Hapa umechanganya mambo.
Umeandika points na uzushi.
Nadhani huna exposure kwenye nchi za ulaya na Amerika.
Ngoja nikupe ufahamu kidogo, maana nina exposure katika kuzitumia hizo treni/mabasi ya mjini ya umeme (tram)
Kwanza hizi tram zinakwenda mwendo wa kawaida au taratibu, kasi ya juu kabisa unaweza kukuta ni 30km/hour. Hazina tofauti yoyote na daladala katika kufanya kazi zake, tofauti ni kuwa zimetengenezewa miundo mbinu yake ya reli (kwenye ardhi) na nyaya (angani).
Wenzetu huko ulaya na marekani walibuni hizo vitu na kuziweka mjini ili kupunguza msongamano wa magari, kupunguza uchafuzi wa mazingira kutokana na hewa ya ukaa, kelele na gharama.
Tatizo kubwa katika hapa Tanzania ni hili..
1. Umeme usiokuwa na uhakika.
2. Miji isiyokubali kupangika.
3. Vurumai za shughuli za mijini.
Note:
Wakati Chuo cha UDOM kinajengwa kilitakiwa kuwa na miundo mbinu ya treni za kuweza kuzunguka kwenye campus zake zote, na michoro ilionyesha hivyo (na pesa huenda ilitolewa lakini wajanja wakapiga na wajinga tukaa kimya), hapo ndipo pangekuwa sehemu rahisi na bora ya kuanzia kuweka hii miundo mbinu ya tram.