Mabasi yote yaende Stendi ya Magufuli, kama huwezi ondoka Dar Es Salaam hupawezi

Wewe ni mpuuzii... Magari haya luxury bus yalikua yana simama mfano magufuri stendi then shekilango stand.

Simple logic bus haliwezi simama Kila kituo kama daladala

Wewe ni wakupuuzwa kabisa
Kaka kwa usalama wa nchi watu wote wanapaswa kuteremkia Magufuli bus stand kwa ukaguzi wa nyaraka badala ya watu kuanza kushukia Bunju, Boko, Kibo, njia 4, kimara mwisho, Shekilango,nk. Hata hawa mungiki waliofanya vurugu oct29 inasemekana walikuja na mabasi hayahaya na kushukia njiani kabla ya kufika stendi ya magufuli.

Lazima pale stendi ya Magufuli kuwe na ofisi na maofisa wa uhamiaji, na scanners za utambuzi.

Kwa usalama wa jiji na nchi watu wote lazima washushiwe Stendi kuu kama vile wanavyoshuka watu Airport na Bandarini na SGR.
 
Jiji linapaswa kuwa sehemu ghali sana kuishi, haiwezekani katikati ya jiji ukute fungu la mihogo la sh 500. Huo ni uholela unaovutia vijana wengi wanaomaliza darasa la saba vijijini kuja kwenye majiji makuu ya nchi.
 
Jiji linapaswa kuwa sehemu ghali sana kuishi, haiwezekani katikati ya jiji ukute fungu la mihogo la sh 500. Huo ni uholela unaovutia vijana wengi wanaomaliza darasa la saba vijijini kuja kwenye majiji makuu ya nchi.
Kwani mtu wa la saba akija mjini Kuna shida gani?

Pelekeni MAENDELEO huko huko vijijini ili wasije mjini..

Kwanini mtu aje mjini kuteseka kama angepata fursa kule kule kijijini kwake/ kwao
 
Kwani mtu wa la saba akija mjini Kuna shida gani?

Pelekeni MAENDELEO huko huko vijijini ili wasije mjini..

Kwanini mtu aje mjini kuteseka kama angepata fursa kule kule kijijini kwake/ kwao
Mtoto wa darasa la saba alipaswa kushindwa kuishi kwenye jiji kubwa kama dar. Alipaswa kushindwa hata kuwaza kuja DSM badala yake ama abaki kijijini kwao au aende makao makuu ya wilaya yake tu. Viongozi wetu wana shida kubwa sana. hawa machinga na wauza bidhaa kandokando ya barabara ni matokeo ya uholela wa viongozi wakidhani wanawasaidia vijana kumbe wanajitengenezea bomu wao wenyewe. Hawa ndio wale wanaoweza kupewa 30,000 wachome SGR yao, hawana cha kupoteza hapa jijini; yote sawa tu.

Ukienda kule Washington au NY mtu masikini atalala mtaloni au kwenye magari mabovu na lazima apewe coupon ya chakula la sivyo atakufa.
 
Uko sahihi, sijawahi ona jiji lolote duniani mabasi aka Coach yanajishushia tu abiria kila kituo. Stand ya basi ni moja na yote lazima yamalizie safari hapo. Hivi Chalamila alivyofanya ndio utaratibu unavyotakiwa, ukiona gharama hama jiji, halikufai.
 
Sahihi, na ndio demand yenyewe. Abiria akiona kushuka au kupakia kabla ya kufika stand ni rahisi zaidi kuliko kufika stand hatofika hata ukilazimisha basi lifike. Lazima serikali itengeneze urahisi abiria aone bora afike stand then atengeneze logistic za kufika anapoelekea. Demand ya kushukia stand ikiwa kubwa wala hulazimishi mabasi, yatafata pesa.
 
Serikali inapunguza kodi za nyumba kwenye miji midogo kivipi? Kuna serikali ina nyumba ya kupangisha uko kisemvule? Hapo si unatupiga changa?
 
