Kwa hali iliyopo sasa dunia inaitaji huduma ya mawasiliano ya mtandao hasa huduma ya internet zaidi kuliko aina yeyote ya huduma za mitandao kwaajiri ya kurahisisha mawasiliano na upatikanaji wa habari kwa urahisi zaidi. Ila kwa tulipo fikia sio tu kutuumiza wananchi wa hali ya chini bali nikutunyima kabisa kama sio kidogo na sisi sehemu ya kuweza kupata huduma hiyo ya internet kutokana na gharama zake kupanda.
Siwezi sema kosa ni la wamiliki wa makampuni yanayotoa huduma za mitandao kwan wao wamefanya sawa na maelekezo wanayopewa na mamlaka husika ila naweza sema kosa ni la mamlaka husika kakita ufanyaji wa maamuzi usio endana na hali halisi ya watumiaji wa hizo huduma.
Sasa ni mda wetu watumiaji na sisi kupaza sauti offline (kama mtaani wanavyo sema) ni mda wetu kuuvua uoga, kuvua kutegeana, kuvua kutegemea flan akusemee, ni mda wa kusimama na kupaza sauti juu ya ongezeko hili la gharama na masharti yasiyo zingatia mahitaji ya mtumiaji kama kufungiwa kutuma sms baada ya kutuma sms100 ndani ya lisaa limoja.
Kabla hujafanya maamuzi mfikilie yule mkulima aliekuwa anatumia internet kupost mazao yake mtandaoni. Mfikirie yule mwanafunzi aliekuwa anasoma online courses na kutafta online academic materials, mfikirie yule mama ntilie aliekuwa akipost chakula chake insta ili kuwavutia wateja wake, mfikirie yule kijana alikuwa anatakiwa kufanya online interview, mfikirie yule mfanyabiashara ambae internet ndio duka lake na mwisho jifikirie wewe mwenyewe.