Mabasi ya Allys Star na Katarama Express yapigwa 'Stop' kusafiri usiku

Mabasi ya Allys Star na Katarama Express yapigwa 'Stop' kusafiri usiku

View attachment 2662535
Uamuzi huo umetolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Ardhini (LATRA) baada ya kubaini Mabasi hayo kuchezea Mfumo wa Kufuatilia Mwendo (VTS) kwa lengo la kusafiri kwa Mwendokasi ili kushindana kufika Stendi.

Kwa mujibu wa LATRA, watoa huduma hao wamekuwa wakitumia fursa ya kuanza safari mapema (Saa 9 Usiku hadi 11 Alfajiri) kwa kufanikisha malengo ya kufanya mashindano huku kukiwa na wanaobashiri Basi linalofika mapema wakipata ushindi kwenye Kamari.

Mabasi 6 ya Allys Star na Matatu ya Katarama yamerudishwa kwenye ratiba ya ya kuanza safari Saa 12:00 Asubuhi kuanzia Juni 21, 2023. Aidha Kampuni ya Isamilo imepewa onyo kali la mwisho kabla ya kuchukuliwa hatua stahiki.

--
View attachment 2662579View attachment 2662580View attachment 2662581
wanazidi kuwapa umaarufu tu
 
Hii ligi huwa inanishangaza kitu kimoja tu, hizo katarama ukikuta wanazi wanavozifia alafu kaangalie mikeka sasa utashangaa mwenyewe.

Yaani kwenye mikeka ni tofauti na wanavozisifia,

Mikeka ya mwezi mzima ally's ndo huwa inafungua geti mara nyingi kuliko gari zote ila sasa wanazi wakute wanasifia katarama!

Kuna jamaa anasema katarama anafika dodoma saa 3 asubui kama vile ni jambo la ajabu!! Wakati hao wote wanatoka saa 9 usiku dodoma wanapitaga wote saa 3
wasukuma toka wazaliwe hawajawahi kuliona g7 so sishangai wanavyolisifia ni sawa na kule mbeya hawakuwahi kuliona g7 mpaka sauli alipolipeleka.....
 
Nani kakwambia biashara ya mabasi unarudisha pesa ndani ya miezi 3?

Si mjinga kulipa Bima ya zaidi ya milioni 180 kwa mabasi 3

Ukiona hivyo hana hela za mawazo
hawa jamaa sijui wanamchukuliaje yule mhaya katarama
waambie tu before hajaingia kwenye mabus ana milori ya kutosha na sheli kama zote....sio mnyonge hata kidogo
 
Yule jamaa katisha ana Number A zimesimama sana

Yeye na World Oil ni balaa

Number A yake kama DSA
nasikia mzungu huyu... na dereva ukikutwa hata na spana tu kazi huna
 
Mi gari yangu ni kiazi kitamu tu[emoji1787] Mwanza Arusha kama napaaa vile,ukiliona kwa nje bayaaaaa,ila moto wake waulize kina loliondo[emoji3]
 
Satco nimewapenda sana Dodoma- Kagera madereva kama wale wa Diplomatic ,

Nimepata mrejesho toka Kwa jamaa zangu wa karibu wana wakubali sana kwa kuendesha kiusalama,

Yaani abiria hadi analala bila kuwa roho juu wala mkononi.

Mwendo wa usalama kabisa,

Hawana break za kustukiza, hawana papara Yaani kama uko kwenye utalii wa ndani vile.

Isijekuwa ni coincidence tu bali iwe ni lifestyle yenu .
 
Abiria wamekaa ndani wamerelax gari yao inaoshwa maji nje kisa imewahi kufika stendi 😅😅😅🤔
 
Satco nimewapenda sana Dodoma- Kagera madereva kama wale wa Diplomatic ,

Nimepata mrejesho toka Kwa jamaa zangu wa karibu wana wakubali sana kwa kuendesha kiusalama,

Yaani abiria hadi analala bila kuwa roho juu wala mkononi.

Mwendo wa usalama kabisa,

Hawana break za kustukiza, hawana papara Yaani kama uko kwenye utalii wa ndani vile.

Isijekuwa ni coincidence tu bali iwe ni lifestyle yenu .
Jambo usilolijua ni sawa na usiku wa giza😂, halafu katika watu ambao hutakiwi kuwasifia kwa ustaarabu ni watu wa mabus coz wanaweza kukushangaza anytime
 
Jambo usilolijua ni sawa na usiku wa giza[emoji23], halafu katika watu ambao hutakiwi kuwasifia kwa ustaarabu ni watu wa mabus coz wanaweza kukushangaza anytime



Ni kweli kabisa nakubaliana na nawe lakini wakati mwingine ukiona mtu anafanya vizuri kumtia moyo sio vibaya!
 
Naona siku hizi Katarama inaingia Dar saa nne asubuhi na saa kumi na moja jioni. Sijui huwa anaondoka Mwanza saa ngapi.
 
Naona siku hizi Katarama inaingia Dar saa nne asubuhi na saa kumi na moja jioni. Sijui huwa anaondoka Mwanza saa ngapi.
Wanatoka mwanza SAA 2 usiku na wanaingia DAR SAA 3-4.
Pia lipo linalotoka DAR 2 usiku na linaingia mwanza SAA 3-4 na wameanza Toka juzi na polo kichaa DXE linatoka SAA 1 usiku hili bus linaitwa kichaa kutokana na speed
 
Back
Top Bottom