Mabasi aina ya Scania na Mercedes Benz vs Yutong na Zongtong: Mchina ameuza ramani ya vita kwa adui

Inabidi tutoe maoni yetu kwa hawa wabunge wetu labda wanaweza badilisha hizi sheria zao za kishamba
 
Inabidi tutoe maoni yetu kwa hawa wabunge wetu labda wanaweza badilisha hizi sheria zao za kishamba
Kama pesa ya kuleta hiyo bus ipo, ilete tu ukizungumza nao vizuri watakuruhusu tu!

Kipindi cha nyuma ilikuwa ni lazima pulling iwe na ekseli 7, semi trailer iwe na ekseli 6 lakini sasa hivi pulling zenye ekseli 8 na semitrailer zenye ekseli saba ni nyingi tu.

Na kuna semi trailer inavuta denglar yenye ekseli mbili (10 ft long).

Hivyo ni swala la wewe umejipangaje

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakuelewa sana kaka! Ila tuliwahi kukwambia hapa hapa kuhusu volvo na ulitukatalia kabisa.

Kuna ile FH16 610hp ya wanalambalamba, waliiuza mahali siku ukiiona utastaajabu sana, imekuwa takataka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakuelewa sana kaka! Ila tuliwahi kukwambia hapa hapa kuhusu volvo na ulitukatalia kabisa.

Kuna ile FH16 610hp ya wanalambalamba, waliiuza mahali siku ukiiona utastaajabu sana, imekuwa takataka

Sent using Jamii Forums mobile app
Haha mlima siikumbuki Kama tuliwahi kuongea habari ya ubora wa Volvo, Ila nafahamu kuwa vovlo ni gari nzuri sana , sema shida yake zikichoka ndo zinasumbua
Kwenye suspension kwa mfano vovlo Wana 4point airbags kwa Kila axle , ndo system hii ipo kwenye daf , strallis , man pamoja na mercedes ,system hii gari ikichoka huwa inasumbua sana

Vovlo zenye horse power kubwa ndio kabisa hazina maisha , lambalamba alikuwa nazo 610 na 660 Kama sikosei , nadhan zote zipo hoi,
Fh 16 ilitabiriwa na wataalamu kuwa isingeweza kuishi maisha marefu , zilikuwa ni mbio za kupambana na scania interms of power , scania alipotoa 580 vovlo akaja na 610, ilipo toka 620 vovlo akaja na 660, ilipotoka R730 vovlo akaja na 750 ,mechanically speaking ni risks sana kutoa HP nyingi kwa idadi ndogo ya cylinders , vovlo fh 16 unazungumzia cc 16000, maana yake Kila cylinder ina ujazo wa cc 2600, put it simple Kila cylinder moja ya fh 16 ni zaidi ya ujazo wa engine ya 1jz ambayo ni 2500cc, challenge kubwa aliyokuwa anapambana nayo vovlo ni excessive vibrations kutokana na ukubwa wa cylinders , na ndio inayouwa engine , ,watu wa scania wao HP kubwa kubwa zote wanadeliver kupitia V8, naturally firing oder tu ya v8 huwa inaondoa vibrations.
Kuna uwezekano hii 770 ikawa king kwa muda mrefu maana reputation ya vovlo 750 ilikuwa mbaya sana na vovlo huenda wameamua kuachana na mpambano na scania
 
Saizi Bongo Inter-link trailers zimeanza kuwa nyingi, hizo Dangler wamiliki wa semi-trailer wameanza kuzifunga Kwa fujo.
Ila Specialized Hauliers kavunja anavuta dangler na tela za tipper.
 
Saizi Bongo Inter-link trailers zimeanza kuwa nyingi, hizo Dangler wamiliki wa semi-trailer wameanza kuzifunga Kwa fujo.
Ila Specialized Hauliers kavunja anavuta dangler na tela za tipper.
Hahahaha sipo bongo muda sasa, hizo dangler za spec. Hauliers anasombea makaa au zinabeba nini?

Interlink mlipigwa mkwara mkaleta vifupi vifupi ila trust me, ni swala la muda tu tutaanza kuziona zile ndefu kama za mataifa mengine

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Special sijajua anabeba nini, maana zinapotoka Dar naziona zinavuta Dangler na zimefunikwa turubai.

Interlink naona Simba Logistics na wakina Salman Transport wanakomaa nazo.
 
Kwenye game la kubeba makaa ya mawe saizi gari zipo kampuni kibao. Mwezi wa 5 nilikuwa Songea nimekutana na gari nyingi za kampuni imeandikwa Dollow Boy/Tuxson huyu na Benz za warwanda. Special itakuwa kapunguza nguvu kule kahamia mazima kazi za Mbagala-Bandari kubeba Bulk cargoes.
 
Nimekupata vyema kaka! Naomba nikuulize vitu kadhaa..

Vifuatavyo vinaathari yoyote kwenye horsepower & torque? Kama athari zipo ni kwa namna gani?

