Mabeberu, Vibaraka wa Mabeberu, Wazalendo wa Hayati Magufuli, na Mradi wa Bandari ya Bagamoyo

Kwa kifupi, atapata kile kama ambacho TPA au TICTS anapata leo hii, lakini kwa kawaida Mchina huwa anaomba apate msamaha wa kodi ya mapato kwenye hizi pesa anazoingiza!
Hatari umeiona hapo, ambayo pengine TPA inawatia kiwewe?

Bandari ya Dar haitapata kitu? Mapato inayopata sasa yote yatakwenda kwa mchina?

Unaweza ukasema ni ushindani wa kibiashara, lakini hapo ni wazi bandari ya Dar haitaambulia kitu!

Itabidi ife tu!
 
Umesoma vema mada au umekurupuka Mkuu? Yote hayo yametajwa na mtoa mada na mwisho wa siku amekuonesha kwanini Bagamoyo na si huko kwingineko unakodhani kunafaa...
Muwe mnasoma kwanza neno kwa neno... uvivu wa kusoma ni ugonjwa mbaya zaidi ndio unaosababisha wengi kizuri wakiambiwa sicho huitika "ndiyoo..." na mauno juu... na kibovu wakaaminishwa ndicho wakashangilia tena!!! Hivi faida ya bandari ya Bagamoyo mnajisahaulisha mhusika si mchina pekee hamjui na Oman ilikuwa mwekezaji mwenza? Je baina ya hiyo bandari na kile kiwanja cha ndege kule.... kipi kina fursa ya kuwa faida katika ajira na mapato kwa Taifa?
Waswahili wanasema "mjamba kwa hasira huishia kujinyea" waganda nao wana msemo wao "...kichwa cha mjinga husumbua miguu..." wazaramo wao husema "...ukikiona cha nini wenzako wanajiuliza watakipata lini..." hizihizi akili ndio zilifanya ati lami ikipita Serengeti ekolojia itaharibika ilhali Mikumi na mbuga zingine lami imekatisha na wanyama hawajawahi kuhama!!!
 
Huwa hakuna ushindani baina ya bandari kubwa na bandari ndogo... kwa ubovu wa huduma za watendaji wetu lazima waingiwe kiwewe na woga juu ya ushindani...
Je Fastjet au Community Air kwanini ziliondolewa? Zingeiua ATC? Je kwanini kampuni binafsi za simu ni maarufu kuliko TTCL? Ukiona watu wanaogopa ushindani jua hawana ubunifu na wana harufu zote za kifisadifisadi...
 
Gobole, ni hivi:
Tukiweka pembeni kupenda au kutopenda mradi huo ujengwe na wachina..., maoni ya chige ni muhimu, angalao kutupanua mawazo zaidi juu ya mradi wenyewe.
Chige, kwa bahati nzuri ameshiriki katika utafiti unaohusisha mradi wenyewe, kwa hiyo anao upeo zaidi kuhusu mradi; hata kama maoni yake anayaegemeza upande mmoja.

Kama na wewe unazo taarifa za upande wa pili, itapendeza sana kukusoma hapa ili tulinganishe taarifa zenu.
Sasa unachofanya hapa ni kutaka kuziba mdomo kwa kumshambulia yeye binafsi bila ya wewe kuchangia chochote cha maana.
 
Chige story ndefu sana kwanini usiweke huo Mkataba hapa mezani km ulizunguka na huyo Mmarekani, halafu Tafsiri zako ndio nikashtuka huyo Rais Xi Ping anataka China ndio iwe dereva mbona umeruka hapo?
Tafsiri ya Google kwa sisi tusioelewa huyo Rais wa China anataka wawe vinara na watushike masikio wewe umeweka bandari mara reli na viwanja vya ndege
"China itahimiza kikamilifu ushirikiano wa kimataifa kupitia Mpango wa Ukanda na Barabara. Kwa kufanya hivyo, tunatarajia kufanikisha muunganisho wa sera, miundombinu, biashara, fedha na watu na kwa hivyo kujenga jukwaa jipya la ushirikiano wa kimataifa kuunda dereva mpya wa maendeleo ya pamoja. "
mwenye Mkattaba atuwekee tuusome na sisi

Kalamu1 Gobole

 
Ninakubaliana nawe kuhusu ushindani.

Ila sikubali kuhusu ubunifu, sio 'preserve' ya watu walioko skta binafsi pekee.

Serikali ikitaka watu wake wawe wabunifu na wafanye kazi ya kufanikisha mashirika, inaweza sana.

Viongozi serikalini ndio tatizo.
 
Imenibidi nirudi kwenye mchango wako huu ambao kwa haraka haraka unaonekana kuwa na ukweli, lakini unasahau pia kwamba sio swala tu la "ushindani".

Hata wewe utakuwa unajua kwamba mwenye raslimali na uwezo humnyongea mbali asiye na uwezo kwa kila njia hata zisizo halali anazoweza kuzitumia ili abaki bila ushindani. Hili sio jambo geni katika biashara.
 
