Mabasi ya Kilimanjaro yafungiwa kutoa huduma

Mabasi ya Kilimanjaro yafungiwa kutoa huduma

Wahuni hao sina hamu nao. Majuzi stendi yao ya Moshi almanusura nizichape nao baada ya kunikatisha ticket ya basi daraja la juu lakini basi lililokuja ni mkweche kabisa namba "A"

Nikajuta kwanini sikukata ESTHER au TILISHO, baadae nikaamua kukata BM baada ya kurejesha nauli.

Labda wanachoweza kwa sasa ni kusafirisha vifurushi tu ila biashara ya kusafirisha watu imeshawashinda.

Hao ikiwezekana wafungiwe tu moja kwa moja waanze upya
Mbona mkuu unaongea kwa makasirikoo
 
Hii kampuni inaelekea kufa

20240106_221125.jpg
 
Wahuni hao sina hamu nao. Majuzi stendi yao ya Moshi almanusura nizichape nao baada ya kunikatisha ticket ya basi daraja la juu lakini basi lililokuja ni mkweche kabisa namba "A"

Nikajuta kwanini sikukata ESTHER au TILISHO, baadae nikaamua kukata BM baada ya kurejesha nauli.

Labda wanachoweza kwa sasa ni kusafirisha vifurushi tu ila biashara ya kusafirisha watu imeshawashinda.

Hao ikiwezekana wafungiwe tu moja kwa moja waanze upya
Na ninyi bado mpaka leo hamyajui ma bus mazuri aisee na kila siku yanaonekana Road wacha wawapandishe kwenye Punda mshazoea kukariri..
 
MAMLAKA ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), imeyasimamisha magari yote ya Kampuni ya Kilimanjaro Express kutoa huduma ya usafirishaji kuanzia jumatatu kutokana na kukiuka masharti ya leseni ikiwamo kutotoa tiketi ya kielektroniki na kuzidisha nauli kwa abiria.

Agizo hilo limetolewa leo na Mkurugenzi Mkuu wa LATRA, Habibu Suluo baada ya kufanya ukaguzi wa kushtukiza katika stendi ya mabasi ya Magufuli pamoja na ofisi za mabasi ya kampuni hiyo ya Kilimanjaro Shekilango Dar es Salaam.

Akizungumza baada ya kufanya ukaguzi huo, Suluo amesema mabasi hayo pekee ndio bado yanatoa tiketi zisizo za kielektroniki na kwamba yamebainika kukiuka masharti mengi ya leseni licha ya kuonywa mara kwa mara na kutozwa faini.

"Na leo tumelikamata gari jingine la kampuni hii ya Kilimanjaro inayofanya safari zake Dar es Salaam kwenda Moshi na Arusha likiwa limezidisha nauli kwa abiria, kila abiria alilipishwa nauli tofauti, tukawataka wawarejeshee nauli zao, wakakubali, lakini muda mfupi tumetoka kwenye ofisi zao wakakataa tena kurejesha eti mpaka bosi wao aseme,"amesema Suluo.

"Na hii siyo mara moja, wamekuwa wakifanya hivi mara nyingi na tumewaonya mara kwa mara na anaona kulipa faini ni kawaida kwake. Sasa sisi lengo letu ni kutaka wafuate sheria na masharti ya leseni, watoe huduma bora na siyo kutoa faini. Na kama anaona kulipa faini ni kawaida kwake sisi hatuwezi kuvumilia, tumetoa maagizo asitoe huduma kuanzia jumatatu mpaka atakapofanya maboresho na kufuata masharti ya leseni yake."

Mnamwonea tu, ushindani tu wa biashara
 
Back
Top Bottom