Mabadiliko TRA: Kamishna wa Forodha Mtanganyika Said Athuman Kiondo aondolewa awekwa Juma Bakari Hassan kutoka Zanzibar

Mabadiliko TRA: Kamishna wa Forodha Mtanganyika Said Athuman Kiondo aondolewa awekwa Juma Bakari Hassan kutoka Zanzibar

Kamishna wa forodha Said Athuman Kiondo (Tanganyika), ameondolewa nafasi yake na kuchukuliwa na Juma Bakari Hassan (Zanzibar)

Kamishna Juma Bakari ndiye atahusika na ushuru wa Forodha TRA (customs) ndani ya ofisi ya meneja wa Bandari wakati Bandari zetu zikiwa mateka wa DP WORLD

Idara ya Ushuru na Forodha inasimamia kodi zote zinazohusu biashara ya kimataifa. Kodi hizo ni pamoja na Kodi ya Uingizaji Bidhaa, Ushuru na Kodi ya Ongezeko la Thamani kwa bidhaa ziingizwazo nchini. Kodi ya uingizaji bidhaa ni kodi inayotozwa kwa bidhaa zinazoingizwa nchini.
View attachment 2706440View attachment 2706442View attachment 2706447
Mkuu hii taarifa ndio umeiona Leo?

Cc Moderator , Fang, Active
 
Acheni kuchochea ubaguzi tafuteni sababu kwanini kaondolewa, kwani huyu mzazibari hana sifa au asipewe kwasbb nj mzazibar, hizo propaganda sio nzuri kabisa wengi mnapenda nchi ipasuke vipande
 
Mbona alishakuwepogi Marehemu Walid Juma nafasi hiyo ya Kamishna wa Forodha?

Ambaye naye alikuwa Mzanzibar/Mpemba /Mkojani/ Mshiraz?!

Marehemu Walid Juma alifia madarakani miaka ya (late 2000).
2009 Kama sijakosea.
 
Kwani tatizo ni nini hapo iwapo atatumikia wananchi kwa uadilifu bila kutumika na wakubwa?!

Na iwapo atatumiza majukumu yake bila upendeleo kutakuwa na shida gani?
 
Zamani hawa jamaa walikuwa waadilifu hasa ktk kazi lakini siku hizi mashaka yameingia! [emoji848][emoji848]

Sijui imekuwaje?! [emoji848][emoji848]
 
Mifupa hiiiiii
Wanajaribu kuzima Sakata la Bandari kugawiwa.

Watanganyika wasilaghahiwe Mpaka Kieleweke.... rudisheni .Bandari yetu tu!

Haoooo kamata haooooooo shikaa haooooo
 
Mkuu hii taarifa ndio umeiona Leo?

Cc Moderator , Fang, Active

Mh! Swali zuri. Lakini inakuaje Kuna ofisi za TRA Zanzibar kama sio mambo ya muungamo?
 
Haters wanahangaikaaa, mama Samia, The Mother of Modern Tanzania, amewakaba kiakili na vitendo basi vyupi vinawabana........hawana hata pakutokea. Bakna sasa hv wanahangaika na agenda yao mfu hii ya uzanzibar na utanganyika. Nayo wameshindwa kabla ya kuanza, Watanzania wamewapuuza majuha haya!!
 
Kama ana faa katika hyo nafasi haina shida.dhambi ya utengano ikianza kutula haita ishia Tanganyika na Zanzibar pekee.kwan tukitengana miaka ijayo tutakosoa kwa ukanda au ukabila like kwanii viongoz wa ikulu wote ni kabila flani,au watu wa kusini watasema sisi tuna gesi ruvuma watasema sana makaa so kwanini wasiwe inch wajitegemee kutokana na malighafi walizo Nazi.nao wazanzibar watajikuta kuna waunguja na Pemba nao watajitenga.etc
 
Washauri wa Rais wameshindwa kujua Bandari na TRA ambazo ndio roho za Tanganyika hazipo kwenye Muungano au ni amri kutoka juu kwa ajili ya ujio wa DPW

ZPA - ZANZIBAR PORT AUTHORITY

TPA - TANZANIA PORT AUTHORITY

ZRA- ZANZIBAR REVENUE AUTHORITY

TRA - TANZANIA REVENUE AUTHORITY
Hakuna tatizo Tanganyika sio Tanzania
 
Unelewa vizuri sana sema umeamua kujitia ujinga.

Zanzibar wana Bandari zao kwaajili ya Wazanzibari.

Zanzibar wana Mamlaka yao ya kodi kwaajili ya Wazanzibari.

TPA & TRA ni kwaajili ya watanganyika kutuletea Wazanzibari huko ni kuwadharau watanganyika million 61.

Kwakuwa hakuna mtanganyika ZPA & ZRA ni ujinga wa kiwango cha SGR kutuletea Wazanzibari kuongoza taasisi ambazo zipo Tanganyika.
Hii iambatane na Rais wa Tanganyika kuwa Mzanzibar....hii imekaaje? Kwa sasa bro ni kukaa kwa utulivu mpaka katiba mpya ije na mengineyo. Bi tozo anatuchezesha kipemba full stop.
 
Back
Top Bottom