Mabadiliko ya mwonekano JamiiForums - Juni 2022

Mabadiliko ya mwonekano JamiiForums - Juni 2022

Muonekano mbaya mnooo too faint 100% wa kwanza ni much better. Hata ikifungua inaonyesa thread moja mpaka u scrow down iliyopita zilikua zikionekana zaidi 4.
 
Huu mfumo mpya sijauelewa kabisa TRENDING na NEW POST uki VIEW MORE; ndo mwisho au mie ndo sijaelewa. Zama zile ilikuwa unaweza kufungua new post mpaka page ya 25. Inanikata stimu kweli kweli inanilazimisha niingie kwenye majukwaa moja moja wakati nilikuwa naweza kuingia kwenye new post na kusoma majukwaa mbalimbali au mie ndo sijaelewa huu mfumo mpya. .

Hapa yenyewe nahangaika kutafuta my past thread, aisee huu mfumo bado haujanikaa vizuri kabisa. Tupeni somo Maxence Melo sielewi elew. Maoni yangu mfumo wa kwanza ulikuwa vizuri sana huu uko very boaring. Maandishi yapo makubwa sana kero kweli
Imani yangu watayasikiliza maoni ya watumiaji maana wengi muonekano huu haujawapendeza.
 
Kama kichwa kinavyosema.
Kwa kweli mmeharibu muonekano na majukwaa.
Unajua hata makampuni makubwa kama CocaCola, Pepsi, Nike, Adidas, Barclays etc. huwa hayabadili logo wala UI mbali na ilivyokuwa awali. Sababu kubwa ni biashara. Kwa mabadiliko haya mlioweka, mtatutopoteza wengi ambao hatupendi kulazimisha mambo. Rudisheni muonekano wa zamani tulioupenda.
Mngekuwa hata mnaongeza vitu bila kubadili muonekano sana.
Muda hautoshi. Naishia hapa.
 
JF uongozi.
Kwa heshima na taadhima naomba msikilize mtoa mada.

Hii iko bomba sana. Ya sasa
 
Wakuu,

Tupo kwenye hatua za mwisho kuja na JF yenye mwonekano mpya ambayo inaendana na mabadiliko ya teknolojia. Kwa wanaohitaji kuwa sehemu ya majaribio, mnakaribishwa...

Katika mabadiliko haya, huenda ukakutana na kitu kikakufurahisha, kikakuchanganya, kikakufanya uone kuna haja ya kuongeza au kupunguza n.k - usisite kutujulisha kupitia uzi huu.

Thread hii itatumika kukusanya maoni yenu na yatazingatiwa ajili ya kujenga sehemu bora na salama zaidi kwa ajili ya kila mmoja wetu.

Kwa wale watumiaji wa App, tunashauri kujaribu App Mpya ya JamiiForums: Fuata hatua hizi kwani itaendana vema zaidi na kinachokuja.

Tunawashukuru kwa ushirikiano mnaotupa kila mara kwani hadi toleo hili ni tokana na maoni yenu.

Kutakuwa na features kadhaa hazitakuwa released mapema hadi zikamilike kufanyiwa testing ndipo ziwe applied.

Tunawapenda, tunawajali na tunaahidi kuendelea kutoa huduma bora.

Asanteni sana!

===== UPDATES======

Changes on the new version:

1) Kuna urahisi wa kufichua mambo mazito bila data zako zozote kuchukuliwa na bila post kwenda public kwanza (utaona button ya Fichua Uovu). Hii itasaidia hata wasio wanachama (baadae) kushiriki kikamilifu kupinga ufisadi na rushwa kwa ujumla.

2) Faragha ya mwanachama imelindwa zaidi, hakuna wa kujua wewe ni nani on JF bila wewe kumpa access ya kifaa chako (simu, tablet au pc). Tulipata vilio vya watu kuchunguliwa IDs tukaja na suluhu.

3) Unaweza kuchagua kutumia JF ikiwa light version, dark mode au dark blue mode (my favorite).

4) Maandishi ya sasa yanasomeka kirahisi zaidi na wenzetu wenye uoni hafifu. Wasioona kabisa lakini wana vifaa vya kusomea wataweza kuitumia JF kwa urahisi zaidi.

5) Soon kuna mambo mapya yanaanza kufanyika via JF, mabadiliko haya yamelenga kupokea yajayo kuanzia mwezi huu na kuendelea.

6) Ukiwa kwenye forum yoyote, huhitaji kubonyeza Page 2, Page 3, Page 4. Wewe vuta kwenda chini tu, mada zitakuja (scroll down).

Nitaendelea…
Watu awaitaki ii new interface si mtusikilize wateja wenu au na ili ni swala la katiba mpya
 
Muonekano mpya si rafiki, Muonekano wa awali uliniwezesha kupata heading nyingi kwenye screen ya simu yangu.

Hakukuwa na usumbufu wa ku scroll ili kusoma headings nyingine kama ilivyo sasa.
Nilitaka kuandika hili. Warekebishe maana ni kero mno kuscroll just for titles. Maxence Melo
 
Chondechonde Maxence Melo mabadiliko yako yasije kuhusisha pesa tu,ila mode ya zamani kabla ya hii mpya uliyoiweka ilikuwa ni nzuri sana
 
Back
Top Bottom