barafuyamoto
JF-Expert Member
- Jul 26, 2014
- 32,404
- 29,811
Ndio, inanitoa povu.Vyuma vimekaza mda sio mrefu wote tutaimba wimbo mmoja kwa sauti kuubwa...yaani hadi wewe sh 50inakutoa povu?
Juzi baada ya kubishana na keshia kituo fulani nikaichukia vocha ya 50, jana narudi nayo na kuambatanisha na 600 na namkuta yeye mwenyewe aliyenipa juzi na akanikumbuka fresh, ananiambia hawezi nipa tiketi mpaka nimpe 650, akisema wameambiwa wasizipokee ila watoe tu.Ngoja siku wanifanyie mimi ivyo niwawashie moto wa mtema kuni
Mtu hauna voda, wao wanalazimisha na hata kama nina voda, haikuwa ktk mipango yangu kununua vocha ya 50,100 au 200 kwao.Kumbe na wewe unayemsifia bwana yule unakumbana na haya mambo.
Pole, nunua line ya voda ili mambo yawe sawa ukipewa hiyo vocha.
Hii mbinu ya kutuchuna kiaina sana walioianzisha.
Hilo suala sikubaliani nalo.Mtu hauna voda, wao wanalazimisha na hata kama nina voda, haikuwa ktk mipango yangu kununua vocha ya 50,100 au 200 kwao.
Nasubiri jibu na mimi.Kuna vocha za sh 50?
shangaa ya Firauni MKUU BAADA YA KUYAONA YA MUSAKuna vocha za sh 50?
Kwanini usitumie mtandao huo, vipende viwanda vya nyumbani, kama hutumii kampe mkeo au mmeo, watanzania tunao ndugu vijijini wanazihitaji hizo vocha, kawape.Habari zenu.
Kwa kweli nimeshangazwa sana ktk mabasi yaendayo haraka.
Inakuwaje nakupa pesa yangu ya kutaka kupata tiketi, mfano nakupa 1000Tshs, unatakiwa unirudishie 350Tshs sababu nauli ni 650Tshs, sasa unanipa "CHENJI" shilingi 300 na vocha ya VODA ya 50?
Nimeona wengine wanarudishiwa "CHENJI" ya vocha za voda 100 na 200 bila wao kukubali. Yaani hizo vocha zimegeuka pesa halali kwa kurudishiwa chenji.
Mimi kama situmii mtandao wa voda kwa nini mnanilazimisha nichukue hiyo vocha?? Cha ajabu nikiichukua na kesho kuja hapo hapo kituoni na shilingi 600 na hiyo vocha mliyonipa ya 50, HAMTAKI!!
HUU NI UPUUZI WA HALI YA JUU, sijajua ni kitu kipo ktk majaribio au ni mradi wa mtu kulazimisha vocha zake zinunuliwe, na kwa nini voda tu?
TUSIHARIBIANE BAJETI KWA KULAZIMISHANA KUNUNUA VOCHA ZA VODA.
Yeah, mwendo kasi vituoni wanazo. 50, 100 ma 200.Kuna vocha za sh 50?
Kwa nini tulazimishane? Mwisho wa siku naona ni mradi tu wa mtu huu.Kwanini usitumie mitandao huo, vipende viwanda vya nyumbani, kama hutumii kampe mkeo au mmeo, watanzania tunao ndugu vijijini wanazihitaji hizo vocha, kawape.
Ishu sio kutaka au kutotaka.Sasa wewe Kama hautaki vocha ya Tsh.50 c uwe unaenda na pesa kamili. kwani tatizo liko wapi mkuu