Mabadiliko TRA: Kamishna wa Forodha Mtanganyika Said Athuman Kiondo aondolewa awekwa Juma Bakari Hassan kutoka Zanzibar

Mabadiliko TRA: Kamishna wa Forodha Mtanganyika Said Athuman Kiondo aondolewa awekwa Juma Bakari Hassan kutoka Zanzibar

Mtu ukiwa na akili ndogo utautesa sana mwili wako. Kwanza mi namshangaa mtu anayehangaika na kaanchi kadogo km Zanzibar. Tanganyika ndio Tanzania, ndio yenye soveregnity, issue zote za kimataifa ni Tanzaniia ambayo kimsingi ndio Tanganyika. Mi ningemwelewa mzanzibar kulalamika siyo hao mnaojiita Tanganyika ila ni kwasababu hamna akili. TRA inafanya kazi Zanzibar kwa taasisi zile za muungano, Ziko za kutosha. Mfano uhamiaji, mambo ya nje, ulinzi na usalama na mengine, Hata hivyo umoja ni nguvu mtu anataka utengano. Nyie kuna watu wanawatumia.
Umeeleweka
 
Kama ni hivyo inamaana, mzanzibar kwa sababu ni mtanzania ana haki ya kuwekwa kwenye uongozi wowote Tanzania na Zanzibar. Ila mtanganyika haruhusiwi kuwekwa Zanzibar ila ni Tanzania pekee.
Huu Muungano huitaji degree kuukataa.

Hata kama hujui kusoma haufai kabisa.

Madokta na maprofesa wa Tanganyika Sijui wanafikiria nini kuhusu Muungano
 
Unalijua aliloliandika mwandishi? Bandari ni swala la muungano kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri. Lakini Zanzibar walijizima data wakavunja katiba na wakaanzisha mamlaka yao. TRA pia inatakiwa kukusanya ushuru hadi Zenji lakini hapo pembeni kuna ZRA. Sasa waziri anayesimamia bandari ni Mzenji na ndo Kasaini DPW baada ya kunyofoa bandari za SMZ.

Sasa mleta uzi anashangaa kuweka boss wa Zenji wakati wana ZRA.
Safi, umefafanua vizuri sana. Hata mtoto wa chekechea kaelewa.
 
Mwenzio kyke
Washauri wa Rais wameshindwa kujua Bandari na TRA ambazo ndio roho za Tanganyika hazipo kwenye Muungano au ni amri kutoka juu kwa ajili ya ujio wa DPW

ZPA - ZANZIBAR PORT AUTHORITY

TPA - TANZANIA PORT AUTHORITY

ZRA- ZANZIBAR REVENUE AUTHORITY

Nenda ukafungue kesi mahakaman kama unaona Serikali imekosea au imevunja Sheria mwenzio kule Mbeya tayar miguu Chali mawakili wa serikali wanataka aivunje kesi kwa gharama alipe Serikali ameeanza kutoka huruma
Washauri wa Rais wameshindwa kujua Bandari na TRA ambazo ndio roho za Tanganyika hazipo kwenye Muungano au ni amri kutoka juu kwa ajili ya ujio wa DPW

ZPA - ZANZIBAR PORT AUTHORITY

TPA - TANZANIA PORT AUTHORITY

ZRA- ZANZIBAR REVENUE AUTHORITY

TRA - TANZANIA REVENUE AUTHORITY
 
The United Republic of Tanzania imeundwa na pande mbili kwa gharama ya upande mmoja kuji dissolve huku upande mwingine ukibaki. Tanganyika ilijigeuza mshumaa, ilijiangamiza kwa lengo la kuangazia wengine.
Hivyo, Muungano huu unampa Zanzibar kuwa access ya nafasi zote, maana Tanganyika ilishajiua hivyo kukabidhi kila kitu kwa Zanzibar, maana katika Muungano huu Zanzibar ndiye pekee aliye hai.
So, unapoongelea maliasili, taasisi, n.k Zanzibar ana mamlaka nazo zote, kama mmiliki upande mmoja, huku upande mwingine akiwa kama msimamizi maana Tanganyika ilipojiua iliacha watoto na wake kadhaa ambao wote walendelea kulelewa na Zanzibar. Hapo ndipo hesabu za nyerere zilipopotea na kuvurunda kila kitu.
Laiti Tanganyika ingekuwepo au ingefufuka leo, basi hapo itakua sawa kusema kuna vitu vya Muungano. Ila kwa sasa, Zanzibar ndiye anayetambuliwa ni vile tu hawaijui nguvu yao.
Sasa hivi Zanzibar wana nguvu ya kuamua lolote ndani ya Muungano na watoto na wa tanganyika wakatakiwa kupokea tu maelekezo.
Kwa kuwa Tanganyika ilishakufa, sasa hivi serikali ya Muungano inabaki kuwa chombo kinachomsikiliza zaidi Zanzibar kabla ya kufanya maamuzi yoyote yale. Maana ndiye pekee aliye hai.
Ingawa Nyerere alikuwa kichwa sana, kwenye Muungano alichemsha vibaya mno.
 
