Mabadiliko ya Tabia Nchi isiwe kichaka cha kuwanyima huduma muhimu wananchi

Mabadiliko ya Tabia Nchi isiwe kichaka cha kuwanyima huduma muhimu wananchi

OLS

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2019
Posts
426
Reaction score
685
Mtanzania ukimpa sababu, umemaliza, ataitumia sababu hiyo kila sehemu. Ukizungumzia umasikini wa bongo watasema ni kwa sababu ya ukoloni ambao umeisha miaka 60 iliyopita lakini bado hakuna hatua serious. Kwa sasa dunia ipo kwenye agenda ya Mabadiliko ya Tabia nchi, na Tanzania imeichukua suala hilo kuwa sababu ya kutokuwa umeme thabiti na maji kwa muda wote.

Natambua uwepo wa Tabia Nchi ila sikubali suala hili kuwa sababu ya uhaba wa maji unaondelea nchini. Sababu zangu ni

1. Suala la maji halitegemei miti, ni aibu kwa karne hii kutegemea mvua wakati tunajua yako maji mengi ardhini.

2. Miti hutumia muda mrefu kuwa mikubwa je, tutakaa bila maji hadi miti iwe mikubwa?

Jamani, mabadiliko ya Tabia nchi yameanza lini, maana suala la maji kuwa adimu ni tangu enzi na enzi. Suala tu kwa kipindi hiki mmetukazia maana zamani walau tuliamka usiku kukinga maji.

Hatuoni aibu dhidi ya watu ambao wako jangwani, ambao hawana shida ya maji mbali na kutokuwa na miti kabisa? Huku mvua zikiwa haba na mito ya kutiririsha maji ni jambo geni kabisa kwao.

Huu ni uzembe ambao tumekuwa nao kwa muda mrefu, hatufikirii namna bora ya kuweka huduma thabiti na kwa kuwa dunia inatusaidia kutupa sababu. Tunatembea nazo bila kujua kwamba suala la maji kwa Tanzania halitakiwi kuwa shida kutokana na wingi wa maji ardhini na juu ya ardhi tulionao.

Mabadiliko ya tabia nchi isiwe kichaka
 
Tuna viongozi ambao tunawalisha na kuwatunza kwa kodi zetu lakini si watu wa kutafuta solutions bali ni wa kutupatua excuse
 
Back
Top Bottom