The Stig
JF-Expert Member
- Apr 11, 2011
- 1,113
- 1,105
Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam imepitisha Sh75 bilioni za bajeti kwa mwaka 2018/2019 huku kipaumbele kikiwekwa kwenye utalii.
View attachment 701231
Kati ya fedha hizo, Sh65 bilioni ni za maendeleo ambazo zitahusisha miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa kituo cha mabasi Mbezi Louis, madarasa na vibanda vidogo vya biashara eneo la Gongo la Mboto.
Ndani ya bajeti hiyo zimetengwa fedha kwa ajili ya kununua mabasi makubwa ya kitalii ambayo yatakuwa yakizunguka katika viunga mbalimbali vya Jiji la Dar es Salaam kuwazungusha watalii.
Meya wa jiji hilo, Isaya Mwita alisema tayari mabasi mawili yameshawasili na yanasubiriwa mengine ili biashara ya utalii ndani ya jiji ianze mapema iwezekanavyo.
“Nadhani madiwani kwa pamoja tumeona imefika wakati kuweka nguvu kubwa kwenye utalii katika jiji letu kama ilivyo katika miji mingine mikubwa barani Afrika mfano majirani zetu Mombasa na Lamu,” alisema.
Mjumbe wa baraza la madiwani la halmashauri hiyo na mbunge wa Temeke, Abdallah Mtolea alisema ni hatua kubwa kwa jiji na ilipaswa kuwa hivyo muda mrefu.
“Ukitembea katika nchi mbalimbali wenzetu wamezingatia mno suala la utalii wa ndani ya mji, naweza kusema tumechelewa ilitakiwa tufike huko muda mrefu ndiyo sababu suala hili lilipokuja kwetu tumeliridhia,” alisema.
Chanzo: Mwananchi
Huo mradi wa mabasi ya utalii ni biahsara kichaa na hayo mabasi yatakufa baada ya muda mfupi.
Tatizo la utalii kuwa mdogo Dar siyo kukosekana kwa mabasi, bali kukosekana kwa product ya utalii per se. Kama ingekuwepo hiuo product, usingekuta yale ma coster mazuri yanapaki bure pale biafra yakisubiri kupeleka misiba moshi.
Hauwezi uka force eti kitu kiwe cha kitalii kwa sababu tu umekula maharage sijui ya wapi. Halafu ukaleta miundo mbinu ya kulazimisha watu waende huko. Hii supply side strategy is bound to fail miserably.