Mabango yenye picha za Hayati Magufuli yaanza kuondolewa barabarani na kwenye ofisi za chama

Mabango yenye picha za Hayati Magufuli yaanza kuondolewa barabarani na kwenye ofisi za chama

Kweli kufa kufaana! Haya mabango yalitarajiwa kudumu mpaka 2025! Na hakuna ambaye alijaribu hata kuyagusa tu na mkono! Ila leo yanatolewa kwa kutupwa tu chini!

hayaheshimiki wala kuogopwa tena!
Kwenye ofisi za serikali ni lazima yaondolewe ili kupisha picha ya Rais mpya!! Ila huyo anayeyaondoa Kama anavyoonekana kwenye clip amekosa adabu!! Hakutumwa ayaondoe kwa chuki hivyo! Inabidi achukuliwe hatua!! Ameonesha chuki ya binafsi!
 
Orodha ya maraisi walio fariki Tanzania
1. HAYATI MWALIMU J.K NYERERE
2. MAREHEMU MZEE MKAPA
3. MWENDAZAKE..............
 
Daaah Maisha ni hadithi!!
Yalibandikwa kwa fujo na sasa yanaondoshwa kwa fujo!!
 
Inaonekana mnaumia sana. Maana tayari tuna Rais mpya hata picha maofisin zimeshatolewa ipo ya nyerere na mh samia
 
Jamaa watamsahau na kumtupa hadi huko aliko kama anaona atapigwa na butwaa!

Kweli CCM si watu wema.
 
Kwani hayo mambango yana kazi gani?
Mbona Yalitakiwa kuondolewa mara tuu baada ya uchaguzi kwisha?
Gia angani ? Hata wewe haya mabango yalitakiwa yajengewe temple kila yalipo ili waimba mapambio ya kusifu na kuabudu , wewe na kundi lako mpate pa kuabudia jamani , mbona mapema hivi ?
 
Back
Top Bottom