KERO Mabasi ya Mwendokasi: Hili suala la mimi nakudai chenji wewe unanipa vocha ya VODA, kuna nini hapa?

KERO Mabasi ya Mwendokasi: Hili suala la mimi nakudai chenji wewe unanipa vocha ya VODA, kuna nini hapa?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Kama wameamua kuturudisha kwene barter trade basi nao wakubali kuzipokea hizo vocha pale mtu anapokua na 600 na vocha ya 50, waache ushenzi chenji zinauzwa wakanunue pumbavu zao
 
Sasa vocha ya 50 nifanyie nn kwani kuna kifurushi cha sh 50...hiii nchi bana [emoji17] [emoji17]
 
Habari zenu.
Kwa kweli nimeshangazwa sana ktk mabasi yaendayo haraka.
Inakuwaje nakupa pesa yangu ya kutaka kupata tiketi, mfano nakupa 1000Tshs, unatakiwa unirudishie 350Tshs sababu nauli ni 650Tshs, sasa unanipa "CHENJI" shilingi 300 na vocha ya VODA ya 50?
Nimeona wengine wanarudishiwa "CHENJI" ya vocha za voda 100 na 200 bila wao kukubali. Yaani hizo vocha zimegeuka pesa halali kwa kurudishiwa chenji.

Mimi kama situmii mtandao wa voda kwa nini mnanilazimisha nichukue hiyo vocha?? Cha ajabu nikiichukua na kesho kuja hapo hapo kituoni na shilingi 600 na hiyo vocha mliyonipa ya 50, HAMTAKI!!
HUU NI UPUUZI WA HALI YA JUU, sijajua ni kitu kipo ktk majaribio au ni mradi wa mtu kulazimisha vocha zake zinunuliwe, na kwa nini voda tu?

TUSIHARIBIANE BAJETI KWA KULAZIMISHANA KUNUNUA VOCHA ZA VODA.
Hizo ndiyo akili za watendaji wa serikali ya CCM.

Endelea kukata viuno kusherehekea chama kimeshika hatamu.
 
Mpka lina
Poleni mnaotumiaa mwendokasi bt fikisheni hili swala sehemu husikaa kwa msaaada zaidi
Ujue mpaka linafanyika limeanzia sehemu husika.hapo hakuna msaada zaidi ya kuzigomea hizo vocha
 
Juzi baada ya kubishana na keshia kituo fulani nikaichukia vocha ya 50, jana narudi nayo na kuambatanisha na 600 na namkuta yeye mwenyewe aliyenipa juzi na akanikumbuka fresh, ananiambia hawezi nipa tiketi mpaka nimpe 650, akisema wameambiwa wasizipokee ila watoe tu.
Ningemtoa miguu walahi
 
Hizo ndiyo akili za watendaji wa serikali ya CCM.

Endelea kukata viuno kusherehekea chama kimeshika hatamu.
Jicho lako halioni mbele ya mipaka ya vyama vya siasa, umelaaniwa mpaka Yesu arudi ndio utaponywa.

Chama kimeshika hatamu na hatamu imeshikwa ma chama.

26.04.2018 IS A NATIONAL KEYBOARDS DAY, usisahau! Tell your friends to go tell their friends down the line.
 
Kama vile yule nesi alivokamatwa anauza nguo hospitali basi naomba na hawa makonda akawakamate wanafanya biashara ya vocha mahala pa kazi...

Hapo kuna faida wanapata kwa sababu hizo vocha hawazichukui kwa bei kamili huko Voda.
Huenda hiyo ya 50 ikawa 45, ya 100 kwa 90 na 200 kwa 180 hivo kuna faida kubwa watakuwa wanapata..
 
Wonders shall never ends. .
Yani jamaa wame amua kuwawekea vocha ya 50?? Ndio mbadala wa chenji! !!!
[emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji38]
 
Back
Top Bottom