BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Uamuzi huo umetolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Ardhini (LATRA) baada ya kubaini Mabasi hayo kuchezea Mfumo wa Kufuatilia Mwendo (VTS) kwa lengo la kusafiri kwa Mwendokasi ili kushindana kufika Stendi.
Kwa mujibu wa LATRA, watoa huduma hao wamekuwa wakitumia fursa ya kuanza safari mapema (Saa 9 Usiku hadi 11 Alfajiri) kwa kufanikisha malengo ya kufanya mashindano huku kukiwa na wanaobashiri Basi linalofika mapema wakipata ushindi kwenye Kamari.
Mabasi 6 ya Allys Star na Matatu ya Katarama yamerudishwa kwenye ratiba ya ya kuanza safari Saa 12:00 Asubuhi kuanzia Juni 21, 2023. Aidha Kampuni ya Isamilo imepewa onyo kali la mwisho kabla ya kuchukuliwa hatua stahiki.
--