Mabadiliko ya mwonekano JamiiForums - Juni 2022

Mabadiliko ya mwonekano JamiiForums - Juni 2022

I always late.

Asante boss.

Hata kabla sijaona huu uzi nilikuwa nawaza kutokana na uzi mmoja uliosema.... mwana jf akifariki nani atatoa taarifa, ... na pengine was like mchango au rambirambi zetu kwa mwana jf aliyefariki inakuwaje, (japo niliomba [emoji871] but was jocking )

So nikawaza uwe ( Maxence Melo ) na something like database itakayobeba watu wako jf wote.

Japo mengi tunaona ni siri but ukimtaka mtu private anakupa contact.

Okay wapo watakaokataa kukupa kitu cha kuweka database but I know more than 75% will give you, yaani wewe kama wewe siyo mtu mwingine.

Let's see kuna some benefits like bima ie ya mazishi etc au wale wanaofikia kupata gawio kutokana na faida iliyopatikana kwa mauzo au matangazo but all in all even it's small ila huwa inaburudisha.

Again I thank you Maxence Melo kwa kuwa unajali. [emoji109]
 
Wakuu,

Tupo kwenye hatua za mwisho kuja na JF yenye mwonekano mpya ambayo inaendana na mabadiliko ya teknolojia. Kwa wanaohitaji kuwa sehemu ya majaribio, mnakaribishwa...

Katika mabadiliko haya, huenda ukakutana na kitu kikakufurahisha, kikakuchanganya, kikakufanya uone kuna haja ya kuongeza au kupunguza n.k - usisite kutujulisha kupitia uzi huu.

Thread hii itatumika kukusanya maoni yenu na yatazingatiwa ajili ya kujenga sehemu bora na salama zaidi kwa ajili ya kila mmoja wetu.

Kwa wale watumiaji wa App, tunashauri kujaribu App Mpya ya JamiiForums: Fuata hatua hizi kwani itaendana vema zaidi na kinachokuja.

Tunawashukuru kwa ushirikiano mnaotupa kila mara kwani hadi toleo hili ni tokana na maoni yenu.

Kutakuwa na features kadhaa hazitakuwa released mapema hadi zikamilike kufanyiwa testing ndipo ziwe applied.

Tunawapenda, tunawajali na tunaahidi kuendelea kutoa huduma bora.

Asanteni sana!
Mkuu hongera sana kwa maboresho.
Font size imekuwa kubwa sana, kama inawezekana ibakie ya zamani.
Kwa upande wa font style imekaa vizuri sana.
 
Username change iwe automatically sio hadi kuomba ruhusa ya mods

Tena iwe hadi kwa app sio hadi tutumie web
 
1. Option ya kufuta account naomba muiangalie, kama mtu ameamua kwa dhati hataki kuendelea na account yake na anatamani kuifuta, mumpe hiyo option ya "delete account ".

2. Option ya kufuta uzi, inaweza isiwe realistic lakini kuna wakati mtu anaona uzi wake unaleta sintofahamu, kuwe na option ya kuomba direct kwa mods uzi ufutwe kwa sababu ambazo zitakuwa valid.

Hongereni kwa kazi nzuri jf team!
 
Boss maombi yangu kwenu.

Naomba kuwe na algorithm ambayo itaweza deduce ni contents gani unaziangalia mara nyingi hivyo uwe unaletewa contents ambazo hazitakufanya uwe unarefresh over and over just kupata kitu kipya.

Kwa sasa hivi unaweza kuta Id moja ina nyuzi zake nne zipo kwenye user interface, ukirefresh, bado zinakuja za Id hiyo hiyo. Bahati mbaya waweza kuta hiyo Id hua inaandika miyeyusho day in day out.

Najua kuna ignore button ila ukimuignore mtu ikatokea siku kwa bahati mbaya au nzuri kaandika contents unazozielewa hautaweza ona.

Natanguliza shukrani.
Ungeandika kiswahili tuu
 
Wiki nzima sasa notifications zinakuja baada ya masaa 7 kwanini?
Je ndio uboreshaji huo na maandilizi yake yanakuwa hivyo mwanzo
 
Maxence Melo nina maoni kidogo kwenye mabiresho yanaoyendelea.