Mabasi yana vituo mkuu. Hichi unachosema ni mambo ya miaka mingi nyuma sio sasa. Treni za kasi zina vituo sembuse mabasi? Mfano China Beijing Shanghai line vituo ni karibu kila 60 km.
Wuhan–Guangzhou line vituo katibu kila 80km.

La kufanya ni kututengeneze sababu za kwanini abiria atake kuifuata stand. Tikitengeneza demand wala hutalazimisha.
 
Kwa ushauri wako hata wale wa kibamba inabidi washukie mbezi ili wakaguliwe then wapate public transport back to kibamba
 
wakishukia mlandizi nani atawakagua? Au abiria wa Mlandizi nao wafike mpaka Magufuli terminal?
 
tatizo letu ni exposure ndogo na watu waliopewa nafasi ya kutoongoza hawana exposure na maarifa makubwa ya kutuongoza. Jiji ni chafu na kila sehemu kuna biashara. Utakuta kijana kawasha moto kwenye service road anakaanga ships na maganda ya viazi anasukumiza kwenye njia ya majitaka na kila mtu anapita, anamuona na kumuacha anafanya vile. Barabara inayeyuka kwa moto wa jiko lake na mitaro inaziba kwasababu yake. na hapo anapochomea chips kuna balozi, viongozi wa serikali ya mtaa, kata na hata mkuu wa wilaya anapita hapohapo kila siku, na pengine hata chips za wafanyakazi wa ofisi yake zinatoka hapohapo. Shida ni kubwa mno.
 
Kitafutwe kituo cha daladala za njia zote palepale nje tu kidogo ya stendi ya magufuli ambako hata mgonjwa anaweza kwenda kupanda daladala yake kwenda anakoelekea. hata pale Airport kuna kituo cha mwendokasi kwa asiyeweza kuchukua Taxi. Hata hivyo majiji yote ni sehemu ghali kwa wakazi wake. Sisi hapa Dar hata sh.100 unaweza kupata pande kubwa la mhogo wa kukaanga ukanywa maji ya kandoro ya 100 ukashinda siku nzima bila wasiwasi. Jiji la namna hii hailiishi changamoto ya msongamano na uchafu.
 
Kitafutwe kituo cha daladala za njia zote palepale nje tu kidogo ya stendi ya magufuli ambako hata mgonjwa anaweza kwenda kupanda daladala yake kwenda anakoelekea. hata pale Airport kuna kituo cha mwendokasi kwa asiyeweza kuchukua Taxi.
Kabisa mkuu. It means mtu ataona kwanini nishukie njiani wakati stand napata usafiri wa kwenda ninapoelekea? Akiwa na mizigo ndo kabisa anajua atapata na wa kumbebea. Tayari ushatengeneza demand. Kupakia hivyo hivyo.
 
wakishukia mlandizi nani atawakagua? Au abiria wa Mlandizi nao wafike mpaka Magufuli terminal?
Vituo vya kupakia na kushusha abiria njia nzima lazima vifahamike na viratibiwe vyote ili kila anaepanda na kushuka afahamike kapandia wapi na kashukia wapi na amepanda na nini na ameshuka na nini. Mfano, mimi nafahamu kuwa mabasi ya mikoani ndiyo yanayokuja mijini na magunia ya bhangi, watu wenye madini, watu wenye pembe za ndovu, nk lakini wanashukia njiani kisha wanaingia mjini kwa bodaboda, gari ndogo kwenda kwenye stoo zao na masoko yaliko.
 
Acha kuchanganya madesa, Train na mabasi. Mabasi uwa yana kituo kimoja kikuu kwa mabasi yote ya mikoani, nimeishi majiji mengi duniani ndio hivyo na hata uwe unaishi sehemu ya mbali na hicho kituo kikuuu lazima ukifate ili upate usafiri unapotaka kwenda kwa kidhungu wanaita "Central Station" unakuta mabasi yote ya mikoani yamepaki hapo. Train hio ni habari nyingine haihusiani na mabasi tunaweza kuifungulia uzi wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…