- axle configuration (6×6, 6×4, 6/4×2)
Hapa zungumzia R420 tractor.

-driving/propeller shaft (urefu & ufupi)
Hapa zungumzia R420 tractor(shaft fupi) & R420 rigid (shaft ndefu).
Hii tractor na rigid zote ziwe na same axle configuration sana sana 6×4

-hub reduction
Hapa zungumzia R420 rigid 6x4, moja iwe na diff za kawaida na nyingine iwe hub reduction.

-customisation /modification
Mf. R420 4×2 tractor ambayo ni stock, ikarefushwa chassis na shaft then ikaongezwa diff na kuwa 6×4! ile max . torque na hp at a certain rpm zitachange au zitabaki kama ilivyokuwa stock?

Lengo kuu nahitaji kujua max. Torque &hp at a certain rpm haziwezi kuathiriwa na hivyo vikorombwezo hapo juu?

Nakaribisha michango ya wadau wengine pia.
Asante!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizo benz za TransAfrica, zinapitia dodoma kwenda kwao japo kuna baadhi niliwahi kuziona kajiado kenya!

Dollow boy niliziona kipindi fulani mwanza zikiwa pamoja na wanalizombe walipeleka makaa bandarini pale..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mlima
Honestly sielewi kwa nn transporters bongo wamezishobokea interlink zenye masharti kibao, ukiacha ufupi pia zimekuwa limited kwenye tani 56, Yani hakuna tofauti kubwa na dolly (pulling)
Sasa unaoperate magari matatu, matairi kibao halafu hakuna tija , southern huko interlink ipo na 70 gvm
 
Unataka kusema nini? Mabasi yote yamefungwa speed limit, barabarani Kuna touch, huo mwendo Ni upi? Issue kubwa hapo Ni unafuu wa manunuzi na uendeshaji wa mabasi ya kichina basi.
unaonekana husafirigi sijajua unaishi wapi wewe ..pamoja na limit na tochi bado kuna watu wanapigwa gape ya masaa mawili
 

Huyo jamaa hasafirigi naona ..nishapanda bus flani gps speedometer ilikuwa inasoma top speed ni 102 tu muda mwngi tulikuwa tunacheza na 88 to 95....ndo siku nilijua kuwahi sio lazima ufike 150kph ..just maintain ile speed tu ....

Kuna kipande kilikuwa na 78km pamoja na bamsi zote kubwa milima ila tulitembea kwa lisaa limoja kamili kitu ambacho hakiwezekani kwa costa yenye abiria hata iwe haina vts ingetumia zaidi ya ule muda

Gari ndogo eg cresta tumetembea nayo zaidi ya kilometa 200 pakinyooka hamna bamsi inawapita kama mmesimama ila sisi tume maintain ile 88 muda wote ..kuna bamsi tulipita na 72kph then within less than 8sec tayari tuko pale pale kwenye 88kph

Ngoma mapema sana mjini stand shangwe za kutosha
 
For some reason ufupi wa propeller shaft huongeza ufanisi , ndio sababu g series huwa zinakuja na shaft fupi.
Hub reductions ni kwa ajili ya performance pia Ila ni option kwa wale wanataka high torque kutoka kwenye engine ndogo, hub reduction zipo za Aina mbili high speed na low speed , high speed ,
Tukija kwenye axle configuration 6x2 tag ndio the best kwa torque maana hii huja na propeller fupi , 6x4 ni kwa ajili ya off road applications
 
Kwa faida ya wengi, tunaomba ufafanue "drive train" ni Nini na inafanyeje kazi?

Vitu vinavofanya kazi kwa pamoja ili chombo kiende

Eg kwenye baskeli drive train ni jembe la mbele mnyororo na rear sprocket ama free hub/ wheel
 

Aya ya mwsho nimegundua na wewe ni infantile

Sometime bora unyamaze
 

Hatuangalii gia unayopanda nayo mlima ila ni kwa speed gani unapanda ....

Kila mtu anajua endesha baskeli itakuwa ya gia kila mtu atapanda mlima flan hata katoto cha 12years ila ni kwa speee gan anapanda?

Hio gia yako ya tano ratio zake unaeza kuta kwangu ni ya nne ratio ndo zile zile...

Ni kama honda shadow yenye gia 5 ikiwekwa tatu ikavutwa toyo haifurukuti😁
 
Unataka kusema nini? Mabasi yote yamefungwa speed limit, barabarani Kuna touch, huo mwendo Ni upi? Issue kubwa hapo Ni unafuu wa manunuzi na uendeshaji wa mabasi ya kichina basi.
Hakuna cha speed limiter wala nini. Majuzi nilikua naendesha Dar - Iringa, nikiwa speed 110 nilipitwa na basi kama nimekaa. Nikabaki nashangaa tu iwapo kweli limiter zinafanya kazi
 
[emoji119][emoji119][emoji119]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…