1. App iwe na uwezo wa kufungua attachments aina zote bila kuwa na haja ya kupitia kwenye browser. Nasema hv kwakuwa sio watumiaji wote wanajua kubadili permission kwenye simu zao hasa zile ambazo zinamtaka mtumiaji akubali kufungua link/attachment kwa kutumia third party application ("just once" "always") ambapo kuna muda mtumiaji anaweza kuselect app kama sehemu ya kutumia alway hasa watumiaji wapya nakujikuta wanashindwa kuona attachments zinazokuwa zimetumwa humu.

2. Nyuzi zinazofanana ama kushabihiana zimekuwa zikiunganishwa. japo zinaweza kuwa na maudhui, kuna muda mjadala hutofautiana kulingana na mleta uzi mwenyewe. Inapotokea hivi, sio mbaya ikawekwa link mwanzo kabisa mwa uzi kuonesha uzi uliounganishwa unapoanzia kama inavyofanyika pindi mjadala unapokuwa na mwendelezo mrefu hivyo kuwekwa link ya episodes.

3. Siku zq karibuni kumekuwa na shida upande wa notifications. Unawsza kutumiwa ujumbe ama mtu kukutag kwenye uzi fulani, unachelewa kupata notification. Hili nalo lifanyiwe kazi.

4. Ikitokea uzi umefutwa kwasababu yoyote ile, basi heading/link yake isionekane kwenye orodha ya nyuzi ama notifications. Kwasababu unaweza kukuta notifications 5 lakini zote nyuzi zake zimeshafutwa hivyo kuonekana kama usumbufu. Kama hilo litakuwa na ugumu, basi kuwe na alama ya kuonesha kuwa uzi uko pending.

5. PM iboreshwe pia. Sio kila unapoanzisha chats na mtu yuleyule jumbe ziwe separate kama visimu vidogo vinavyopokea ujumbe. Ninapendekeza kuwe na sanduku moja kwa kila member utakayechat naye. Akituma ujumbe ama ukimtumia ujumbe, basi automatic ujumbe unaungana na jumbe za nyuma kwa mtu huyo iwapo mlishachat.

6. Mada ambazo zinashusha credit ya jf kwakuwa ni mtandao ambao watu tunaamini tunaweza kupata taarifa husika kwa ukamilifu, zisiruhusiwe kuwa hewani. Kwa mfano, mtu anaweza kutuma ujumbe akiomba ushauri labda ameuguliwa, badala ya kushauriwa anaanza kudhihakiwa. Inawezekana mleta uzi asiwe na uelewa wa kureport lakini ikitokea mtu ameripotiwa mara nyingi kwa mada/hoja chochezi ama zenye kutweza utu, basi awe blacklisted mojakwamoja kutumia jf hata kwa kubadili id.

7. Mijadala ya kuponda imani yoyote ile ikiwemo wasioamini katika dini, isiruhusiwe kwa namna yoyote kwani kila mmoja anao uhuru wa kuabudu ama kuamini chochote ilimradi asivunje sheria.

Kwa sasa ni haya tu. Naomba kuwasilisha.
 
Wadau mnavyotoa mapendekezo, maprogrammer wako wanaangalia wanasema hiiiii 🤣
 
natamani ningekuwa na uwezo wa kuignore au kuficha uzi usionekane, kuna nyuzi zinatembea kweli lakini maudhui hayafurahishi kabisa huwa nachukizwa kukutana na updates zake
 
Ushauri wangu,

Kwenye kila uzi, mods wapandishe juu zile top comments haijalishi zina likes au reaction ngapi.

Point yangu ni ili msomaji aliyevutiwa na heading ya uzi akutane na comments za maana tu zinazohusiana na uzi kwanza.

Zile cheap comments ambazo hazihusiani na mada husika kama kusalimiana na kutaniana ziwe chini. Kwaiyo msomaji akifungua uzi anakua na uwezo wa kuona machangio yanayohusiana na mada kwa mtitiriko mzuri!

Shukrani!
Naunga mkono hoja.
 
Back
Top Bottom