Mabeberu, Vibaraka wa Mabeberu, Wazalendo wa Hayati Magufuli, na Mradi wa Bandari ya Bagamoyo

Serikali ipi unayotaka iaminike?!

Huyo Kakoko mwenyewe ana tuhuma za wizi, na ndio maana kasimamishwa! Sasa unataka tumwamini mtu mwenye tuhuma za wizi?!
Sasa weka wewe mkataba basi tuuuone ili kumkata kabisa ngebe za kakoko na ili kusapoti hii mada yako.
 
Pole sana!!

Kwa mfano, ulitaka niseme kitu positive kipi?! Kununua ndege? Kujenga Chato International Airport?! Kipi hasa ambacho ulitarajia nikiseme?!
Kwa hiyo hayo tu ndio aliyoyafanya tangu awe rais?

Mkuu hivi ndio unataka tukusapoti kwenye hii mada yako kwa mitazamo hii kweli?
 
Mradi wa Bandari wa Bagamoyo ulikuwa na mambo makubwa matatu:-
1. Bandari yenyewe
2. Industrial Park
3. SGR kutoka Bagamoyo to the main SGR line!
Mradi una mambo matatu, umejuaje?

MWONGO MKUBWA!

Umejuaje contents za mkataba bila mkataba?

TUNATAKA KUUONA MKATABA!
 
Mradi una mambo matatu, umejuaje?

MWONGO MKUBWA!

Umejuaje contents za mkataba bila mkataba?

TUNATAKA KUUONA MKATABA!
Toka kule juu page ya kwanza watu wamedai aweke mkataba hapa ila anajibu blaa blaa
 
Muongozo mkuu wa miradi ni Mkataba, bila mkataba kuhusishwa hata ukiandika maneno matamu kiasi gani bado yanakuwa hayana maana.
 
Kwa hiyo hayo tu ndio aliyoyafanya tangu awe rais?

Mkuu hivi ndio unataka tukusapoti kwenye hii mada yako kwa mitazamo hii kweli?
Hapa chini ni hoja niliyotoa miaka 3 iliyopita kuhusu SGR!

Again, pole sana kwa hayo mawazo yako kwamba mtu akimpinga jambo la JPM basi ana chuki na JPM!!!

Lakini siwezi kuwa mjinga wa kuunga mkono ununuzi wa ndege!

Siwezi kuwa mjinga wa kuunga mkono ujenzi wa Uwanaja wa Ndege wa Kimataifa eneo ambalo halina sifa hizo!!

Hata alipojenga hospitali ya rufaa Chato, hoja yangu haikuwa ujenzi wa hospitali bali kwanini asingejenga Geita iliyo katikati ya mkoa na kwenda kujenga chato ambayo ipo pembezoni kabisa mwa mkoa!!

Na hata lilipokuja suala la CRDB Chato miaka 3 iliyopita, hoja yangu ilikuwa hii hapa:-
Kwa mara nyingine, pole sana!!!

Hizo fikra zako za kudhani watu tunamchukia JPM zitakuzeesha kaba ya wakati wako kwa sababu, yale ambayo hatukukubaliana nae, watu tutaendelea kuandika, na wewe utaendelea kutoa povu!!!
 
MAPENDEKEZO

Reserved for later
Sawa sawa mkuu (nasikilizia mapendekezo yako)

ila binafsi, nasema kitu kimoja tu katika hili sakata:

maendeleo yawe kwa nchi (1) na wananchi (2)

kuna mijitu kila kona wapo! wale wa 'unanijua mimi ni nani?' kisa Mh. Rais anamsikia(na sio kumjua). huu ushamba uishe sasa.

kuna kampuni nyingi za kigeni ambazo zilikuja na kutaka kujikita kwenye maswala ya infrastructure zilisepa. they counted and weighed their losses wakaona ni uendawazimu. maana ofisi za mabalozi wanatangaza fursa hii wakati on ground ni utumbo mwingi na ukaangaji wa maini. kuna mabalozi wenye heshima zao walioneka bure kutokana na utendaji nchini pale mwekezaji anapoingia.

wajenge wasijenge, taratibu zifatwe na vyombo husika vichunguze kampuni na viongozi wa makampuni hayo na pale inaonekana kuna jambo sio sahihi, watu wawe bold kusema. bila kumuogopa mtu kwani ujenzi wa leo ni kwa manufaa na matumizi ya vizazi vijacho. maana kama jiwe alivyosema, unaweza kutaka kuchukua ng'ombe wako pale ambapo simba kashambana na ukajeruhiwa pamoja na kwamba ni mali yako!

miradi mingi ya Tanzania imekua kituko. Hebu angalia mwendo kasi, pale bonde la msimbazi, ni nini kile kama sio uchafu. na anayedhalilika ni kiongozi wa nchi kwani watendaji wake wakishapata chao, wao ni matumbo yao na familia zao. mwisho wa siku kiongozi unaonekana kituko.

bado watanzania (wengi) hatujastaarabika, kutoka viongozi mpaka wananchi! kila mnapoenda kwenye nchi zilizoendelea mnang'atuka meno na ku-admire ya wenzenu, wakirudi nyumbani mziki ni ule ule.

tubadilike! nchi isiwe shamba la bibi...

waweke mikataba wazi, vyombo kama takukuru wahusike!

it's high time our nation benefits and reaps from the fruits that she bares for the benefit of all not a few!
 
Nami nakuuliza kwa mara ya pili, kwa akili yako kubwa sana ni hayo tu ndio JPM kalifanyia hili taifa,,?

Tukirudi kwenye mada,..

Kwanini usitimize takwa la wengi kwenye huu uzi wako wa kisomi kwa kuweka mkataba hadharani na ili tuzidi kumdharau sana huyu JPM?
 
Kwahiyo unataka nianze kujadili yooote aliyofanya JPM, ninayoyaunga na nisiyoyaunga mkono?! Nimekutajia miradi ya JPM ambayo watu wenye chuki nae tumekuwa tunaipinga... mbona unashindwa kuelewa?

Halafu acheni kujificha kwenye mkataba kwa sababu tu hamna hoja!!!

Nimekuuliza, Kakoko aliyewaambia Wachina wanataka kusamehewa kodi kwa miaka 30, amekuonesha huo mkataba?

Ikiwa hata huko bungeni Wabunge wamekuwa wakililia kupewa mikataba na hawapewi, halafu unataka huo mkataba nikuwekee mimi JF?

Upo serious kujadili mada wewe?!

Hoja zangu zinajadilika bila kuona mkataba kwa sababu ni matokeo ya research!!!
 
Mradi una mambo matatu, umejuaje?

MWONGO MKUBWA!

Umejuaje contents za mkataba bila mkataba?

TUNATAKA KUUONA MKATABA!
Nimeshasema huna hoja, so stop wasting my time!! Huwezi kushindwa kujadili mada eti kisa hakuna mkataba wakati tangu umezaliwa hujawahi kujadili mada yenye mkataba hapa JF!!

Na ikiwa unashindwa kujua hata mambo madogo kama hayo ambayo yameshawekwa wazi tangu zamani, si itakuwa kupotezeana muda tu kuendelea kujadiliana na mtu wa aina yako!
 
Kwa vile kakoko hajaweka mkataba akaja na blaa blaa..

Wewe hujaweka mkataba umekuja na blaa blaa..

Wote nyie ni wa kupuuzwa..
 
Mtaleta hoja nyingi zenye kila aina ya rangi lakini hicho unachokitetea hakina tija. Weka kataba wake hapa sio kuleta porojo za utafiti feki na makala zilizojaa hisia binafsi kutokana na maslahi uliyokuwa nayo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…