Mabaraza ya Katiba: Dr. Slaa ndani ya Ukonga, Uwanja wa Kampala ulioyopo Gongolamboto

Mabaraza ya Katiba: Dr. Slaa ndani ya Ukonga, Uwanja wa Kampala ulioyopo Gongolamboto

Mwita Maranya

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2008
Posts
10,565
Reaction score
7,984
Tayari katibu mkuu wa Chadema Dkt. Slaa ameshawasili uwanjani. Mjumbe wa kamati kuu anatoa maneno ya utangulizi.
Viongozi wengine walioambatana nae ni Mama Kaihula-mbunge, Katibu wa mkoa Mzee Chacha, Mwenyekiti wa Segerea kamanda Mchele na wengine wengi.
 
Mkutano wa ukusanyaji wa maoni umeanza hapa Gongo la Mboto. Idadi ya watu waliohudhuria ni wengi na tayari Dr. Dlaa ameshasili na kabineti yote.

Stay tuned kila kitu utakipata hapa hapa.

IMG_0173.JPG

IMG_0176.JPG

IMG_0164.JPG
 
Wakili Edson Mbogolo ndiyo yupo jukwaani akitoa elimu kwa raia juu ya umuhimu wa kutoa maoni ya katiba mpya.
 
Wananchi wanagawiwa rasimu ya katiba mpya ili baada ya elimu waende wakajisomee na mabaraza yatakapopita watoe maoni kwa weledi wa l
kutosha
 
Mjumbe wa kamati kuu kamanda Edson Mbogoro anatoa utangulizi juu ya historia na umuhimu wa katiba na umuhimu wa wananchi wote kushiriki kutengeneza katiba itakayokuwa bora na manufaa kwa miaka mingi ijayo.
Anatolea mfano wa katiba ya marekani iliyotengenezwa zaidi ya miaka miatatu na imedumu hadi leo kwakuwa ilizingatia maslahi ya wamarekani na kuweka kando maslahi ya vyama vya siasa hasa republican na democratic kwakuwa waliweka mbele utaifa.
 
Watu wametulia sana kusikiliza nondo juu ya elimu ya uraia hasa kipengele cha uwazi ambacho kimenyambuliwa saizi.
 
Mwanasheria Mbogoro anaendelea kusema Chadema inaunga mkono tunu saba kuwemo katika katiba kama inavyopendekezwa na tume. Ccm wanapinga tunu ya uwazi kwasababu ya historia yao ya wizi na ufisadi katika mikataba mbalimbali wanayoingia bila uwazi. Mathalani mkataba wa buzwagi uliosainiwa hotelini, mikataba 17 baina ya Tanzania na China.
Uwazi ni lazima uwe kwenye katiba hata uendeshaji wa serikali.
Wananchi wanapaza sauti kuunga mkono uwazi na kuipinga ccm na msimamo wake.

Namuona hapa amewasili Mzee Kimesera.
 
mmhhh....mbona majanga , je waweza kunithibitishia kuwa "moderator" wa hiyo kitu kuwa atakuwa "impartial?" ili kuondoa unnecessary "biasness"
COZ kwani wananchi wanatakiwa kuwa huru kutoa mawazo yaliyopo vichwani mwao na sio yaliyopo kichwani mwa babu zilipendwa. ni hayo tu.
 
Huyu Edson Mbogolo ni mtu hatari kwa jinsi anavyochambua hoja katika hii rasimu ya katibaa mpya. Saizi anazungumzia maadili ya viongozi kwa jinsi yalivyojadiliwa katika katiba mpya.
 
Kamanda Mbogoro anaendelea; Chadema inaunga mkono rasimu juu ya haki zote za kiraia, kiuchumi na kijamii kwa makundi yote hasa wakulima, wafugaji na wafanyabishara wadogo, haki zao zitambuliwe kikatiba ili wawe na uwezo wa kuzidai mahakamani inapotokea hazijatimizwa.
 
mmhhh....mbona majanga , je waweza kunithibitishia kuwa "moderator" wa hiyo kitu kuwa atakuwa "impartial?" ili kuondoa unnecessary "biasness"
COZ kwani wananchi wanatakiwa kuwa huru kutoa mawazo yaliyopo vichwani mwao na sio yaliyopo kichwani mwa babu zilipendwa. ni hayo tu.

Kuna upotoshaji mkubwa sana ubaofanywa na magamba baada ya kuona wameshindwa kuelimisha wananchi na kuwahamasisha juu ya utoaji wa mawazo ya rasimu ya katiba mpya.
 
tena wewe una njaa mbaya manake umepost na hakuna comment hewani umebaki wewe mwenyewe au hujajiona kama sio cheap labour ni nini sasa

Anyway huo ni mtazamo wako duni endelea wewe na huo utajiri wako wa kifisadi.

Kama huna cha kucomment acha wapo watakaokuja kuchangia.
 
Mkuu Maranya vipi viongozi wa serikali Ukonga wamehudhuria? Kwa sababu huu mkutano wa katiba na siyo wa kisiasa
 
Kamanda Mbogoro: ibara ya 20 juu ya miiko ya uongozi wa umma. Chadema inaunga mkono asilimia mia ili kukomesha tabia ya wafanyabiashara kuhamia kwenye uongozi wa umma na kuzitumia kujinufaisha kibinafsi. Mali za viongozi zifahamike kwa uwazi na bayana ili kulinda na kuheshimu maadili na miiko ya viongozi. Wananchi wanapaza sauti kuunga mkono mapendekezo ya rasimu juu ya miiko ya uongozi wa umma.
 
Back
Top Bottom