazo Shirikisho la Mpira wa Miguu duniani FIFA inazifanyia majaribio ni mpira kuchezwa dakika 60 badala ya 90 kama ilivyozoeleka.

Kwa maana hiyo kipindi cha kwanza kitakuwa na dakika 30, na kipindi cha pili mwamuzi atachezesha hizo hizo 30 na hatimaye kukamilika dakika 60 na sio dakika 90 tena.

Mwamuzi wa mchezo pia atasimamisha saa yake endapo kuna kitu chochote kitatokea uwanjani kama vile mabadiliko ya wachezaji, mpira kutoka nje nk.

2. IDADI YA WACHEZAJI WA ‘SUB’ KUONGEZEKA (substitution)
Kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa Corona duniani, idadi ya mabadiliko ya wachezaji imeongezeka kutoka watatu (3) hadi kufikia watano (5). FIFA inafanya majaribio katika mashindano hayo ya The Future of Football kuangalia kama itawezekana timu kufanya mabadiliko ya wachezaji kadri timu husika itakavyoweza.

3. KADI ZA NJANO
Maboresho yanayofanyika ni kuwa mchezaji anapopewa kadi za njano atatoka nje ya uwanja kwa maana ya kwenda benchi kwa muda wa dakika tano (5) kisha ataruhusiwa kurejea tena uwanjani.

Kwa mantiki hiyo kadi za njano zitakuwa na adhabu zaidi kuliko ilivyozoeleka kwa sasa.

4. MIPIRA YA KURUSHA
Inatarajiwa pia kuondoa sheria ya mipira ya kurusha, endapo mpira ukitoka nje utaanzwa kwa kuweka chini kisha kupigwa kwa miguu na sio kurushwa kama ilivyozoeleka hivi sasa.

5. CHENGA KWENYE KONA (Dribbling)
Mipira ya kona mchezaji ataruhusiwa kuanzisha mpira mwenyewe pasipo kupata msaada kutoka kwa mchezaji wa timu yako. Mchezaji anayepiga kona anaweza kupiga chenga mwenyewe bila kumuanzishia mchezaji mwenzake.

Mwanzoni mwa mwaka huu Florentino Perez alikuja na wazo la kupunguzwa kwa muda kwenye mchezo wa soka wakati walipokuwa wakiitengeneza michuano ya European Super League ambayo ilikuja kupigwa marufuku.

Alipozungumza na El Chiringuito, Perez alisema “Mpira lazima ubadilike, lazima tuchambue kwa nini vijana wenye umri kati ya 16 hadi 24 asilimia 40 miongoni mwao hawavutiwi na soka. Wanasema mechi huwa ndefu mno, na hivyo wanaingia kwenye ‘platforms’ nyingine za burudani. Ni lazima tubadilike kama tunahitaji mchezo wa soka uwendelee kuishi.”

Naye Bosi wa kitengo cha maendeleo ya soka ndani ya FIFA, Arsene Wenger aliwahi kusema siku zijazo sheria nyingi za soka zitabadika.
Dakika za majeruhi au za nyongeza nazo zifanunuliwe na ikibd zifanyiziwe marekebisho.

Kupoteza mda ni jambo lisilokubalika na ndio maana kuna adhabu au karipio.

kuna janja janja nying zinafanyika, kama mbinu ya kupoteza mda na kumlaghai refa hasa nyakati za dk za nyongeza..mfano:

Dk ya 90:04 timu inafanya sub..

Dk ya 90:03 golikipa kalala chini.atagalagala hapo dk 2 kati ya 3.

Sheria inaelekeza kufidia events hizo kwny zile dk 90..ila imemwachia uhuru wa 100% refarii kwny kufidia dk zile za fidia.
 
Well said
 
Back
Top Bottom