KERO Mabasi ya Mwendokasi: Hili suala la mimi nakudai chenji wewe unanipa vocha ya VODA, kuna nini hapa?

KERO Mabasi ya Mwendokasi: Hili suala la mimi nakudai chenji wewe unanipa vocha ya VODA, kuna nini hapa?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

barafuyamoto

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2014
Posts
32,378
Reaction score
29,739
Habari zenu.
Kwa kweli nimeshangazwa sana ktk mabasi yaendayo haraka.
Inakuwaje nakupa pesa yangu ya kutaka kupata tiketi, mfano nakupa 1000Tshs, unatakiwa unirudishie 350Tshs sababu nauli ni 650Tshs, sasa unanipa "CHENJI" shilingi 300 na vocha ya VODA ya 50?
Nimeona wengine wanarudishiwa "CHENJI" ya vocha za voda 100 na 200 bila wao kukubali. Yaani hizo vocha zimegeuka pesa halali kwa kurudishiwa chenji.

Mimi kama situmii mtandao wa voda kwa nini mnanilazimisha nichukue hiyo vocha?? Cha ajabu nikiichukua na kesho kuja hapo hapo kituoni na shilingi 600 na hiyo vocha mliyonipa ya 50, HAMTAKI!!
HUU NI UPUUZI WA HALI YA JUU, sijajua ni kitu kipo ktk majaribio au ni mradi wa mtu kulazimisha vocha zake zinunuliwe, na kwa nini voda tu?

TUSIHARIBIANE BAJETI KWA KULAZIMISHANA KUNUNUA VOCHA ZA VODA.

Leo tarehe 13.03.2018, nimepanda kituo fulani na pia kushuka kituo fulani. Nimewauliza makeshia kulikoni leo hajanipa chenji ya vocha, kasema ZIMEZUILIWA KUUZWA NA UONGOZI WAO MPAKA FURTHER NOTICE
.
 
Ngoja siku wanifanyie mimi ivyo niwawashie moto wa mtema kuni
Juzi baada ya kubishana na keshia kituo fulani nikaichukia vocha ya 50, jana narudi nayo na kuambatanisha na 600 na namkuta yeye mwenyewe aliyenipa juzi na akanikumbuka fresh, ananiambia hawezi nipa tiketi mpaka nimpe 650, akisema wameambiwa wasizipokee ila watoe tu.
 
Kumbe na wewe unayemsifia bwana yule unakumbana na haya mambo.

Pole, nunua line ya voda ili mambo yawe sawa ukipewa hiyo vocha.

Hii mbinu ya kutuchuna kiaina sana walioianzisha.
Mtu hauna voda, wao wanalazimisha na hata kama nina voda, haikuwa ktk mipango yangu kununua vocha ya 50,100 au 200 kwao.
 
AISEEEE MBONA MAAJABU HAYO ..CJATUMIA HUO USAFIRI KATIKA SAFARI ZANGU YAPATA MWEZI SASA ...SIKUTEGEMEA KUSIKIA WALA KUONA JAMBO LAKIPUUZI KAMA HILO...
YAANI PESA YANGU MWENYEWE KISHA INAAMULIWA MATUMIZI NA KIKUNDI CHA WATU .,...sasa kama situmii huo mtandao napewa hiyo line iliiweje ..naweza nikawa na utumia huo mtandao pia ..lakini nikawa sina uhitaji wa hiyo voucher ...kwa ujinga ambao tunao watanzania naimani kuna ambao watakuw hawajali kuhusu hilo kwa mantik yakudharau hicho kiasi cha tsh50 ..lakini laiti wangejua baada ya hizo Pesa kukusanywa kwa ujumla wawatu wote naimani wange jiona kuwa ni majuha..
 
Habari zenu.
Kwa kweli nimeshangazwa sana ktk mabasi yaendayo haraka.
Inakuwaje nakupa pesa yangu ya kutaka kupata tiketi, mfano nakupa 1000Tshs, unatakiwa unirudishie 350Tshs sababu nauli ni 650Tshs, sasa unanipa "CHENJI" shilingi 300 na vocha ya VODA ya 50?
Nimeona wengine wanarudishiwa "CHENJI" ya vocha za voda 100 na 200 bila wao kukubali. Yaani hizo vocha zimegeuka pesa halali kwa kurudishiwa chenji.

Mimi kama situmii mtandao wa voda kwa nini mnanilazimisha nichukue hiyo vocha?? Cha ajabu nikiichukua na kesho kuja hapo hapo kituoni na shilingi 600 na hiyo vocha mliyonipa ya 50, HAMTAKI!!
HUU NI UPUUZI WA HALI YA JUU, sijajua ni kitu kipo ktk majaribio au ni mradi wa mtu kulazimisha vocha zake zinunuliwe, na kwa nini voda tu?

TUSIHARIBIANE BAJETI KWA KULAZIMISHANA KUNUNUA VOCHA ZA VODA.
Kwanini usitumie mtandao huo, vipende viwanda vya nyumbani, kama hutumii kampe mkeo au mmeo, watanzania tunao ndugu vijijini wanazihitaji hizo vocha, kawape.
 
Kuna vocha za sh 50?
Yeah, mwendo kasi vituoni wanazo. 50, 100 ma 200.
Yaani zile hamsini hamsini tulizokuwa tunalalamika tunaziacha sababu "hawana" chenji sasa wanatupatia vocha ya 50 tena wametuchagulia na mtandao wa voda tu.
 
Kwanini usitumie mitandao huo, vipende viwanda vya nyumbani, kama hutumii kampe mkeo au mmeo, watanzania tunao ndugu vijijini wanazihitaji hizo vocha, kawape.
Kwa nini tulazimishane? Mwisho wa siku naona ni mradi tu wa mtu huu.
 
Sasa wewe Kama hautaki vocha ya Tsh.50 c uwe unaenda na pesa kamili. kwani tatizo liko wapi mkuu
Ishu sio kutaka au kutotaka.
Wewe unaona hili liko sawa?? Voda pekee, mitandao mingine vipi??
Na kama nikiichukia nisiitumie, wao wataipokea kama shilimgi 50 nikienda na shilingi 600 na hiyo vocha ya 50 waliyonipa??
Jibu ni hapana maana nimejaribu wakakataa.
 
Back
Top Bottom