MwanaDiwani
JF-Expert Member
- Mar 22, 2013
- 5,536
- 2,266
Misimamo wa wananchi wengi ndiyo upi huo wakati wanaowawakilisha ni wananchi wengi waliowachagua. Huku ni kuwadharau na kuwatukana wananchi wengi waliowachagua kwa mujibu sheria ya mabadiliko ya katiba kifungu cha 83.Kama ungekuwa na akili timamu ungetambua kuwa hakuna namna unaweza kuijadili rasimu ya katiba kwa siku moja ama mbili na kuimaliza.
Kama ungekuwa na akili timamu ungegundua kuwa kinachofanyika sasa ni kuangalia maeneo yanayohitaji kuboreshwa na ndio maana Chadema tumeamua kwenda kwa wananchi wenyewe watoe maoni yao ili sisi tuyafikishe tume kwakuwa wajumbe wengi wa mabaraza ya katiba ya wilaya ccm imeyachakachua kwa kuwalazimisha wanachama wake kukariri msimamo wa chama badala ya msimamo wa wananchi wengi waliowachagua na kuwatuma huko.
By the way, CHADEMA ni kama taasisi, asasi au kikundi cha watu wenye mtazamo mmoja katika macho ya sheri ya mabadiliko ya katiba lakii kikubwa zaidi, Tume ya Jaji Warioba haitachukua maoni ya jukwaani wala ya kwenye Helikopta.
Endeleeni na mikutano yenu ya kwenye helikopta na majukwaani.