Pamoja na kwamba hakuna muafaka wa pamoja ila uzi umerudisha kumbukumbu za JF ya kipindi nashawishika kujiunga
Mada za akina MALCOM LUMUMBA Eiyer lee van cliff MSEZA MKULU pamoja na wadau wengine kibao ambao wametususa siku hizi.

Huwa naiona Jf kama platform bora kabisa ya kupata madini ya wajuvi tofauti hata na kule twitter wanakojiita jamhuri.
Huku ndio kulitakiwa kuwa jamhui maana unapata vitu kwa kina zaidi.
 
Nimekwishajibu hili huko juu.
Bila shaka hata wewe unajuwa kwamba bomba halijengwi na lisafirishe mafuta bila malipo yoyote.

Kwa hiyo, kama wewe unajuwa ni kiasi gani kimekubaliwa kama tozo, kwa nini usikiweke hapa, badala ya kuendelea kuniuliza mimi!

Wewe sema, ni kiasi gani kilikubaliwa?
 
Hamna hatari yoyote!

Bandari ya Bagamoyo haitarajiwi kuwa competitor wa Bandari ya Dar es salaam coz' target areas zake hazifanywi na Bandari ya Dar es salaam!

Target ya kwanza ya Bandari ya Bagamoyo ni kuwa Transshipment Port. Target ya pili ni ku-serve Industrial City ambayo itajengwa sambamba na bandari as well as reli!

Kwa maana nyingine, pamoja na suala la transshipment, Mchina atakuwa analeta malighafi za kulisha viwanda, na atakuwa anatoka na malighafi au bidhaa zilizozalishwa na viwanda vitakavyojengwa kwenye SEZ!

But all in all, inabidi ufike wakati tukubali kwamba solution ya Bandari ya Dar es salaam sio kubaki peke yake bali kuongeza efficiency! Ni umaskini wetu na majirani zetu unaofanya tuwe na bandari moja tu!
 
Kama masharti ya mwekezaji ni magumu Hii bandari tuijenge wenyewe mdogomdogo kwa miaka 30. Tufanye kama tulivyoanza kujenga barabara za ndani enzi za Mkapa kwa pesa zetu za madafu mdogomdogo.

Kwa approach hii tunaweza kuwa na bandari yetu wenyewe after 30 au 40 years.

I believe kama kila mwaka serikali itatenga kiwango fulani cha pesa tunayoimudu na ujenzi ukawa unafanyika mdogomdogo kwa muda wa miaka 30, tutakuwa na umiliki wa bandari hiyo 100%.

Tena uzuri wa approach hii, Tukifika mwaka wa 15 wa ujenzi huenda hiyo bandari ikawa imeshaanza kutumika kwa baadhi ya mizigo na hivyo kupunguza gharama za ujenzi
 
Wewe ndiye uliyekuja na hiyo bei ya $16. Mimi sijui ndiyo maana ni meuliza kwa vile haimake sense.

Anyway, point hapa siyo kwamba ni mradi nzuri sana kuliko wa bandari. Bandari na industrial park Zina more long term benefits in terms of work creation na income kwa individuals na serikali kuliko Bomba la mafuta. Eneo la bandari ni dogo kuliko hilo la Bomba ambalo litakuwa hapo kwa probably more than a century.

Vile vile hilo Bomba linaweza kuwa target ya maadui wetu na wa Uganda especially extremists.
 
Gamba la n
Hii aproach Ni nzuri mkuu, ila Kila wazo la mradi Linakuwa na msingi wake au kusudi ambalo anakuwa nalo yule mwenye kulianzisha ,So tukitekeleza kinyume na kusudi hutuwezi kupata faida iliyokusudiwa, Hii inaaply kote hata Tanzania ya viwanda Bila kufikiri tunamzalishia nani (soko) haitawezekana, Pia kabla ya kujenga hii bandaei lazima tijiulize tunamjengea kwa ajili ya Nini, maana tayari tunazo bandari zingine nyingi tu,Kwenye huu mradi asilimia kubwa mchina ndo kulishikilia kwa sababu yeue ana uhakika wa asilimia kubwa kuitumia yeye meli zake bidhaa zake na baadhi ya viwanda vyake ,nafikiri anaweza kuweka vya assembly tu.So nachokiona tukiamua kutekeleza Bila kumshirikisha tunaweza kujenga ikose shughuli za kutosha
Pia tutachukua mrefu ,miaka thelathini dunia inabadilika Kila siku na fursa Ni mpya Kila siku.
 
Hoja yako ni ya msingi lakini kujenga bandari kwa ajili ya target ya mzigo wa nchi moja tu nayo ni useless, je uchumi wa nchi hiyo ukiyumba?, au je tukikorofishana nayo kwa sababu ya maslahi yetu ya geopolitics au usalama wa nchi ndo bandari imeishia hapo?

Sisi tupo katika strategic region, tunazilisha landlocked countries kibao, kwa hiyo it doesn't matter whether mchina anataka au hataki, hiyo bandari yetu kama ikiwa ba viwango tunavyokusudia, yaani ya kubeba mizigo mikubwamikubwa kwa ajili ya nchi zilizolandlocked haitokosa biashara maana hizo nchi hakuna mwaka zitasita kuhitaji mzigo.

