Mabasi ya utalii yatua Dar, mabilioni ya fedha yatengwa

Mabasi ya utalii yatua Dar, mabilioni ya fedha yatengwa

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
5,227
Reaction score
5,299
Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam imepitisha Sh75 bilioni za bajeti kwa mwaka 2018/2019 huku kipaumbele kikiwekwa kwenye utalii.

pic+bajeti.gif

Kati ya fedha hizo, Sh65 bilioni ni za maendeleo ambazo zitahusisha miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa kituo cha mabasi Mbezi Louis, madarasa na vibanda vidogo vya biashara eneo la Gongo la Mboto.

Ndani ya bajeti hiyo zimetengwa fedha kwa ajili ya kununua mabasi makubwa ya kitalii ambayo yatakuwa yakizunguka katika viunga mbalimbali vya Jiji la Dar es Salaam kuwazungusha watalii.

Meya wa jiji hilo, Isaya Mwita alisema tayari mabasi mawili yameshawasili na yanasubiriwa mengine ili biashara ya utalii ndani ya jiji ianze mapema iwezekanavyo.

“Nadhani madiwani kwa pamoja tumeona imefika wakati kuweka nguvu kubwa kwenye utalii katika jiji letu kama ilivyo katika miji mingine mikubwa barani Afrika mfano majirani zetu Mombasa na Lamu,” alisema.

Mjumbe wa baraza la madiwani la halmashauri hiyo na mbunge wa Temeke, Abdallah Mtolea alisema ni hatua kubwa kwa jiji na ilipaswa kuwa hivyo muda mrefu.

“Ukitembea katika nchi mbalimbali wenzetu wamezingatia mno suala la utalii wa ndani ya mji, naweza kusema tumechelewa ilitakiwa tufike huko muda mrefu ndiyo sababu suala hili lilipokuja kwetu tumeliridhia,” alisema.

Chanzo: Mwananchi
 
Hii imekaa vizuri sana.

Ikiwezekana fanyeni mpaka mikoa ya pembezoni. Mfano mnakuwa na mabasi kama manne kwenda kwenye mbuga na sehemu nyingine zenye vifutio mtapataje Wateja ni kujitangaza tu. Watu hawana sehemu za kwenda kubadilisha akili kwani safari kama hizi humfanya mtu kuwa na mtazamo mpya.
 
Nadhani wamefikiria mbali sana, watanzania hawana pesa na wanazidi kufulia hivyo kodi za kawaida za jiji lazima zitakuwa zinashuka. Kwa hiyo watalii ni source nzuri sana ya mapato ambayo haitegemei waliokazwa na vyuma hasa ukizingatia potential ya utalii ya Dar es salaam ni kubwa sana na bado haijafunguiwa ipasavyo.

Ila wajihadhari na Bwanayule na Mwanaye mpendwa maana mabwana wale kwa kudandia treni kwa mbele hawajambo, kila kukicha wanawaza namna gani wapore mapato ya halmashauri za miji/majiji.
 
Hao watalii watazungushwa wapi katika jiji letu pendwa?

Amandla...
Manzese , tandale , Tandika, mburahati, mbagala, Keko maana huko ndio maeneo yanayoweza kukupa picha halisi ya Mtanzania na nchi yake inayotajwa kama moja ya nchi fukara duniani.
 
Wazo zuri tatizo foleni
Hii plani ni mpya kwa hiyo ni wao kuajuri watu markeng kwani kuna makampuni mengi wafanyakazi wanahitaji mitoko kama hii .Ila wajikite ktk zile sehemu za vivutio ktk nchi nzima.
 
Hii imekaa vizuri sana.
Ikiwezekana fanyeni mpaka mikoa ya pembezoni. Mfano mnakuwa na mabasi kama manne kwenda kwenye mbuga na sehemu nyingine zenye vifutio mtapataje Wateja ni kujitangaza tuu. Watu hawana sehemu za kwenda kubadilisha akili kwani safari kama hizi humfanya mtu kuwa na mtazamo mpya

Siungi mkono.

Wajenge vituo vya afya kwanza

Waimatishe elimu na miundo mbinu yake

Wajenge masoko makubwa na ya kisasa.

Wajenge vituo vya michezo ikiwezekana kila kata kama kile cha jk na pia vya sanaa ili kukuza vipaji vya ngoma na mziki.
nk
 
Aisee maajabu haya; utalii wa manzese! Hilo wazo linaakisi kabisa sera za Chadema.
 
Manzese, tandale, Tandika, mburahati, mbagala, Keko maana huko ndio maeneo yanayoweza kukupa picha halisi ya Mtanzania na nchi yake inayotajwa kama moja ya nchi fukara duniani.
Bila kwamtogole utalii utakuwa haujafanyika
 
Na haya maandamano siyatakuja vunjwa vioo bure, nani atakuja kutalii jiji linalokimbizana na FFU kila siku.
 
Hahaaa utalii wa mabsi Dar!! joto, foleni, mji unanuka nk. wangeboresha tu safari za mbudya na bongoyo au wangeboresha na kusafisha coco beach iwe kama Copacabana.
 
tunahitaji machinjio ya kisasa, maeneo kama jangwani yalitakiwa kuboreshwa, masoko ya kisasa na uboreshaji wa miundo mbinu
 
Hahaha mabasi ya habiria nyie mnaita ya watalii, Darisalama watalii wanapita tu, watatalii wapi?! Bora mgenunua helikopta?!
 
Back
Top Bottom