Mabadiliko TRA: Kamishna wa Forodha Mtanganyika Said Athuman Kiondo aondolewa awekwa Juma Bakari Hassan kutoka Zanzibar

Chini ya CCM mmekubali wenyewe Wazanzibar wawe Watanzania ila Watanganyika sio Wazanzibar, Kwa maana wewe Mtanganyika huna haki ya kufanya kazi au kuteuliwa kwenye SMZ, ila Mzazibar anaweza kufanya kazi popote pale ndani ya JMT.
Haya maswali yenu mnatakiwa kuidhibiti CCM iwape serikali 3 ndio mtatatua huu mkwamo
 
Hoja ipo mkuu labda kama huioni, mfano ofisi gani pale zanzibar ambayo mteuliwa ametoka bara na anaonekana kabisa huyu Mheshimiwa Rais kamtoa huko Itegambwike au Butata huko na kutokana na weledi wake anaweza kushika nafasi hiyo kwenye SMZ.
Hilo la mtu wa bara kuteuliwa kufanya kazi Zanzibar haliwezi kutokea kwa sababu ofisi za Zanzibar siyo za muungano. Wazanzibari wanateuliwa kufanya kazi Tanzania bara kwa sababu ofisi za Tanzania bara kuanzia ikulu, mahakama, Baraza la mawaziri,bunge na majeshi yote ni ya muungano.
 
Kama
Mleta uzii anashangaa na wengine pia wanashangaa kwa sababu mfumo wenyewe wa Muungano hauna tafsiri kwa vile Tanganyika haipo vyatanganyika vyote ni vyaa muungano
Kama Tanganyika haipo Watanganyika wametokea wapi?
 
bwanamdogo tuliza tako hilo mambo ya muungano yako juu ya uwezo wako, soma historia vizuri kuna vitu siyo vya kugusa mojawapo ni muungano. Muungano huu umeamuliwa nje ya nchi ilikuwa ni wa lazima. kwa leo we usipoteze muda wako naona unahangaika sana na vitu ambavyo hata huvielewi, kafanye mambo yako utakuja kufa maskini labda kmm unalipwa na kundi flani.
 
Hizo mamlaka zinaitwa Tanzania haziitwi Tanganyika, elewa dogo. Tanzania ni pamoja na Zanzibar.
 
Bandari ni suala la Muungano
 
Kumbuka wazanzibari ni watanzania pia
Hapa Kuna hoja, tubakie kwenye taasisi zile za Muungano tu...Zile ambazo Tanganyika imefunikwa ndani ya Tanzania lakini upande wa pili Kuna inayofanana kama hiyo hiyo ya Tanzania, Mfano, kama TRA wabakie watanganyika pekee maana Kuna conflict of interests ..Hii ni kwasababu, ukinipa bandari, nikaiua Ili Ile ya Zanzibar ndiyo iwe na faida si ni common sense tu?
 
Hapo kulipaswa kuwe na Tanganyika port Authority

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Serikali ya mapinduzi Zanzibar

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wabunge wa Tanganyika hiki kitu hawakijui?
 
imefika wakati tufungue kesi za kuwaondoa Hawa wazanzibar kwenye nafasi wanazopewa ambazo SI za Muungano kama yule Shaka ameteuliwa kuwa mkuu wa wilaya. Hawa watu wamezoea Chao Chao Chao kwetu ni Cha wote.

Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Serikali ya mapinduzi Zanzibar

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mene
Mene
Tekeli
Peresi
 
JUMA BAKAR, KWA JINSI NINAVYOMFAHAMU MCHA MUNGU HUYU, WATU WA MAMBO YA CHINI CHINI MMEKWISHA,JAMAA AMENYOOKA VIBAYA SANA,PIA HANA MARINGO KABISA,HONGERA!



Ni kweli kabisa,

Labda abadilike.

Huwa namfananisha na Yule Marehemu Walid Juma alikuwaga Commissioner wa Forodha naye.

Naye alikuwa mtu wa Muungwana tu na kujali watu wote bila kuangalia dini zao , kabila wala tabaka lolote.

The Gentleman J. B. [emoji56]
 
Mtu ukiwa na akili ndogo utautesa sana mwili wako. Kwanza mi namshangaa mtu anayehangaika na kaanchi kadogo km Zanzibar. Tanganyika ndio Tanzania, ndio yenye soveregnity, issue zote za kimataifa ni Tanzaniia ambayo kimsingi ndio Tanganyika. Mi ningemwelewa mzanzibar kulalamika siyo hao mnaojiita Tanganyika ila ni kwasababu hamna akili. TRA inafanya kazi Zanzibar kwa taasisi zile za muungano, Ziko za kutosha. Mfano uhamiaji, mambo ya nje, ulinzi na usalama na mengine, Hata hivyo umoja ni nguvu mtu anataka utengano. Nyie kuna watu wanawatumia.
 
Lakin wanzanzibar sio watanganyika! Ujue hlo pia. Je watanganyika ni wakina nani?
Wazanzibari ni watanzania 100%
Watanganyika hawapo! Walikufa wote wakazaliwa watanzania. Tutasemaje watanzania wapo wakati hawana rais, hawana bunge Wala hawana jeshi.
Vyeo vyote vya watanganyika kabla yamuungano vilibadika nakuwa vya watanzania na wanavigawana na ndugu zao kutoka upande wa pili wa muungano yaani Znz. Vyeo vya wazanzibari ndani ya Zanzibar ni vya wazanzibari peke Yao kuanzia Rais , mahakama na wajumbe wa Baraza la wawakilishi isipokuwa polisi na jwtz hao wanafanya kazi sehemu zote za muungano nadhani kwa sababu wizara ya ulinzi na wizara ya mambo ya ndani ni ya muungano.
 
Kumbuka wazanzibari ni watanzania pia
Kama ni hivyo inamaana, mzanzibar kwa sababu ni mtanzania ana haki ya kuwekwa kwenye uongozi wowote Tanzania na Zanzibar. Ila mtanganyika haruhusiwi kuwekwa Zanzibar ila ni Tanzania pekee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…