Mabadiliko ya mwonekano JamiiForums - Juni 2022

Mabadiliko ya mwonekano JamiiForums - Juni 2022

Ndugu Max mimi naomba mniambie kwanini ni mimi peke yangu ndio napigwa Ban kila nikifuta Comments tena Ban zangu hua za kuanzia mwezi hadi miezi 7. Why only me?? Wakati sio mwenyewe ninaefuta michango. Kuna watu humu ni vinara wa kufuta Comments ila hawajawahi kupigwa ban ila mm nikifuta tu.. nakula ya miezi
Inauma sana[emoji20][emoji20][emoji17][emoji17]
View attachment 2239898View attachment 2239900
Inatakiwa wakulime japo ya mwaka.
Wenzio wote hawafutifuti hovyo kama wewe Vinci.

Ulishaambiwa wewe ni bingwa wa kuharibu flow ya mada,bado unauliza tena kitu kilekile!


Sent from my TECNO CG6 using JamiiForums mobile app
 
Mi ningeomba msamehe zile ID zilizokula life ban tuanze upya.
 
Maxence Melo kuna watu wao kazi ya ni kucheka tu kwenye Uzi, hata kama jambo alichekeshi, wapeni onyo. Alaf pia kuna wegine ni midume ila inatumia ID za kike, hao wapigwe ban
 
Hahaha... Mnanifurahisha.

Nikiri, thread hii nitakuwa karibu nayo ili kuhakikisha kila maoni yanafanyiwa kazi.

Kufikia Jumatatu next week tutakuwa tumekamilisha kuweka fixes (kama zitahitajika).

Timu yetu itakuwa hapa kukuhudumia; ni furaha yetu kusikia toka kwako
Mapendekezo yangu huenda nikawa nje ya uzi.
1. Tv ya jf iliiuwaje mkuu.
2. Jf mna page zenu mitandao mingine
Mfano tweeter..huko mna habarisha,
Kwanini humu hakuna page yenu maalum
Kwa ajili ya kuleta habari zilizo confirmed na vyanzo vingine?
 
Mbona mi sipati notification?

Kuna watu tunawablock ila bado wakianzisha mada twaona mada zao

Kwanini msiweke ukimtia mtu block usione mada yoyote anayoanzisha wala hata changizo zake zozote zile

Pia kwanini msituwekee uwezo wa kuzuia mada fulani, tusizione kabisa ie mada za kukashfu dini za wengine etc
Hili sasa ni janga karibu kila mtu
 
News mpya za kila siku ziwe na muonekano au rangi tofauti ili ziweze kusomeka kwa urahisi.
2. Punguzeni Ban
3. Lianzishe jukwaa la wapendanao ili vijana walitumie kupata marafiki wa kuoana/ kuoa
4. Lianzishe jukwaa la kazi na ajira tu kwa ajili ya vijana ambao ni kundi kubwa
Majukwaa yatajaa so hayatakuwa na maana.
 
•Chonde chonde Boss ,wekeni option ya kuedit na kudelete message PM.
Kwa sisi wa App.
•Mpangilio wa private messages ni mbaya mno sijapata kuona, hasa pale mtu anaporeply message kwa kuiquote.


•Pia rekebisheni system ya kuquote comments.
App sasahivi haiwezi kuquote comments zaidi ya moja.
Ukitaka ujibu comments zote kwa kuziquote pamoja inagoma.
Hii inakera sana.
Mfano;
Watu 10 wamekupa hongera..
Unataka kuwajibu " Asante" kwa comment moja tu itakayojumuisha comments zao hizo zote;App inagoma kuquote zote kwa pamoja.
Inatulazimu tujibu mojamoja.


•Notifications ni balaa jingine.
Haziji kwa wakati..na hata zikija kwa wakati kuna namna App mmelimit kiasi cha notifications.
Mfano mtu akapita akanimwagia likes 100..App haiwezi kuonyesha zote hizo.
Inaonyesha notifications chache tu!
Mwisho wa siku mtu anashindwa kuona notifications nyingine aidha alikuwa tagged huko nyuzini.



•App iongezewe features za reactions
Kama ilivyo browser...kuna reactions mbalimbali mf;thanks,dislike,Sad nk
Lakini kwenye App kuna like tu.

App pia iongezewe baadhi ya manjonjo ya mwandiko.
Kuwe na miandiko hadi ya milazo kama ilivyo browser.


•Uwekwe mfumo unaotema baadhi ya maneno ya matusi .
Mtu akitaka kuandika tusi, system iteme hilo neno..
Yaani iwe kama system fulani ya ajira portal.. ukitaka apply kazi usiyo na vigezo inakutema yaani inakataa mapema kabisa.
Hii itasaidia kupunguza watu wanaopenda kuropoka matusi hovyo.
Wee sis yote haya khaaaah. [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Bora wafanye inaonyesha android au iphone kidogo hii inapunguza makali kuliko kunitajia techno yangu hii kitu inaumiza Sana , unashindwa hata kuandika kitajiri (kuvimba)

Kwanza madam nisaidie kuangalia inaonekana techno yangu hapo chini
Haionekan sir, [emoji23][emoji3][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom