Mabasi yote yaende Stendi ya Magufuli, kama huwezi ondoka Dar Es Salaam hupawezi

Mkuu utaratibu wa kuchukuwa abiria ni jukumu la wamiliki wa bus,.na sio abiria.
Mfano south Africa.
Ukiwa Pretoria unataka kwenda labda durban au cape town..
Mfano umekata bus la intercape au lolote,
Bus zinaanzia joberg to Durban,,ila ukiwa utapanda bus lingine local ukifika Park station Joberg unabadilshiwa gari lingine la Durban...

Iwe pia hapa dar,kwamba kuna min buses zinabeba abiria toka mitaani zinaleta Magufuli bus terminal,wanabadilisha bus wanaendelea na safari..
Tatizo lipo wp?
 
Wapiga debe sikuhizi wamejaa jf
Tatizo la jf ni baadhi ya watu kujifanya ujuwaji,sasa nipige debe kwa kipi?
Yaani tuache watu wachache wasiojuwa kwenda na wakati waharibu mji ?
Sio kila wanalopanga serikali basi ushupaze shingo na kupinga.
 
Unatoka safari umechoka basi linapita kituo chako pyuu mpaka magufuli
unaanzj tena safari ya kurudi nyuma ulipotoka..hapo bado folen road
unafika home umechoka mbaya!
Kushusha na kupakia iruhusiwe kwenye special bus terminals zile unapaki na kuondoka, ila basi kuingia stand ndo iwe lazima ili abiria anayetaka kufika stand asinyimwe haki yake.

Sasa nina basi langu nalinadi Lina VIP treatment nauli badala ya 50,000/= ni 100,000/= kwanini nisiruhusiwe kuwapa VIP care?
 
Ni sawa pia. Sio utaratibu mbaya kwenye upakiaji, ni mzuri. Wakati wa kushuka? Lakini mbona ni rahisi zaidi kuwa na terminal mbili au tatu kuliko hii? Jiji Lina watu M6+ kila mwaka wanaongezeka 100,000+ bado wanaokuja na kutoka uhalafu limetanuka haswa tunashindwa kuwa na small terminals nyingine 2 au tatu? Basi linapita tu, kushusha na kupakia ila stand kuu ni JPM.
 
Unatoka safari umechoka basi linapita kituo chako pyuu mpaka magufuli
unaanzj tena safari ya kurudi nyuma ulipotoka..hapo bado folen road
unafika home umechoka mbaya!
Mkuu bus linapita wp wakati unashuka unapotaka?
Hakuna hata sehem moja bus litampitisha abiria bila kusimama..
 
basi linalotoka mbeya, abiria anayekaa kibaha, unataka apelekwe mpk stendi ya magu halafu apande daladala impeleke kwake kibaha?
 
Huyu anaongea hivi mpaka Unashangaa hii jeuri anaipata wapi.
 
Wenye mabasi wabadilishe vibali na kuandika destination yao ni Mkuranga toka wanapotoka. Iwe Tanga- Mkuranga, Arusha- Mkuranga na kwingine. Yawe yanapita hapo Mbezi na abiria wengine kuelekea huko. Sababu destination si Dar hakuna ambaye atalazimisha washukie stendi fulani kwa pamoja. Likitoka Mkuranga linapita zake Shekilango na kuchukua abiria wengine wa kutokea Dar kwenda mikoa mingine
 
Unajua sababu ya mabasi yote yaanzie magu term na kuishia hapo hapo?
Sababu ni
  • kutoa kero za msongamano wa ofisi na mabasi mitaani..
  • stand imejengwa kwa ajili ya mabus na haitumiki..
-serikali kukosa mapato kwa sababu 99% ya bas zisizotumia Magufuli terminal,zinapita njia ya bagamoyo road na kukwepa kulipa pesa Magufuli terminal.
 
WM = Mabasi yaruhusiwe kuwa na ofisi zao nje ya stendi.

MWMDSM = Marufuku mabasi kushushia abiria nje ya kituo cha mabasi kikuu.

Je, MWMDSM > WM?
Kaka haya mabasi yanayolazimisha kuwa na vituo vyao binafsi mitaani baadhi yao kama sio mengi ya hayo wamebobea kwenye biashara za magendo/haramu. Mabasi haya yanatumika kusafirisha ama bidhaa haramu au watu haramu kwa taifa. Kwaajili ya usalama wa Taifa lazima wahakikishe kuwa abiria wanapandia na kushukia kwenye vituo maalumu vya mabasi vyenye miundombinu ya utambuzi na upekuzi wa watu na mizigo. Madawa ya kulevya, madini na nyara za serikali kama pembe za ndovu na faru zinasafirishwa kwa njia ya mabasi. Wahalifu wanapandia na kupakia kwenye vituo visivyo rasmi na kushukia na kuteremshia kwenye vituo visivyo na ulinzi wala utambuzi.
 
Hiyo sawa, hata hivyo Dar kuna kituo kimoja tu cha kupakia na kushushia ambacho ni Magufuli stendi tu baasi. Ukitoka hapo Magufuli hakuna kituo kingine tena Dar es salaam hadi Mkuranga.
 
Pale Tanga stendi kuu ya Kange wenye mabasi wanaleta abiria wao kutoka ofisi zao za katikati ya mji (Ngamiani) kwa mabasi madogo kwenda Stendi yaliko mabasi yao makubwa ya kwenda mikoa mingine. Hata hapa kuna ubaya gani mabasi madogo ya Mkuranga, Kisarawe, Mbande yasilete abiria Magufuli?
 
Hakika mkuu
 
Hiyo sawa, hata hivyo Dar kuna kituo kimoja tu cha kupakia na kushushia ambacho ni Magufuli stendi tu baasi. Ukitoka hapo Magufuli hakuna kituo kingine tena Dar es salaam hadi Mkuranga.
Hata ukiingia Dar kama unashuka kituo cha njiani kabla kufika stendi utashushwa tu. Hivyo sehemu zote ambaxo basi litapita kwenye vituo vya kushukia na kupandia daladala, abiria atashushwa tu
 
Hata ukiingia Dar kama unashuka kituo cha njiani kabla kufika stendi utashushwa tu. Hivyo sehemu zote ambaxo basi litapita kwenye vituo vya kushukia na kupandia daladala, abiria atashushwa tu
Vituo vya daladala ni vidogo kwa mabasi makubwa kusimama.
 
Wanachotakiwa jiji na Mkuu wa Mkoa ni kusogeza karibu huduma za daladala karibu zaidi na stendi ya magufuli kuliko kule viliko vituo vya daladala; kuna watu hawawezi kupanda lile daraja ili kuvuka ng'ambo ya barabara wakapande daladala.
Kwa Mujibu wako kama hawawezi kuvuka daraja lile wakae huko huko Mkoani, sio lazima waishi jijini
 
Shida sio Stand kuwa Magufuli,Shida Sio Gari kwenda Magufuli.

Shida ni Convenience.Private Bus Standa Ziwekewe Vigezo vya Msingi ili kuhakikisha Huduma zinakuwa bora na Pia Kuingia Stand ya Magufuli iwe ni Lazima.
Kuiacha Gari Magomeni Mwembe chai ili uifate ukaandie Mbezi Louis kwa sababu Tu serikali inataka hovyo, ni akili za ajabu Sana.
Watu watapanda Bus linapoanzia lakini litaita Stand kuchukua wengine walioko hao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…