Mabadiliko ya mwonekano JamiiForums - Juni 2022

Ndugu Maxence Melo , kwanza hongereni kwa kazi murua ya kuiboresha Jamii Forum, kiukweli jukwaa hili limekuwa burudani na kilevi kwa wengi wetu ambao tunapenda kupata habari na kusoma mitazamo ya watu mbalimbali .

Mbali na kuja na muonekano huu, ila kiukweli nahisi bado kuna kazi ya kuifanya kuboresha muonekano huu haswa kwa wale wenye kutumia simu zenye vioo vidogo, muonekano uliopita ulikuwa rahisi zaidi kwetu, kwani uliifanya themes iwe responsive kwenye smart vitochi vyetu na binafsi nilikuwa naenjoy mnoo, kwani nikiwa mbali na laptop yangu ningeweza kuperuzi jukwa hili kupitia kitochi changu na nikaburudika.

Lakini toka mmebadili ile thems, kwa kweli ni kama kule mmetuachia mateso ya kuperuzi hili jukwaa, font zake kule zimekuwa kubwa mnoo, kiaisi zinabeba nafasi kubwa na kufanya kuscrow kuja chini ichukue muda mrefu, ile sehemu ya kubonyeza upate latest news pale juu haipo tena, si kwenye simu mpaka kwenye laptop view, hii inapelekea mtu anarudi tena home , au kwenye general forums kupata new update, usumbufu huu.

Pia, huku kwenye viswaswadi vyetu hili jukwaa haliwi responsive , linakuwa out of screen view, mpaka usogeze kulia kushoto ndio upate kusoma ujumbe wote, tafadhali turekebishieni hili.

zile gadget pale juu natamani zirudi kama awali,

mengine nitayatoa nikiendelea kuperuzi zaidi.
 
Kwa ule muonekano bora nibaki kwenye App tu ingawa inazingua sana kupata notification.
 
Reactions: _ly
Hiyo pop up ni repeatatio ya kile kilichopo kwenye headline kwa nini isiondolewe ili kutoa nafasi kwa msomaji kutosumbuka kuiondoa kila inapojitokeza?
 

Attachments

  • Screenshot_20220610-014341_Samsung Internet.jpg
    247.8 KB · Views: 22
Kwenye APP unatusahau jaman, tunataka App iwe na fixtures nzuri, muonekano wa PM, na video kufunguka.
Please Mr Tufanyie maboresho.

Yeeees, upo sahihi tena video iwe unaiplay palepale kama zilivyo Fb na Twitter, asisahau na option ya kuidownload hiyo video
 
Mods mmeshindwa kabisa kuondoa hiyo kero au mfumo wenu ni copy and paste
 

Attachments

  • Screenshot_20220625-130358_Samsung Internet.jpg
    195.8 KB · Views: 13
wakuu kwa sasa ndakuwa offline siku wakirekebisha App naomba mnitag ili niingie Jf maan saiz App inazingua na max kama katupotezea tu watumiaji wa app.
Browser ni upuuzi tu kwa sisi tuliozoea app
 
Utakua sio uhuru tena wa maoni, acha watu waongee chochote, hujalazimishwa kusoma mada ya mtu, kama mtu anadanganya atakua exposed na mda, so relax

Sent from my SM-A025F using JamiiForums mobile app
 
wakuu kwa sasa ndakuwa offline siku wakirekebisha App naomba mnitag ili niingie Jf maan saiz App inazingua na max kama katupotezea tu watumiaji wa app.
Browser ni upuuzi tu kwa sisi tuliozoea app
Mkuu, kwani ile old version imeondolewa? Mbona bado ipo? Na mimi ndo ninayotumia!
 
wakuu kwa sasa ndakuwa offline siku wakirekebisha App naomba mnitag ili niingie Jf maan saiz App inazingua na max kama katupotezea tu watumiaji wa app.
Browser ni upuuzi tu kwa sisi tuliozoea app
Kiukweli watumia wa app kama tumetengwa kiasi fulani, manake mimi nimelalamikia swala langu la ku ignore baadhi ya forums lakini bado naendelea kuzikuta kwenye new posts na trending

Inaboa sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…