Mabasi yote yaende Stendi ya Magufuli, kama huwezi ondoka Dar Es Salaam hupawezi

Wenye inchi na walipa kodi ndio wanaoamua na kutaka nini kiende. Kubishana na raia ni akili za kijima (communism) ambazo ni akili za kishamba kupita maelezo.

Machinga complex pale raia walipahoji na kupakataa ila wakaza fuvu wakasema NO,nini kimetokea, umeona lile eneo linatumika kwa makusudio yaliyopangwa?

Pale fire,kulijengwa karakana ya Mwendo kasi,raia wakasema haifai wakaza fuvu wakasema NO nini kimetokea? Umeona eneo linatumika kwa makusudio yaliyopangwa?🤔

Haya sasa na hii ubungo ni another project ambayo nadhani isipozingatia matakwa ya wenye inchi yao haitakwenda according to makusudio yake bali itaishia kuwa ni tatizo.
 
Ndio shida kuwapa cheo au wadhifa watu wasio na exposure. Unakuta mtu ni mshamba,akikaa Bar na washamba wengine wanashauriana ushamba wanauleta katika maisha ya watu wanaojua kuishi kituristi dem shiti.

Ni vema kukagua sana background za watu kabla ya kuwapa wadhifa, vyetu tu na elimu haitoshi. Mtu anaweza kuwa na ufaulu ila sehemu ya kwanza kuishi ni Dar. Mtu huyu anabishana na watu ambao Dar ni nyumbani kwa kuzaliwa na wametembea hadi huko mbeleni mataifa ya majirani.

Exposure ina mata sana.
 
wewe itakuwa unaishi kwa shemeji yako au unalishwa na mshangazi
Jijini sio kwa kila mtu, ndio maana jiji ni chafu sana. Watu wanapika kwa kuni na vifuu vya nazi jijini. Katikati ya jiji mtu anafuga kuku na mbuzi wanaozurura mitaani. Jiji gani hilo duniani kama sio tz tu?
 
Kwa usalama wa abiria na nchi abiria lazima apandie kwenye kituo na kushukia kwenye kituo kilichoratibiwa. Huwezi kupakia kwenye private station yako kiholela. Hii ndio maana ya public transport; usafiri wa umma. Unalinda umma unaosafiri na usiosafiri kwenye bus hilo.
 
Sheria na taratibu sio lazima ziwe rafiki kwako.
 
Nchi inaweza kupata kiongozi mshamba basi mtapata shida sana wananchi wenye exposure.
 
Basi gani linashusha kila kituo kama daladala?

Mabasi yalikua na sehemu maalum za kushusha na kupakia.
Kusema mabasi yanasababisha foleni huo ni uongo.
 

Ni kweli bus terminal zinatakiwa zi operate kama airport, ili kusimamia ulizi na usalama wa abiria, kukuza utalii, Biashara, and safety logistics
 
Wakienda pale watamuenzi Magufuli Kwa sababu pale ndio alitoka spichi yake ya mwisho kabla ya kukata roho.
Inanikumbusha yule jamaa aliyekuwa ananiambia,
Nina mambo mengi ya kusema kuhusu yaliyomfika Magufuli baada ya kutoka pale Stendi ya Mbezi.
Yule jamaa ninemchukulia kama chizi kwa sababu what he says does not add up.
Magufuli alitoka Stendi ya Mbezi akaenda Chuo cha Polisi Kurasini ambapo aliongea lugha ya vitisho dhidi ya Makamanda wa Jeshi.
Hawa walikuwa Makamanda wa Jeshi la Polisi.
Sijui kama ilikuwa inahusisha pia Makamanda wa JWTZ.
Lakini akawaambia atarudi baada ya siku chache and he will arrest them all.
Lakini hakurudi tena kwa sababu alipata pressure na ugonjwa wa moyo ndio imetokea watu wanavumisha habari za uongo kwamba kuna mtu alimdhuru Magufuli.
 
Mfano, Mtu kakulia kijijini, maisha yake yote yeye na familia yake yalikuwa kujisaidia porini na kuchamba kwa kusota mchangani, ghafla unampa uongozi wa jiji/wizara/urais unadhani jiji/nchi itakuwa safi?. Exposure haina mbadala wake.

Maisha ya majiji hayapaswi kuwa ni kimbilio kwa vijana kutoka vijijini. majiji duniani kote huwa yanaogopwa kwa sheria kali na ughali wa maisha. Jijini hupaswi kupata chumba cha Tsh 20,000, kuuza genge na mapakacha ya maembe kwenye baiskeli. Majiji hayatakiwi kuwa sumaku (centrifuge) ya kukusanya vijana kutoka mashambani badala yake majiji yanapaswa kuwa mawimbi ya maji kupwa ya bahari yanayosukuma uchafu kutoka katikati ya bahari kwenda nchi kavu. Vijana na watu wachovu walipaswa kuhamia mashambani kwenye nafuu ya maisha.

Hebu nenda pale marekani ukaone misururu wa watu siku za weekends wanaoelekea mashambani (nje ya majiji) kununua bidhaa, kunywa na kustarehe kwakuwa bei za vitu huko ni nafuu tena sana. Na wengine wanaishi huko na kuja majijini kufanya kazi na kurudi.

Hapa kwetu kila abiria anataka apandie na kushukia karibu na kwake eti kumpunguzia gharama, sheet!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…