Mabaraza ya Katiba: Dr. Slaa ndani ya Ukonga, Uwanja wa Kampala ulioyopo Gongolamboto

Mabaraza ya Katiba: Dr. Slaa ndani ya Ukonga, Uwanja wa Kampala ulioyopo Gongolamboto

Dr anaendelea kutoa elimu ya uraia,Mwita,Malemo endeleeni kufikisha ujumbe kwa watu.
 

Attachments

  • uploadfromtaptalk1377350277685.jpg
    uploadfromtaptalk1377350277685.jpg
    45.3 KB · Views: 145
Dkt. Slaa anasema Chadema inaunga mkono mia kwa mia juu ya mapendekezo ya rasimu ya katiba juu ya kutoa ulinzi wa wananchi dhidi ya umasikini, manyanyaso na dhulma wanazofanyiwa wananchi kutoka kwa viongozi na watendaji wa serikali.

Sasa wananchi wanaanza kutoa maoni yao.
Mwananchi wa kwanza Joel Chacha anapendekeza maadui wa taifa watambuliwe kikatiba. Zamani tulikuwa na maadui watatu ujinga, maradhi na umasikini lakini sasa ameongezeka adui rushwa. Wananchi wote wanamuunga mkono juu ya rushwa kuongezwa kuwa adui wa taifa!
 
Mwananchi 2; Anapendekeza katiba itambue haki za kiraia za wananchi ambazo ni pamoja na kitambulisho cha uraia ili kulinda na kutambua haki za raia dhidi ya wageni na wakimbizi/wahamiaji. Katiba iziainishe ili zikinyimwa basi mamlaka husika kama NIDA waweze kushitakiwa mahakamani.
Wananchi wote wanalipuka kwa shangwe na wanamuunga mkono.

Mwananchi 3: anapendekeza muundo mpya wa baraza la ulinzi na usalama ambalo raisi si mwenyekiti wake, ambalo litapendekeza wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama na raisi afanye kumtangaza tu!
 
Mwananchi 5; Anapendekeza katiba imtambue mwananchi kuwa ndiye mmiliki wa ardhi na raisi asiwe mdhamini ama asiwe na mamlaka yoyote juu ya ardhi ya mtanzania. Mwananchi mwenyewe awe na umiliki wa ardhi na kama kuna mtu ama mwekezaji ama serikali inaihitaji ardhi yake basi mwananchi mwenyewe awe na mamlaka ya kuzungumza juu ya kuuziana.
 
Usitume tena mpaka wakupe buk 5 yako,hawashindwi kukutosa kama ilivokuwa kwa Ludo,
 
Mwananchi 6; Anapendekeza kuwa katiba iwape watanganyika haki ya kumiliki ardhi visiwani Zanzibar kinyume na sasa ambapo watanganyika hawaruhusiwi kumiliki ardhi zanzibar lakini wazanzibari wanamiliki ardhi huku bara.

Dkt. Slaa anafafanua kuwa katiba ya sasa haimzuii mtangabyika kumiliki ardhi zanzibar isipokuwa kuna sheria ambazo ni kali kidogo ili isijekutokea watanganyika wameijaza zanzibar. Kama kuna mtu anazuiwa pamoja na kufuata sheria basi ni makosa.
 
Mwananchi 7; Anapendekeza katiba iainishe na kutambua muwekezaji awe wa ndani au wa nje, awe mtu binafsi au taasisi. Kitamkwe kiwango cha uwekezaji cha mtaji ama teknolojia anayotakiwa kuwa nayo muwekezaji ili kutambuliwa badala ya huu uhuni unaofanyika sasa.

Mwananchi 8; Anapendekeza katiba itambue haki ya huduma za kijamii hasa afya ili watu wote wapate huduma bora za afya kwa usawa badala ya sasa ambako kuna madaraja ya haki za kiafya ambapo viongozi wanatibiwa India na ulaya huku wananchi wakikosa madawa hapa nyumbani.
 
Mwananchi 9; ANAPENDEKEZA Raisi asiwe na kinga ya kutoshitakiwa akiwa madarakani ama hata akitoka madarakani ili kuwafanya maraisi wawajibike kwa uadilifu na kuondoa tabia ya maraisi kujifanyia mambo kiholela kwakuwa hawezi kuguswa.

Mwananchi 10; Anapendekeza serikali itoe pensheni kwa wazee wote bila kujali kama alifanya kazi serikalini ama alikuwa mkulima, mfugaji, mmachinga ama mfanyakazi wa ndani.
 
Mwananchi 11; Anapendekeza wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa wasiwepo. Na kama wakiwepo wasiteuliwe na raisi bali wachaguliwe na wananchi wenyewe kwa kupigiwa kura na vilevile majukumu yao yabainishwe kikatiba kuliko ilivyo sasa ambapo kazi wanazofanya ni kuhudhuria katika matukio ya maafa na kufungua matamasha na makongamano bila kusahau kuhujumu vyama vya upinzani.

Angalizo: wakuu wa wilaya na mikoa wanalipwa mishahara mikubwa sawa na wabunge lakini hakuna tija yoyote wanayochangia katika uchumi na ustawi wa nchi.
 
Mwananchi 12; Anapendekeza katiba itoe haki kwa wananchi kuhudumiwa kikamilifu na serikali kwa kiwango kinachokubalika pale wanapokumbwa na majanga ya milipuko ama mafuriko.
Kwa uzoefu uliopo serikali imekuwa haiwajibiki kabisa kwa wananchi hata misaada inayotolewa kusaidia waathirika imekuwa ikiwanufaisha viongozi wa serikali zaidi kuliko waathirika wa majanga.
 
Dkt. Slaa anafafanua juu ya mapendekezo ya rasimu ya katiba juu ya suala la dini. Kwa miaka mingi sana watanzania tumeishi pamoja bila kujali ama kubaguana kwa dini zetu kwahiyo ni muhimu kama taifa tukaheshimiana na kustahimiliana kwa imani zetu huku tukiweka mbele utanzania wetu.
 
Dkt. Slaa anamalizia kwakuwataka watanzania kuweka mbele utaifa wao utanzania wao kwakuwa vyama vya siasa vitapita lakini nchi ya Tanzania itaendelea kuwepo.

Sasa kamanda Waitara anapanda jukwaani kutoa matangazo ili kutoa fursa ya kufunga mkutano.
 
Mwita Maranya
Asante sana mkuu
Pamoja sana...wananchi wameamka sana pande hizo...



Dkt. Slaa anamalizia kwakuwataka watanzania kuweka mbele utaifa wao utanzania wao kwakuwa vyama vya siasa vitapita lakini nchi ya Tanzania itaendelea kuwepo.

Sasa kamanda Waitara anapanda jukwaani kutoa matangazo ili kutoa fursa ya kufunga mkutano.
 
Hivi haya mapendekezo ya Dr.Slaa yatatumika wapi.
 
Dkt. Slaa anamalizia kwakuwataka watanzania kuweka mbele utaifa wao utanzania wao kwakuwa vyama vya siasa vitapita lakini nchi ya Tanzania itaendelea kuwepo.

Sasa kamanda Waitara anapanda jukwaani kutoa matangazo ili kutoa fursa ya kufunga mkutano.

Asante sana mkuu Mwita Maranya kwa kazi nzuri.Nimekuwa kama niko mkutanoni.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom