Habari zenu.
Kwa kweli nimeshangazwa sana ktk mabasi yaendayo haraka.
Inakuwaje nakupa pesa yangu ya kutaka kupata tiketi, mfano nakupa 1000Tshs, unatakiwa unirudishie 350Tshs sababu nauli ni 650Tshs, sasa unanipa "CHENJI" shilingi 300 na vocha ya VODA ya 50?
Nimeona wengine wanarudishiwa "CHENJI" ya vocha za voda 100 na 200 bila wao kukubali. Yaani hizo vocha zimegeuka pesa halali kwa kurudishiwa chenji.
Mimi kama situmii mtandao wa voda kwa nini mnanilazimisha nichukue hiyo vocha?? Cha ajabu nikiichukua na kesho kuja hapo hapo kituoni na shilingi 600 na hiyo vocha mliyonipa ya 50, HAMTAKI!!
HUU NI UPUUZI WA HALI YA JUU, sijajua ni kitu kipo ktk majaribio au ni mradi wa mtu kulazimisha vocha zake zinunuliwe, na kwa nini voda tu?
TUSIHARIBIANE BAJETI KWA KULAZIMISHANA KUNUNUA VOCHA ZA VODA.