Mabadiliko ya mwonekano JamiiForums - Juni 2022

Mabadiliko ya mwonekano JamiiForums - Juni 2022

Sawa boss, nashauri kuwe na kipengele cha breaking news na iwe ni ya muda mfupi wa siku moja tu badala ya kupokea habari kwa kuchelewa Sana. Forum hiyo itatusaidia kupata taarifa kwa haraka!
 
Asante sana Mkuu. Maoni yangu ni kama ifuatavyo kwanza kabisa mnapofuta Nyuzi ni vyema mkamtaarifu muhusika badala ya kufuta kimyakimya Kwa ubabe!!

Pili jukwaa la complain lirudishwe Maana halionekani Kwa sasa, kuna umuhimu pia mkaweka jukwaa la diaspora tuna mengi ya kusemezana, vile vile kumekuwepo Na tabia ya moderators kukimbilia kufuta link zangu za Youtube ambazo kiuhalisia hazivunji sheria yoyote ya JamiiForums! Na wanazifuta bila hata kutoa sababu yoyote!! Najiuliza link zangu zinakosa gani? Alafu kwa video ndefu sana njia nzuri ni ku share link ya Youtube then wahusika watachagua waende huko au la!! Sasa kwanini moderators hukimbilia kuzifuta? Ni kwamba ni washamba wa teknolojia au ni ulimbukeni? Kwakweli huu ni uhuni wa waziwazi Na unakwenda kinyume Na haki ya kujieleza ambayo umekuwa ukiipigania Kwa miaka mingi sasa.

Mwisho ma moderator wamekuwa Na tabia ya kukimbilia kuunganisha nyuzi mpya na za zamani hata kama haziusiani moja Kwa moja bila hata kusoma Na kujua nyuzi inahusu nini? Huu ni uhuni mwingine unaopaswa kukemewa kabisa kwa JamiiForums mpya tuitakayo!
 
Wazinzi na walevi ni tofauti na nyie mapunga,nyie mnaaibisha taifa
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] sasa hawatoki na hawapigwi ban hao watu.
 
•Chonde chonde Boss Maxence Melo ,wekeni option ya kuedit na kudelete message PM.

Kwa sisi wa App.
•Mpangilio wa private messages ni mbaya mno sijapata kuona, hasa pale mtu anaporeply message kwa kuiquote.

•Pia rekebisheni system ya kuquote comments.
App sasahivi haiwezi kuquote comments zaidi ya moja.
Ukitaka ujibu comments zote kwa kuziquote pamoja inagoma.
Hii inakera sana.

Mfano;
Watu 10 wamekupa hongera..
Unataka kuwajibu " Asante" kwa comment moja tu itakayojumuisha comments zao hizo zote;App inagoma kuquote zote kwa pamoja.

Inatulazimu tujibu mojamoja.

•Notifications ni balaa jingine.
Haziji kwa wakati..na hata zikija kwa wakati kuna namna App mmelimit kiasi cha notifications.
Mfano mtu akapita akanimwagia likes 100..App haiwezi kuonyesha zote hizo.

Inaonyesha notifications chache tu!
Mwisho wa siku mtu anashindwa kuona notifications nyingine aidha alikuwa tagged huko nyuzini.

•App iongezewe features za reactions
Kama ilivyo browser...kuna reactions mbalimbali mf;thanks,dislike,Sad nk
Lakini kwenye App kuna like tu.

App pia iongezewe baadhi ya manjonjo ya mwandiko.
Kuwe na miandiko hadi ya milazo kama ilivyo browser.


•Uwekwe mfumo unaotema baadhi ya maneno ya matusi .
Mtu akitaka kuandika tusi, system iteme hilo neno..
Yaani iwe kama system fulani ya ajira portal.. ukitaka apply kazi usiyo na vigezo inakutema yaani inakataa mapema kabisa.
Hii itasaidia kupunguza watu wanaopenda kuropoka matusi hovyo.
 
Jukwaa na Safari liongezeke, tuwe tunapeana experience za kusafiri
 
Nashauri,

Comment inayopata 'likes' nyingi, iwe juu. Maana yake comment lazima iwe imefurahisha au imeelimisha au kujibu kulingana na uzi wenyewe.

Hii itasaidia kuondoa kiherehere cha baadhi ya Members kukimbilia kuchukia nafasi, ambao huanzisha mzaha na hatimaye kuondoa maana nzima ya uzi husika. Utasikia, 'siti ya kwanza'.

Utadhani wanawahi viti vya Paradiso.
 
Mnapofuta nyuzi muwe mnatoa na sababu juzi tu hapa nililalamikia wadada wanao inama kama ngamia wakiwa sita kwa sita badala ya kubinuka binu!..
Uzi ukafutwa sababu sikupewa!

Ahsante nanyinyi kwa ushirikiano wenu jf for life.
Ehehe Enaseketesha Sana Kwakweli [emoji1]
 
Nashauri,

Comment inayopata 'likes' nyingi, iwe juu. Maana yake comment lazima iwe imefurahisha au imeelimisha au kujibu kulingana na uzi wenyewe.

Hii itasaidia kuondoa kiherehere cha baadhi ya Members kukimbilia kuchukia nafasi, ambao huanzisha mzaha na hatimaye kuondoa maana nzima ya uzi husika. Utasikia, 'siti ya kwanza'.

Utadhani wanawahi viti vya Paradiso.
Pia inamsaidia msomaji kupata maelezo mazuri zaidi au msaada zaidi juu ya mada husika haraka mwanzo kabisa baada ya mada kuliko jibu la maana unalikuta kwenye cokent ya 800
 
Oya Melo wekeni jukwaa la UTALII
Kusaport utalii wa ndani na
Royo tua

Ila watu kama akina Zero IQ hamna kucoment

Afu mturejeshee Lemutuz lemubebeZ hapa jukwaani aendelee kutupa experience za majuu ila chonde chonde yale mashati yakufunika vits mpka haionekani asije nayo
 
Hapa na mie nakazia, watoe hii hali sio nzuri. Wafute kabisaa.
Bora wafanye inaonyesha android au iphone kidogo hii inapunguza makali kuliko kunitajia techno yangu hii kitu inaumiza Sana , unashindwa hata kuandika kitajiri (kuvimba)

Kwanza madam nisaidie kuangalia inaonekana techno yangu hapo chini
 
Maxence Melo mdogo wangu kongole sana kwa JF na poleni kwa mnayoyapitia kwa ajili yetu.

Msisahau kuhakikisha zile emoji zote zinazoonekana kwenye browser ziweze kuonekana kwenye watumiaji wa app, maana kwa sasa ni "like" pekee inayoonekana kwenye app wakati kwenye browser kuna like, dislike, love, wooh.
Mungu awabariki sana.
 
Mbona mi sipati notification?

Kuna watu tunawablock ila bado wakianzisha mada twaona mada zao

Kwanini msiweke ukimtia mtu block usione mada yoyote anayoanzisha wala hata changizo zake zozote zile

Pia kwanini msituwekee uwezo wa kuzuia mada fulani, tusizione kabisa ie mada za kukashfu dini za wengine etc
Block ni udhaifu
 
Back
Top Bottom