KERO Mabasi ya Mwendokasi: Hili suala la mimi nakudai chenji wewe unanipa vocha ya VODA, kuna nini hapa?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Huo ni wizi wa wazi wazi kumlazimisha mtu achukue vocha badala ya pesa. Vocha ya 50 mtu itamsaidia nini. Hiyo 50 kwenye 450 unaweza ongezea ukapata 500 ukanunua fungu la nyanya. Sasa vocha ya 50 kwa mtandao usiotumia itakusaidia nino
 
Nenda kamwambie mwenyekiti wenu
 
Kwanini usitumie mtandao huo, vipende viwanda vya nyumbani, kama hutumii kampe mkeo au mmeo, watanzania tunao ndugu vijijini wanazihitaji hizo vocha, kawape.
Aliyekuambia voda ni kampuni ya Tanzania nani? Kupenda ndo ulazimishwe??
 
Mwendo kasi za huku Mwanza hazifanyi hiyo kitu. Unatoa pesa konda anakupa chako
 
Sasa wewe Kama hautaki vocha ya Tsh.50 c uwe unaenda na pesa kamili. kwani tatizo liko wapi mkuu
Upo shamba wewe ungekua unakaa dar usingeropoka hivo...
Wewe unafanya biashra halafu unasema wateja waje na chenji badala ya wewe kutafuta chenji??

Mi jukumu langu ni kulipia huduma uliyonipa na sio kutafuta chenji pumbavuu
 
Yeah, mwendo kasi vituoni wanazo. 50, 100 ma 200.
Yaani zile hamsini hamsini tulizokuwa tunalalamika tunaziacha sababu "hawana" chenji sasa wanatupatia vocha ya 50 tena wametuchagulia na mtandao wa voda tu.
Mwenye picha ya hyo vocha tuione. Maana vocha ya 50 hakuna.
 
50 ukiweka kwenye simu, kabla hujanunua kifurushi, is haliwi.
Sa ivi vifurushi tuna una kwa kutumia tigo pesa, M-Pesa au Airtel money.
 

Kituo gani hapo ulikumbana na hizo vocha mkuu?
 
Mwenye picha ya hyo vocha tuione. Maana vocha ya 50 hakuna.
Kijana, baki kijijini, usije mjini!
Nimesema vocha za 50, 100 na 200 zinapatikana ktk vituo vya mwendo kasi tu, huzipati ktk maduka ya vocha na sio kwamba wanauza, ni 'chenji' mbadala ya 50, 100 na 200.
 
Kijana, baki kijijini, usije mjini!
Nimesema vocha za 50, 100 na 200 zinapatikana ktk vituo vya mwendo kasi tu, huzipati ktk maduka ya vocha na sio kwamba wanauza, ni 'chenji' mbadala ya 50, 100 na 200.
Basi usiwaongopee watu kama huna hyo picha. iweke hapa kama ushahidi.
 
Hiyo ni ushahidi tosha pesa yetu imeporomoka na uchumi unayumba maana sh 5O inapotea taratibu kwenye mzunguko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…