Mabadiliko ya mwonekano JamiiForums - Juni 2022

Mabadiliko ya mwonekano JamiiForums - Juni 2022

JF itakuwa sehemu salama endapo utatusaidia kutumia REPORT button kwa uzuri. Usiache kutuarifu ili tuchukue hatua
Labda mna staff wachache...watu wanaripoti lkn hatua haichukuliwi kwa wakati.
Jf inapaswa kuwa sehemu salama sio ya kuumiza wengine mkuu
 
Hatua nzuri.....

Ila kwenye website hua kuna tatizo moja kubwa, video na picha hua kuzifungua ni shida sana.Binafsi napenda jf ya kwenye website hasa ya freebasic sasa shida ndo hua hiyo picha na video shida kufunguka

Hata video ikifunguka ina nata sana yaani video ya dakika moja unaweza kutumia hata dakika 10 kuiona hata kama mb na mtandao ukiwa imara.
 
Wakuu,

Tupo kwenye hatua za mwisho kuja na JF yenye mwonekano mpya ambayo inaendana na mabadiliko ya teknolojia. Kwa wanaohitaji kuwa sehemu ya majaribio, mnakaribishwa...

Katika mabadiliko haya, huenda ukakutana na kitu kikakufurahisha, kikakuchanganya, kikakufanya uone kuna haja ya kuongeza au kupunguza n.k - usisite kutujulisha kupitia uzi huu.

Thread hii itatumika kukusanya maoni yenu na yatazingatiwa ajili ya kujenga sehemu bora na salama zaidi kwa ajili ya kila mmoja wetu.

Kwa wale watumiaji wa App, tunashauri kujaribu App Mpya ya JamiiForums: Fuata hatua hizi kwani itaendana vema zaidi na kinachokuja.

Tunawashukuru kwa ushirikiano mnaotupa kila mara kwani hadi toleo hili ni tokana na maoni yenu.

Kutakuwa na features kadhaa hazitakuwa released mapema hadi zikamilike kufanyiwa testing ndipo ziwe applied.

Tunawapenda, tunawajali na tunaahidi kuendelea kutoa huduma bora.

Asanteni sana!
Jambo la muhimu kabisa mnatakiwa kuweka namna ambayo mtu akimblock mtu mwenye lugha mbaya uliyemblock anakuwa haoni contents zake na wewe houni zake kabisa.
 
Hii ya sasa mlitoa ule uwezo wa thread kuendelea pale ulipoishia naomba mzingatie.

Mtu akigungua thread akasoma badae akafunga akija kufungua aendelee pale alipoishia
 
Mnapofuta nyuzi muwe mnatoa na sababu juzi tu hapa nililalamikia wadada wanao inama kama ngamia wakiwa sita kwa sita badala ya kubinuka binu!..
Uzi ukafutwa sababu sikupewa!

Ahsante nanyinyi kwa ushirikiano wenu jf for life.
haaaaaa...
 
Utasema unaonaje changes baada ya release.

Nimelazimika kutoa taarifa mapema ili watu msione tumewashtukiza.
Pm za browser tunaomba mrudishe kipengele cha ‘kick out’

Zamani ilikuwepo kick out na leave.. ila mmeondoa kick out mkabakiza leave. Tunaomba kick out irudi….
 
Back
Top Bottom