Mabango yenye picha za Hayati Magufuli yaanza kuondolewa barabarani na kwenye ofisi za chama

MATAGA watakuwa wanayachukua kwa ajili ya kumbukumbu kama sikosei, maana sio kwa mapambio waliyokuwa wanashusha kila kona.
Jamaa alichofanikiwa nikuwashika akili akawaachia miguu ndo ikawa inafanya kazi

Asilimia 70% ya watz walkuwa wanaishi kwa kutumia akili ya mwendazake
 
Kinachofurahisha zaidi hata picha zake kwenye maofisi zitakuwa zimeshateremshwa chini!!!! UTARATIBU wetu ni picha ya Baba wa Taifa na Rais aliyeko madarakani ndizo hubandikwa maofisini. Mungu ni mkubwa sana aisee.
 
H
Nakuhakikishia hizo picha zitaondolewa kwenye maofisi tu na barabarani lakini kamwe hazitaondoka Facebook, Instagram na majumbani mwa watu
Nyumba yangu ina picha ya baba wa Taifa. Ya Pili itakuwa ya Mh. Rais Samia Suluhu Hassan. Huyu ndiye Mungu alimteua baada ya kuandika "YATOSHA" kwa watanzania. Imetuasa kuwa usilitaje Bure jina la Mungu wako kama unalitaja kuficha uovu wako. Mungu hadhihakiwi kabisa. Na iwe fundisho.
 
Kwanza ilikuwa ni uvunjifu wa sheria za uchaguzi, mabango ya kampeni kuwepo maeneo hayo siku ya uchaguzi. Miaka yote, tulikuwa tukishuhudia hayo mabango, kuondolewa siku ya mkesha wa uchaguzi. Lakini kwa vile Nchi ilikuwa inaendeshwa KI-MAGUFULI, na kwa vile ilikuwa ni faida kwake, TUME YA UCHAGUZI haikusema chochote kuhusiana uvunjaji huo wa taratibu za uchaguzi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…