Hoja ya kuwa tayari tuna bandari nyingi, ukweli ni kuwa bandari hizo ni ndogo sana kutosheleza kutia nanga mimeli mikubwa ya mzigo wa maana!, Kwa hiyo bandari kubwa zaidi inahitajika bila kujali inajengwa na mchina, au sisi wenyewe au kwa kukopa fedha kutoka kokote kule!
 
Mkuu, naungana nawe kwenye hili la kuanza kujenga wenyewe bandari kwa uwezo tutakaokuwa tunauweza wenyewe. Kamwe haiwezi kuchukua miaka 30, kwani uwezo wetu utakuwa ukiongezeka kadri uchumi wetu unavyozidi kukua, na hata mikopo nafuu tunaweza kuitumia katika ujenzi huo.

Zaidi ya hivyo, tukishaanza ujenzi wenyewe, mvuto wa bandari hiyo utawaleta tu washiriki wengine, hata hao wachina watakuja na tutawapa masharti tofauti na haya wanayotuwekea sasa.

Tukiacha woga na kuwa na msimamo wa kufanya mambo kwa ufanisi tunaweza kufanya mambo makubwa sana kuendeleza nchi yetu sisi wenyewe.

Lakini kwa nini hatujiulizi: wao wachina ni nani aliyewajengea miundo mbinu yao mingi? Mbona sasa wao ndio wajenzi duniani kote?
 
Ungekuwa umesoma bandiko langu kwenye mada hii ungejua hiyo $16 nimeipata wapi. Mimi sikuibuni, ni taarifa zilizochapichwa 'widely' kwenye magazeti wakati rais wetu Hassan alipokwenda Uganda kukamilisha majadiliano wa ujenzi wa bomba hilo la mafuta.

Hilo la "uzuri sana wa mradi..." ni swala tofauti kabisa hoja iliyosababisha niandike jibu hilo kuhusu $16.

Tunaweza pia kujadili juu ya hilo nje ya mada hii.

Kwa mfano, hela itakayokuwa inapatikana kutokana na mradi huo wa bomba, haiwezi kusaidia ujenzi wa bandari, kama tukiamua kufanya hivyo?
 
Mkuu ni dola 12 sio 16 kwa pipa.
Mkuu, hata hizo dollar 12 bado ni uongo.

Imagine, sisi kupitisha Bomba tu tupate dollar 12 kwa pipa. Sasa Uganda watapata kiasi gani? Let assume wanapata double of what we get.... Hiyo itakuwa tayari ni nusu ya bei kwenye world market. Kwa hiyo unataka kusema mwekezaji anapata less...!!? Kwa mtaji huo basi tutakuwa tume hit a jackpot.... Hiyo itakuwa kwenye ndoto tu.

Last year May bei ilikuwa ilikuwa below 20, sasa imagine mbomba linvezalisha kiasi gani? Here my point is bei haviwezi kuwa fixed kama tunavyotaka kuaminishwa na MATAGA.
 
Ungesoma wala usingenidai mkataba!!!

Pili, wapi kwenye hiyo quote inaposeama China anataka kuwa dereva?!

Let's umeamua kutafsiri neno kwa neno... sasa tangu lini Drivers ikawa ni Dereva?! China ni mmoja, na singular, sasa kwanini watumie neno Drivers badala ya Driver?

Halafu unasema mbona hapo kwenye "new drivers" nimeacha! Hivi kile nilichoandika kinafanana kweli kwamba nimetafsiri kauli hiyo ya Xi?

Hiyo quote inaonesha lengo la China la promote international cooperation, ushirikiano ambao wanaamini utaunda waendeshaji wapya wa maendeleo ya pamoja!

HOW!

Sio siri kwa East Africa Kenya ndie Driver of the economy in the region!! Sasa China na TZ wakishirikiana kupitia BRI, na malengo yakafinikiwa, huoni a new driver of shared development atakuwa amepatikana in East Africa?

Najua it's too good to be true lakini kama mpango wa Bagamoyo ungefanikiwa kama watu walivyokuwa wanaota, basi Tanzania tungewaacha hata South Africa! Sasa hujaona a new drive in Africa amekuwa created?

What kama kwenye miradi yake mingine, kule Djibouti, Angola na kwingineko na yenyewe inatusua! Huoni hapo new drivers of the maendeleo watakuwa wameibuka!!!
 
Mkuu, kwa vile hatujui mkataba yote tunayoambiwa Inawezekana kabisa siyo kweli. Wengi wetu tu naamini kuwa Mwendazake alikuwa Mzalendo na mkweli kwenye hii mikataba. Tatizo hauna prove yeyote... Tuliamini maneno yake tu.

Pia kujenga bandari haina guarantee yeyote kuwa italipa. Hii biashara inahitaji other connections na kuna other influences. Kwa mfano toka tupanue bandari ya Dar, biashara imeongezeka kwa kiasi gani? The insiders hawawezi kukujibu hilo zaidi ya kupolitisize!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…