Alama ya upinde wa mvua ina tatizo gani?
Upinde umekuwepo kwa mujibu wa Biblia baada ya Gharika; umetumika kama alama ya matumaini kwa vizazi kadhaa.
Zipo bidhaa, taasisi na mashirika yanayotumia alama ya upinde; leo tatizo ni nini?
Vipi kama hao wafedhuli watu wa LGBTQ wangeamua kutumia alama ya Jua - SUN au mwezi? Mngekuwa hamtoki nje kupigwa na miale ya Jua?
Mbona kama tunawapa promo zaidi kwa kuwatangaza kila siku katika kila jambo?
Embu jiulize leo watu wa LGBTQ na wengineo walioamua kuishi kwa namna wanayotaka, siku wakiamua kutumia alama ya mmea wa ngano, mpunga na mahindi mtaacha kula mikate, wali, pilau ikiwemo biriani na mtaacha kula ugali au mikate?
Tusipende kuvipa nafasi kubwa kwenye maisha vitu ambavyo hauna maamuzi navyo; jishughulishe na kile ambacho ni cha msingi zaidi katika maisha yako na familia.
Tuna matatizo mengine makubwa zaidi ambayo tunapaswa kupambana nayo kwa nguvu zaidi kuliko kushughulika na picha ya upinde wa mvua.
Halafu kila Mtanzania anakataa kwamba yeye sio mhusika kwenye LGBTQ lakini mkifumania mtu na mke wa mtu adhabu yetu pendwa ni kumlawiti?
Wanawake wengi wanakiri kuwa wanaume wengi wa siku hizi wanapenda kinyume na maumbile.
Sasa mtu ambaye unaweza kumwingilia mwanamke kinyume na maumbile kipi kinakutofautisha na hao wanaume walioamua kuwa mashoga.
Ikumbukwe kuwe anayeingiliwa na anayemwingilia mwenzake wote ni ''Mashoga''
Kwanini tunapenda kuficha maovu yetu kwa kichaka cha kuwalaumu sana hawa LGBTQ?
Kwanini kila mmoja wetu asiwe responsible kwenye maisha yake kwanza kabla ya kutaka kuubadilisha ulimwengu.
Watoto wanabakwa na kulawitiwa kila siku na jamii inajifanya kuwa haioni kabisa.
Watu wanaiba hela za serikali, hospitali huduma mbovu lakini haya sio masuala yanayoleta mjadala.
ZINGATIA: Simaanishi wala siungi mkono kwamba hao LGBTQ wapo sahihi lakini pia mimi ni nani kuwaamulia wanadamu wengine namna ya kuishi.