Huwezi kufahamu nchi yaendaje kwa kuhudhuria taratibu za mahakamani.
Kuifahamu nchi kwa mapana yake kwa kutumia kesi ya Mbowe si lugha sahihi, kwani ofisi za mabalozi hao na wadau wote wa maendeleo wa kigeni zipo nchini miaka nenda rudi, hivyo tayari taarifa zote kuhusu nchi hii wanazo.
Kitendo cha kuwa wanatekeleza taratibu za kidiplomasia kwa kuwasiliana na serikali ya nchi mwenyeji kisha kusimama bega kwa bega na watuhumiwa mahakamani waona ni sahihi?
Yaani wangefanya hivyo kule Russia, au China?
Au sisi tungefanya hivyo kule Marekani au Canada au Uingereza?
Si mtu ungeanza kufuatiliwa una malengo gani dhidi ya nchi mwenyeji?
Kwani wanapowasilisha zile "credentials" kwa raisi zimeandikwa kuhusu kuingilia shughuli za kisiasa za nchi mwenyeji?
Haya ni masuali ambayo tukiweka ushabiki wa siasa pembeni twaweza kujiuliza kwa upande wa diplomasia.