Washauri wa Rais wameshindwa kujua Bandari na TRA ambazo ndio roho za Tanganyika hazipo kwenye Muungano au ni amri kutoka juu kwa ajili ya ujio wa DPW

ZPA - ZANZIBAR PORT AUTHORITY

TPA - TANZANIA PORT AUTHORITY

ZRA- ZANZIBAR REVENUE AUTHORITY

TRA - TANZANIA REVENUE AUTHORITY
Kuwa balanced dogo

What was your message?
 
Washauri wa Rais wameshindwa kujua Bandari na TRA ambazo ndio roho za Tanganyika hazipo kwenye Muungano au ni amri kutoka juu kwa ajili ya ujio wa DPW

ZPA - ZANZIBAR PORT AUTHORITY

TPA - TANZANIA PORT AUTHORITY

ZRA- ZANZIBAR REVENUE AUTHORITY

TRA - TANZANIA REVENUE AUTHORITY
Kwa ambao hamfahamu suluhisho lote la haya Mambo lipo kwenye Katiba Mpya Ile ambayo ilisimamiwa vyema kabisa na tume ya Warioba.. ninajivunia kuwa moja ya watanzania waliotolea maoni Katiba Ile..

Kwenye Katiba Mpya ya Warioba:
(I) haya mapungufu yanayinekana kwenye Muungano yamekuwa solved..

(II) kwenye Katiba hiyo pia Rais amepunguziwa nguvu kwenye teuzi hivyo itachchea uwajibikaji

(III) kwenye Katiba hii Mpya Rais akizingua inaruhusu kushtakiwa.. so haya Mambo ya kufanya Mambo kinyume na Katiba hayatakuwepo
(III) Mwisho kabisa wananchi pia watakuwa wanashirikishwa Kwa karibu kabisa kwenye mikataba kama hii.. yani kutakuwa na transparency[emoji91][emoji91][emoji91]

Elimu kuhusu Katiba Mpya ilitakiwa iandaliwe program maalumu kuelimisha Jamii.. lakini inavyoonekana Kuna watu wanavutia Kwao mapema kabla hili swala la Katiba halijapiyishwa[emoji28][emoji28][emoji28]
 
Mnachoshndwa kuelewa ni kuwa Tanzania ni Tanganyika na Zanzibar ila katika Tanzania Tanganyika ndio ina eneo kubwa sawasawa na UK ENGLAND,WALES, NORTHERN IRELAND NA IRELAND REPUBLIC ILA ENGLAND NDIO SEHEMU KUBWA YA UK
 
Mnachoshindwa kuelewa ni kwamba mambo ya muungano yanaihusu Tanganyika na Zanzibar. Na Yale ambayo siyo ya muungano yanaihusu Zanzibar peke yake. Kwahiyo wazanzibari Wana haki ya kushiriki kila kitu huku Tz bara kwa sababu mambo ya Tanganyika yote ni ya muungano ila watanganyika hawawezi kushiriki mambo ya Zanzibar kwakuwa mambo ya Zanzibar siyo ya muungano.
katiba imetamka wazi ni mambo gani ya muungano na yasiyo ya muungano. Kesi ya uhaini waliyofunguliwa viongozi wa CUF walichomoka sababu katiba inasema Zanzibar siyo nchi 7ngawa baadae walijitoa ufahamu na kudai Zanzibar ni nchi. Tatizo kubwa ;a katiba yetu na hata rasimu ya Warioba waliachana ni kutowekea katiba Kinga. Kinga nayozungumzia ni kutokuwepo kwa kiongozi au mtu yeyote kuwa juu ya katiba kama Sasa rais haruhusiwi kushitakiwa. Kuna mambo mengi yamefanywa na yanaendelea kufanyiwa na viongozi ya uvunjaji wa katiba mfano kuondoa gesi na mafuta kwenye swala la muungano bila kufata taratibu, mabadiliko mbalimbali yanayofanywa na serikali ya Zanzibar bila kuhusisha serikali ya muungano. Tatizo jingine tumekuwa wavivu kuhoji , juzi 8mefunguliwa kesi ya kupinga mkataba wa bandari hivyo hivyo Bado kesi inaweza kufunguliwa kupinga teuzi anazofanya rais ambazo ni kinyume na katiba ya nchi. Hata uteuzi wa kamishina wa tume ya uchaguzi ambaye alikuwa katibu mwenezi WA CCM unaweza kupingwa mahakamani.
 
Back
Top Bottom