Mabadiliko ya mwonekano JamiiForums - Juni 2022

Mabadiliko ya mwonekano JamiiForums - Juni 2022

Maandishi yamekuwa makubwa sana as if wote ni wagonjwa wa macho pia title ni kubwa sana
Kwangu mvuto umepotea kutokana sipati ninacho kihitaji kwa wakati ila kilichopo
Muonekano huu mpya unafanya nijione nimerudishwa nyuma technically na nahitaji kusonga mbele
Rekebisheni
 
Wakuu,

Tupo kwenye hatua za mwisho kuja na JF yenye mwonekano mpya ambayo inaendana na mabadiliko ya teknolojia. Kwa wanaohitaji kuwa sehemu ya majaribio, mnakaribishwa...

Katika mabadiliko haya, huenda ukakutana na kitu kikakufurahisha, kikakuchanganya, kikakufanya uone kuna haja ya kuongeza au kupunguza n.k - usisite kutujulisha kupitia uzi huu.

Thread hii itatumika kukusanya maoni yenu na yatazingatiwa ajili ya kujenga sehemu bora na salama zaidi kwa ajili ya kila mmoja wetu.

Kwa wale watumiaji wa App, tunashauri kujaribu App Mpya ya JamiiForums: Fuata hatua hizi kwani itaendana vema zaidi na kinachokuja.

Tunawashukuru kwa ushirikiano mnaotupa kila mara kwani hadi toleo hili ni tokana na maoni yenu.

Kutakuwa na features kadhaa hazitakuwa released mapema hadi zikamilike kufanyiwa testing ndipo ziwe applied.

Tunawapenda, tunawajali na tunaahidi kuendelea kutoa huduma bora.

Asanteni sana!

===== UPDATES======

Changes on the new version:

1) Kuna urahisi wa kufichua mambo mazito bila data zako zozote kuchukuliwa na bila post kwenda public kwanza (utaona button ya Fichua Uovu). Hii itasaidia hata wasio wanachama (baadae) kushiriki kikamilifu kupinga ufisadi na rushwa kwa ujumla.

2) Faragha ya mwanachama imelindwa zaidi, hakuna wa kujua wewe ni nani on JF bila wewe kumpa access ya kifaa chako (simu, tablet au pc). Tulipata vilio vya watu kuchunguliwa IDs tukaja na suluhu.

3) Unaweza kuchagua kutumia JF ikiwa light version, dark mode au dark blue mode (my favorite).

4) Maandishi ya sasa yanasomeka kirahisi zaidi na wenzetu wenye uoni hafifu. Wasioona kabisa lakini wana vifaa vya kusomea wataweza kuitumia JF kwa urahisi zaidi.

5) Soon kuna mambo mapya yanaanza kufanyika via JF, mabadiliko haya yamelenga kupokea yajayo kuanzia mwezi huu na kuendelea.

6) Ukiwa kwenye forum yoyote, huhitaji kubonyeza Page 2, Page 3, Page 4. Wewe vuta kwenda chini tu, mada zitakuja (scroll down).

Nitaendelea…
Ahsante sana Mkuu.
Pole na majukumu na Hongera sana sana na Maendeleo ya Tovuti hii.

Mkuu,
...sijui kama ni mimi lakini nina hofu wale wanaounganishwa moja kwa moja hapa kutoka tt wanatumia viboti... naona kuwa vi boti vinatumika...niondoe hofu!

Natumaini umenielewa.

Wako kwa Amani😎Wa Kujenga Taifa.
 
Mabadiliko ya mwonekano ni UTOTO..Heri maboresho ya content..Platfoams mpya zibuniwe..kwa mfano yupo Mshiriki humu aliwahi kupendekeza liwepo Jukwaa la Fununu/Tetesi.
 
Maxence Melo naomba tukibonyeza kwenye JamiiForums ya home twende moja kwa moja kwenye threads na sio topics. 🙏
 
Muonekano mpya kwa watumiaji wa browser uko ovyo kinoma,, ama hakika kuchamba kwingi........
 
Back
Top Bottom