Mabasi ya Allys Star na Katarama Express yapigwa 'Stop' kusafiri usiku

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826

Uamuzi huo umetolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Ardhini (LATRA) baada ya kubaini Mabasi hayo kuchezea Mfumo wa Kufuatilia Mwendo (VTS) kwa lengo la kusafiri kwa Mwendokasi ili kushindana kufika Stendi.

Kwa mujibu wa LATRA, watoa huduma hao wamekuwa wakitumia fursa ya kuanza safari mapema (Saa 9 Usiku hadi 11 Alfajiri) kwa kufanikisha malengo ya kufanya mashindano huku kukiwa na wanaobashiri Basi linalofika mapema wakipata ushindi kwenye Kamari.

Mabasi 6 ya Allys Star na Matatu ya Katarama yamerudishwa kwenye ratiba ya ya kuanza safari Saa 12:00 Asubuhi kuanzia Juni 21, 2023. Aidha Kampuni ya Isamilo imepewa onyo kali la mwisho kabla ya kuchukuliwa hatua stahiki.

--
Your browser is not able to display this video.
 

Attachments

Wanazi wamechangia sana ile mikeka imefanya madereva wakimbize sana hayo mabasi

Ila ligi yao tamu sana

Kwenye ligi la mabio wapo Happy Nation na Frester vipi wao hawajapigwa ban kuanza safari mida hiyo
Hao frester na happy nation ni sawa na championship. Ally's na Katarama ndio EPL yaani ligi ya wakubwa na ukizingatia Katarama ndio kapanda daraja lakini anasumbua.
 
pole
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…